TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,563
Kwaio wewe unataka raisi awe nani labda
Rostam Aziz,Andrew Chenge,Nazir Karamagi=Edward Ngoyai Lowassa.Ndio mnataka tuwakabidhi nchi hawa? Zinachaji kichwani kweli nyinyi?
Kwaio wewe unataka raisi awe nani labda
![]()
Watanzania wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanaaminishwa kuwa ana maono ya kiuongozi ambayo yakitumika yanaweza kulinasua taifa letu toka hapa lilipo. Wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa ni kiongozi bora ambaye Watanzania wanapaswa kumwangalia kwa matumaini - ndio maana ya "safari ya matumaini".
Wapo kati yetu ambao wameshazugika na pendekezo hilo na wamekuwa kama waliorogwa hivi. Wapo baadhi yetu kwa muda wote wa uongozi wa Lowassa (hasa baada ya kuwa Waziri Mkuu na baadaye) tuliona kile ambacho labda kimefichika kwa wengi - Lowassa hafai. Hii si hukumu juu ya utu wake, heshima au ubinadamu wake; ni hukumu juu ya uongozi wake na maono yake kama kiongozi. Kumkataa Lowassa, maono yake, uongozi wake na fikra zake siyo kumchukia yeye kama Mtanzania mwenzetu au kama binadamu. Ni kuwa na tofauti naye na vile anavyowakilisha kiasi kwamba tofauti hizo hazijawezi kupatana (irreconcilable differences). Katika siasa ni lazima tuheshimu uwepo wa tofauti hizi na tuelewe ndio msingi wa kutafuta viongozi bora zaidi au chama bora. Kwa kadiri yeye atakavyojaribu kujiuza ndivyo na sisi wengine tutazidi kuonesha kuwa hauziki au zaidi hanunuliki. Hii si chuki ni tofauti tu ya msingi (fundamental difference).
Pendekezo langu linatokana na hili; kwamba zipo na zimedumu tofauti za msingi kati ya maono ya baadhi yetu na maono ya mgombea huyu mtarajiwa kutoka CCM. Tanzania haiitaji maono na uongozi wa Lowassa kwa sababu nyingi tu; nitaanza na moja ya leo na nitaendelea kwenye mada hii hii kila ninapopata nafasi hadi jina lake litakapotupwa na NEC na yeye akaendelea kuwa Waziri Mkuu wa zamani.
Mara kwa mara baada ya sakata lake na katika jitihada za kujirudisha katika umuhimu (relevance) Lowassa amekuwa akizungumzia mwelekeo wa sera zake na kitu kitakachomuongoza. Aliamua kwenda kinyume na mwelekeo wa serikali ya chama chake ambayo iliweka mkazo kwenye "Kilimo Kwanza"; yeye ameamua kuja na hoja ya "Elimu Kwanza".
Alielezea kupinga kwake hoja ya Kilimo Kwanza miaka michache nyuma alipohojiwa katika kipindi cha Dakika45 (kinachorushwa na ITV). Alinukuliwa kusema "Mpango huu wa Kilimo Kwanza umekosa nguvu kwa sababu kuanzishwa kwake hakukuzingatia dhana ya ukombozi wa mwananchi wa kawaida. Tangu awali ndani ya chama (CCM) nilieleza kuwa sitaunga mkono hoja hiyo mpaka kuongezwe mashiko na kuwa Elimu Kabla ya Kilimo Kwanza"
Hoja hii ameirudia tena juzi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ambao bila ya shaka wengi wamekuwa 'charmed' na wingu la umaarufu wa Lowassa kiasi kwamba hakuna ambaye ameweza kumbana vizuri kwenye maswali. Anasema endapo atachaguliwa basi ataelekeza nchi kwenye "elimu kwanza"; kwamba hiki ndicho kipaumbele chake.
Ndio maana sisi wengine tunasema hafai; kwa sababu inaonekana siyo yeye wala chama chake ambao wamelielewa vizuri tatizo linaloikabili Tanzania; tatizo ambalo limeielekeza (orient) Tanzania kufuata njia ya Nigeria. Kwamba tunaweza kabisa kutengeneza uchumi wenye nguvu lakini wa taifa lenye umaskini uliokithiri, lisilo na usawa na la wasomi wasioweza kulipeleka taifa mbele. Tutakishia kujisifia wingi wa wasomi ambao wengi wataishia kwenda nje ya nchi kutafuta maisha. Taifa ambalo litakuwa limegawanyika sana kama Nigeria - licha ya kuwa na wasomi wengi.
Lowassa inaonekana ameshindwa kuelewa au hataki kukubali kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni la aina tatu:
1. Ufisadi
2. Ufisadi
3. Ufisadi
Lowassa hatopambana na ufisadi kwa uzito unaostahili kwani haoni kuelewa kuwa ni tatizo la hatari zaidi kwa taifa "kuliko vita wakati wa amani" kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Kutokuelewa kuwa Ufisadi ndiyo sekta haramu yenye nguvu zaidi katika nchi yetu ni kushindwa kuelewa tatizo letu hasa ni nini. Ufisadi umepenya (permeate) kwenye kila sekta nyingine zote (rasmi na zisizo rasmi). Umeathiri elimu, afya, usalama, na hata umoja wa taifa. Kutokulielewa tatizo hili kwa mtu anayetaka kugombea nafasi ya Urais (haijalishi anatokea chama gani) ni kutokuelewa namna ya kukabiliana na changamoto nyingine zote.
Kwa sababu hii peke yake Lowassa na mgombea mwingine yeyote ambaye haweki "ufisadi" kama ajenda yake ya kwanza na kubwa zaidi basi hafai. Kwa sababu atatuzungusha kwenye madudu mengine yote isipokuwa kwenye kumkoma nyani giledi. Kikwete - kwa wanaokumbuka - alishabikiwa na wengi si kwa sababu ya "Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya" bali zaidi kwa kuwapa Watanzania matumaini kuwa atashughulikia ufisadi vikali. Hotuba yake ya kulifungua Bunge na ile ya Ngurdoto na zile ziara zake za kutembelea Wizara ziliwafanya watu waamini kidogo kuwa hatimaye "kipele kimepata mkunaji". Leo hii miaka tisa baadaye ripoti ya CAG imeonesha kidogo tu kuwa tatizo hili la ufisadi halijapata mtatuzi ndani ya CCM na hata mtu anayeshabikiwa sana kuwa ati anaweza kuwa Rais inaonekana tatizo hili limempita kabisa.
Nikisema "hafai" simsingizii; nasema kilicho dhahiri; I'm just stating the obvious.
Wanaomtaka Lowassa - wapenzi, mashabiki na waumini wake - watuambie vita dhidi ya ufisadi ina umuhimu na uzito gani katika agenda za Lowassa. Wakituambia kuwa "ni mojawapo" ya mambo atakayoyashughulikia tuendelee kumkataa kwa sababu bado atakuwa hajaelewa tatizo letu hasa ni nini kama taifa.
Nitandelea...
NB: Kwa wageni wa hoja hizi warejee mada yangu ya 2007: Kikwete Siyo Safi, Yes I said it
Elimu jimboni kwake imemshinda , ataiweza nchi Nzima? Huyu mamvi
![]()
Watanzania wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanaaminishwa kuwa ana maono ya kiuongozi ambayo yakitumika yanaweza kulinasua taifa letu toka hapa lilipo. Wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa ni kiongozi bora ambaye Watanzania wanapaswa kumwangalia kwa matumaini - ndio maana ya "Safari ya Matumaini".
Wapo kati yetu ambao wameshazugika na pendekezo hilo na wamekuwa kama waliorogwa hivi. Wapo baadhi yetu kwa muda wote wa uongozi wa Lowassa (hasa baada ya kuwa Waziri Mkuu na baadaye) tuliona kile ambacho labda kimefichika kwa wengi - Lowassa hafai.
Hii si hukumu juu ya utu wake, heshima au ubinadamu wake; ni hukumu juu ya uongozi wake na maono yake kama kiongozi. Kumkataa Lowassa, maono yake, uongozi wake na fikra zake siyo kumchukia yeye kama Mtanzania mwenzetu au kama binadamu. Ni kuwa na tofauti naye na vile anavyowakilisha kiasi kwamba tofauti hizo hazijawezi kupatana (irreconcilable differences).
Katika siasa ni lazima tuheshimu uwepo wa tofauti hizi na tuelewe ndio msingi wa kutafuta viongozi bora zaidi au chama bora. Kwa kadiri yeye atakavyojaribu kujiuza ndivyo na sisi wengine tutazidi kuonesha kuwa hauziki au zaidi hanunuliki. Hii si chuki ni tofauti tu ya msingi (fundamental difference).
Pendekezo langu linatokana na hili; kwamba zipo na zimedumu tofauti za msingi kati ya maono ya baadhi yetu na maono ya mgombea huyu mtarajiwa kutoka CCM. Tanzania haihitaji maono na uongozi wa Lowassa kwa sababu nyingi tu; nitaanza na moja ya leo na nitaendelea kwenye mada hii hii kila ninapopata nafasi hadi jina lake litakapotupwa na NEC na yeye akaendelea kuwa Waziri Mkuu wa zamani.
Mara kwa mara baada ya sakata lake na katika jitihada za kujirudisha katika umuhimu (relevance) Lowassa amekuwa akizungumzia mwelekeo wa sera zake na kitu kitakachomuongoza. Aliamua kwenda kinyume na mwelekeo wa serikali ya chama chake ambayo iliweka mkazo kwenye "Kilimo Kwanza"; yeye ameamua kuja na hoja ya "Elimu Kwanza".
Alielezea kupinga kwake hoja ya Kilimo Kwanza miaka michache nyuma alipohojiwa katika kipindi cha Dakika45 (kinachorushwa na ITV). Alinukuliwa kusema "Mpango huu wa Kilimo Kwanza umekosa nguvu kwa sababu kuanzishwa kwake hakukuzingatia dhana ya ukombozi wa mwananchi wa kawaida. Tangu awali ndani ya chama (CCM) nilieleza kuwa sitaunga mkono hoja hiyo mpaka kuongezwe mashiko na kuwa Elimu Kabla ya Kilimo Kwanza"
Hoja hii ameirudia tena juzi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ambao bila ya shaka wengi wamekuwa 'charmed' na wingu la umaarufu wa Lowassa kiasi kwamba hakuna ambaye ameweza kumbana vizuri kwenye maswali. Anasema endapo atachaguliwa basi ataelekeza nchi kwenye "elimu kwanza"; kwamba hiki ndicho kipaumbele chake.
Ndio maana sisi wengine tunasema hafai; kwa sababu inaonekana siyo yeye wala chama chake ambao wamelielewa vizuri tatizo linaloikabili Tanzania; tatizo ambalo limeielekeza (orient) Tanzania kufuata njia ya Nigeria. Kwamba tunaweza kabisa kutengeneza uchumi wenye nguvu lakini wa taifa lenye umaskini uliokithiri, lisilo na usawa na la wasomi wasioweza kulipeleka taifa mbele. Tutakishia kujisifia wingi wa wasomi ambao wengi wataishia kwenda nje ya nchi kutafuta maisha. Taifa ambalo litakuwa limegawanyika sana kama Nigeria - licha ya kuwa na wasomi wengi.
Lowassa inaonekana ameshindwa kuelewa au hataki kukubali kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni la aina tatu:
1. Ufisadi
2. Ufisadi
3. Ufisadi
Lowassa hatopambana na ufisadi kwa uzito unaostahili kwani haoni kuelewa kuwa ni tatizo la hatari zaidi kwa taifa "kuliko vita wakati wa amani" kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Kutokuelewa kuwa Ufisadi ndiyo sekta haramu yenye nguvu zaidi katika nchi yetu ni kushindwa kuelewa tatizo letu hasa ni nini. Ufisadi umepenya (permeate) kwenye kila sekta nyingine zote (rasmi na zisizo rasmi). Umeathiri elimu, afya, usalama, na hata umoja wa taifa. Kutokulielewa tatizo hili kwa mtu anayetaka kugombea nafasi ya Urais (haijalishi anatokea chama gani) ni kutokuelewa namna ya kukabiliana na changamoto nyingine zote.
Kwa sababu hii peke yake Lowassa na mgombea mwingine yeyote ambaye haweki "ufisadi" kama ajenda yake ya kwanza na kubwa zaidi basi hafai. Kwa sababu atatuzungusha kwenye madudu mengine yote isipokuwa kwenye kumkoma nyani giledi.
Kikwete - kwa wanaokumbuka - alishabikiwa na wengi si kwa sababu ya "Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya" bali zaidi kwa kuwapa Watanzania matumaini kuwa atashughulikia ufisadi vikali. Hotuba yake ya kulifungua Bunge na ile ya Ngurdoto na zile ziara zake za kutembelea Wizara ziliwafanya watu waamini kidogo kuwa hatimaye "kipele kimepata mkunaji". Leo hii miaka tisa baadaye ripoti ya CAG imeonesha kidogo tu kuwa tatizo hili la ufisadi halijapata mtatuzi ndani ya CCM na hata mtu anayeshabikiwa sana kuwa ati anaweza kuwa Rais inaonekana tatizo hili limempita kabisa.
Nikisema "hafai" simsingizii; nasema kilicho dhahiri; I'm just stating the obvious.
Wanaomtaka Lowassa - wapenzi, mashabiki na waumini wake - watuambie vita dhidi ya ufisadi ina umuhimu na uzito gani katika agenda za Lowassa. Wakituambia kuwa "ni mojawapo" ya mambo atakayoyashughulikia tuendelee kumkataa kwa sababu bado atakuwa hajaelewa tatizo letu hasa ni nini kama taifa.
Nitandelea...
NB: Kwa wageni wa hoja hizi warejee mada yangu ya 2007: Kikwete Siyo Safi, Yes I said it
Mimi sina chama ila najua kupitia UKAWA na ndani ya CCM pia kuna watu makini sana tu wanaweza kwa ukamilifu kutuongoza kujenga Nchi yenye maziwa na asali..lakini cha kwanza kabla ya vyote UFISADI NA RUSHWA viondoke ndani ya ofisi za serikali, Binafsi, Majumbani mwetu, ndani ya mifuko ya rafiki zetu, matajri, wanasiasa na umma kwa ujumla wake.ndani ya ccm hakuna mwenye uwezo wa kumwonyeshea kidole mwenzake wote hawafai.
VOTE FOR UKAWA.
Kwaio wewe unataka raisi awe nani labda
Mimi naenda mbali zaidi na kusema kuwa CCM yote haifai kuchaguliwa tena.
Swali ni je, ni nani anayefaa zaidi ya CCM?
Kamwe hautapata jibu...Mimi naenda mbali zaidi na kusema kuwa CCM yote haifai kuchaguliwa tena.
Swali ni je, ni nani anayefaa zaidi ya CCM?
Mkuu
Kukaa kimya Watanzania wakilishwa peremende badala ya mlo si kuwatendea haki.
Jana nilikuwa naangalia BBC nikaona mgao wa mafuta katika taifa mwanachama wa OPEC Nigeria.
Sababu kubwa ni kutokana na ufisadi ambao umefikia mahala pa kuiweka serikali mateka
Kwa wasioona wanaweza kudhani hilo lipo Nigeria na kwingine. Guess what! anayedhani hivyo anahitaji msaada wa wataalamu wa macho, masikio, akili na ubongo. Tatizo lipo nchini na linaimarika kila siku
Ukubwa wake nchini ni zaidi ya Nigeria. Kule Nigeria tunafahamu ufisadi na utapeli ni sehemu ya maisha (norm)
Hapa kwetu limeingia kwa kasi kiasi kwamba, mafisadi wananunua hata hivyo, wakichagua nani aende Ikulu nani
Katika mkutano wa juzi Lowassa ametusaidia sana hasa wasiomjua. Ameeleza kuwa pesa anazopata zinatoka kwa marafiki zake. Utaratibu wa nchi yetu vyama hudhamini watu wao na kuendesha kampeni kwa niaba ya mgombea wao. Ndilo chimbuko la ruzuku za vyama vya siasa. Sasa Lowassa anapotuambia anachangiwa na marafiki zake, je huo ndio utaratibu wa CCM wa siku hizi? Kwanini hakusimama ili sheria ya mgombea binafasi kama yeye pite? Marafiki zake ni akina nani, wanamchangia ili iweje?
Kuhusu suala la Elimu, akiwa mbunge hakuna kumbu kumbu zinazoonyesha kama aliwahi kupingana na chama chake ndani ya vikao kuhusu kilimo kwanza au elimu kwanza. Pengine ushahidi mzuri ungekuwa yeye kujiuzulu nafasi za uongozi kupinga sera zisizo sahihi. Hakufanya hivyo. Leo anaingia na sera yake binafasi
Hapa anatuambia, anachotaka kufanya si sera za wana CCM bali ana zake. Sasa ukichanganya na hoja ya kuchangiwa na marafiki, hakuna shaka kuna 'kachama' kake pembeni kanakohitaji 'label' au logo ya CCM
Hii ndiyo CCM tunayoambiwa?
Lakini pia, tunataka EL atuambie, anasimama vipi katika ufisadi ambao ni tatizo linalodumaza Kilimo kwanza na Elimu kwa upana wake? Huwezi kufanikisha sera ya elimu ukiwa umefungwa mikono na miguu na mafisadi waliowekeza kukupeleka Ikulu
Tuna mahali pa kuanzia na si kutekwa na wafanyakazi wanaoaminisha umma, anafaa bila kutueleza kivipi.