Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

umetoa mfano wa nigeria na kutaka kuaminisha watu.kua ati elimu haitoweza.kuinua hali za watu bali itazalisha zaidi wasomi ambao mwisho watamalizia jela au kuikimbia nchi. mbona hutoi mifano ya nchi nyingi.ambazo zimefanikiwa kama uk malaysia singapore south korea na nyingi kwa kuweka mbele elimu kwanza.

Naomba nijibu hoja hii kwanza na utaona kwanini msimamo wangu ni sahihi na wa kwako umepotoka. Malaysia ni kweli inaonekana imefika mbali sana kiuchumi. Lakini sijui kama unajua kuwa sasa hivi ni nchi inayoongoza kwa ufisadi huko Asia. Malaysia unayoizungumzia wewe ni ile ya wakati wa Mahathir; ambapo ndio nchi ilijengwa hasa hasa. Hivi juzi tu (April) Mahathir mwenyewe amejitokeza na kukemea uongozi wa nchi yake kwa kuwa sasa Malaysia inatajwa kuwa ni nchi ya kifisadi zaidi duniani! SOMA HAPA HILO

Halafu wana elimu!!! Kama elimu ingekuwa ni tiba ya ufisadi Malaysia isingekuwa hapo. Leo hii Malaysia inavuna baadhi ya mbegu ambazo wengi wanaamini zilipandwa wakati wa Waziri Mkuu Mahathir mwenyewe.

Singapore nayo ni hivyo hivyo. Ni kweli ukiangalia kwa nje ni taifa lenye uchumi wenye nguvu sana Mashariki Kusini mwa Asia. Lakini nayo - pamoja na usomi wake wote - imezama kwenye mambo ya ufisadi. Hili unaweza kulifanyia utafiti wewe mwenyewe na utaona. Mwaka 2012 tu Indonesia imepoteza zaidi ya dola milioni 230 kwenye kashfa mbalimbali za ufisadi.

Umeitaja na Korea ya Kusini na hiyo utaona inathibitisha hoja yangu kuliko ya kwako. South Korea wanapambana na ufisadi kuliko hizo nchi nyingine ulizozitaja (ukiondoa UK). Lakini hata hiyo nayo imeshagubikwa na kashfa kadhaa kubwa tu za ufisadi. Lakini Korea imewashughulikia mafisadi wake bila kujali sura zao na kesi zilishaisha zamani. Kuanzia mawaziri na hata marais wa nyuma; tena wao hawana aibu hata kwa kesi za mambo yaliyopita wameyashughulikia. Mwaka juzi tu hapa maofisa wa uchunguzi walivamia ofisi ya Waziri wa Mambo ya Nje wakichunguza tuhuma za ufisadi - fikiria kitu kama hicho kuweza kutokea Tanzania!

Mtu wa Pwani, tunaposema tatizo kubwa letu ni ufisadi hatusemi kwa hisia tu. Na mnaosema ni elimu nadhani hamjakaa chini kufikiria vizuri maana yake nini. Elimu ingekuwa inapunguza ufisadi mafisadi wangepungua duniani!
 
Lose or win i will vote for lowasa.

labda ungesema "afae au asifae nitampigia kura Lowassa". Hapo utakuwa umechukua uamuzi wa dhamira yako. Kwani utakuwa umepiga kura bila kujali habari sahihi (facts).
 
Mwanakijiji

Tatizo la Tanzania siyo ufisadi bali ni ukose wa elimu ambayo humwezesha mtu kutofautisha aliye msafi na fisadi. Upinzani kwa zaidi ya miaka tano imekuwa ikipiga kelele kuhusu ufisadi lakini ikifika uchaguzi wananchi wanashiriki kwenye ufisadi kuchagua mafisadi.

Kumbuka Elimu ni maarifa ya kutambua ambalo ulikuwa hulitambui na kutatua matatizo ya jamii.

Bila elimu bora na yenye kujumlisha utu, bado watanzania wataendelea kuona mwizi kama shujaa na wapiga dili kama watu wajanja.

Hata sasa hivi wananchi wanakosa namna ya kutofautisha Lowasa na wengine kwa sababu ya kukosa elimu.

Elimu itasaidia watanzania kujitambua.
 
nchi hii ina kila kitu na isipokuwa uongozi bora namaanisha maadili ndo kilio chetu kikubwa so kusema El tumpe nchi inahitaji kwanza uwe umejitoa ufahamu au umepigwa sindano ya ganzi ndo useme huyu jamaa anafaa
 
Naomba nijibu hoja hii kwanza na utaona kwanini msimamo wangu ni sahihi na wa kwako umepotoka. Malaysia ni kweli inaonekana imefika mbali sana kiuchumi. Lakini sijui kama unajua kuwa sasa hivi ni nchi inayoongoza kwa ufisadi huko Asia. Malaysia unayoizungumzia wewe ni ile ya wakati wa Mahathir; ambapo ndio nchi ilijengwa hasa hasa. Hivi juzi tu (April) Mahathir mwenyewe amejitokeza na kukemea uongozi wa nchi yake kwa kuwa sasa Malaysia inatajwa kuwa ni nchi ya kifisadi zaidi duniani! SOMA HAPA HILO Halafu wana elimu!!! Kama elimu ingekuwa ni tiba ya ufisadi Malaysia isingekuwa hapo. Leo hii Malaysia inavuna baadhi ya mbegu ambazo wengi wanaamini zilipandwa wakati wa Waziri Mkuu Mahathir mwenyewe. Singapore nayo ni hivyo hivyo. Ni kweli ukiangalia kwa nje ni taifa lenye uchumi wenye nguvu sana Mashariki Kusini mwa Asia. Lakini nayo - pamoja na usomi wake wote - imezama kwenye mambo ya ufisadi. Hili unaweza kulifanyia utafiti wewe mwenyewe na utaona. Mwaka 2012 tu Indonesia imepoteza zaidi ya dola milioni 230 kwenye kashfa mbalimbali za ufisadi. Umeitaja na Korea ya Kusini na hiyo utaona inathibitisha hoja yangu kuliko ya kwako. South Korea wanapambana na ufisadi kuliko hizo nchi nyingine ulizozitaja (ukiondoa UK). Lakini hata hiyo nayo imeshagubikwa na kashfa kadhaa kubwa tu za ufisadi. Lakini Korea imewashughulikia mafisadi wake bila kujali sura zao na kesi zilishaisha zamani. Kuanzia mawaziri na hata marais wa nyuma; tena wao hawana aibu hata kwa kesi za mambo yaliyopita wameyashughulikia. Mwaka juzi tu hapa maofisa wa uchunguzi walivamia ofisi ya Waziri wa Mambo ya Nje wakichunguza tuhuma za ufisadi - fikiria kitu kama hicho kuweza kutokea Tanzania! Mtu wa Pwani, tunaposema tatizo kubwa letu ni ufisadi hatusemi kwa hisia tu. Na mnaosema ni elimu nadhani hamjakaa chini kufikiria vizuri maana yake nini. Elimu ingekuwa inapunguza ufisadi mafisadi wangepungua duniani!
ndugu yangu kila nikiendelea kusoma hoja zako juu ya hili nnaona zaidi chuki na muhemko tu ndio inayokuongoza.ufisadi ni suali mtambuka, ni jambo ambalo lipo kwa mataifa yalio na yasio na elimu. yaliotoa kipaumbele kwa ufisadi ama la. hujaja na hata nchi moja ambayo imefanikiwa moja kwa moja na hamna ufisadi.pili hujanionyesha trend za nchi nilizokutolea mfano kua zimefanikiwa kwa kutoa kipaumbele kwenye hali ya ufisadi ilikuwaje kabla kuimplement hizo policy na baadae kwa nn ?jee huwezi kusema kua kwa kua wananchi wengi wanajielewa imekua rahisi sasa kuona ufisadi kwa macho mawili na kua na ujasiri wa kuusemea na kupambana nao kwa kua wana elimu na ujuzi wa kuutambua ?mheshimiwa lowassa kwa nilivyomfahamu kipao mbele chake kikuu ni elimu na sio kua hatopambana na ufisadi au kuhakikisha afya na bara bara haziko vyema. nilivyomuelewa taifa likiwa na knowledge base ilioandaliwa vyema ni rahisi sana kutatua matatizo yakeleo kwa ukosefu wa hilo ni rahisi kina mwanakijiji na wenzake kutulisha kasumba, kutuaminisha huyu fisadi huyu hapana.wale jana walitwambia cuf ccm b leo cuf jembe. wananchi kwa ukosefu wa elimu wamekuwa muhanga wa kutumiwa na wachache.hatutaki taifa la magoi goi, kina mwanakjj na wenziwe wachache wanatulisha kasumba na kutuchanganya, tunahitaji taifa ambalo watu wake wengi wanajielewa kuanzia vijijini hadi mijini. nchi ikiwa elimu iko juu, ni rahisi kupambana na mengi ikiwemo ufisadi, rahisi kutengeneza ajira, hata kuwa na kilimo kilicho imara. huwezi kupeleka matrekta na vifaa vya kilimo kwa watu wasio na uelewa na mbinu za kisasa.kwa hili lowassa yuko sawa, elimu kwanza mengine yanafuata.na kuhusu kupambana n ufisadi nani asiejua vp ktk kipindi kifupi alichokaa aliwanyoosha watendaji na kuzuia upotevu na utafunaji wa pesa za serikali, hivi hili pia hujaliona?ukiacha kesi ya richmond lete jambo lingine ambalo unaweza kumnyooshea kidole lowassa
 
Mwanakijiji

Mie nafikiri hoja yako haina mashiko, mie nashawishika kuamini kua wewe mwenyewe hulijui tatizo la Tanzania na kama unalifahamu basi correlation ya vimeng'enya vyake ume fail kwa nyuzi za juu kabisa katika mfumo wa mmeng'enyo wa uchambuzi wako.

Namba aushi ulizotabanaisha kwa kuzipigilia mstari kwamba ndo tatizo kuu, nafikiri hazina uwiono na tija murua ambazo kwayo zinaweza tumika ili kuuwezesha uchumi wa Tanzania kushika mchapuko chanya.

Nafikiri na pia naamini ungejielimisha tofauti ya root causes na outcomes/results. Na bado pia naamini unachoongelea yani ufisadi ni results yani ni matokeo. Sasa utayazuia vipi matokeo, ni kutafuta source yake yani root cause. Ehe na root cause ya ufisadi ni nini ni ELIMU MBOVU.

Ukiwa na Taifa la watu wenye elimu bora ufisadi unakufa BY DESIGN. Taifa lolote lenye ufisadi lina wananchi ambao wana elimu mbovu. KITUO KIKUBWA. Na taifa lenye elimu mbovu haliwezi kuondoka kwenye umasikini hata kama mna kiongozi Malaika. Mfano Mwl Nyerere alikuwa kiongozi safi sana sio fisadi na mkemea ufisadi, anaweza kuwa nambari moja ama mbili duniani kwa ubora, swali je mbona umasikini ulibaki palepale?

UFISADI linaweza pia kua kikwazo cha maendeleo, lakini pia linaweza kuwa sio kikwazo cha maendeleo utofauti unakuja ni je ufisadi unafanywa na mwenye elimu mbovu ama mwenye elimu nzuri. Mfano Wamarekani/Waingereza na wamagharibi wote wanafanya ufisadi kila sehemu mara Iraq, yemen, Tanzania, nk Je ufisadi wao huu umekuwa ni kikwazo cha maendeleo kwao? Wakoloni walifanya ufisadi sana je ilikuwa ni tatizo la maendeleo kwao? tofauti ni ELIMU.

Yes, Lowasa yuko sahihi, bila elimu bora ufisadi hauwezi kuisha na maendeleo hayawezi patikana.

Mkuu MkamaP,pamoja na mbwembwe nyiingi za kisarufi bado umeenda off base kabisa...umeongea as if una akili kumbe in a nutshell hujui ukisemacho...

Una correlate vipi "tabia" ya wizi na elimu?Wizi ni tabia ovu iliyojengeka moyoni na haijali una degree ngapi kichwani...Inatakiwa juhudi na dhamira safi kumzuia mtu wa namna hii...hapa ni uadilifu,uadilifu hausomewi

Correlation ya elimu na ufisadi uliyotaja haipo,what u are smoking it'sa hell'fa drug!Unasemaje kwa taifa kama Nigeria elimu kubwa ila ufisadi ni no.1?
 
Sasa naona Mzee Mwanakijiji umegeuka kuwa Kijana wa mjini!! dont jump the gun please! naona kama unajaribu kukataa ukweli kwamba ELIMU ndio ufunguo wa maendeleo; Elimu ndio Urithi endelevu! Elimu ndio STOCK IN TRADE ya watu walio wengi nchini mwetu na duniani kote! (msome hayati Lee kuan Yew; Founding father wa Island state ya Singapore; Hayati baba wa Taifa akiita Singapura!; Taifa Mama la dhana ya Matokeo makubwa Sasa;BRN inayowachanganya viongozi wetu wengi!)

Ukimuhukumu EL na kujaribu kushawishi wana CCM; CC; NEC na mkutano mkuu wa CCM "wamchinjilie mbali EL" kisa tu hakutamka kwamba moja ya agenda zake pindi akiteuliwa na hatimaye kuwa rais wa tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ni "Kupambana na Ufisadi; Ufisadi na Ufisadi ni sawa na kutwambia kwamba "kutamka ni sawa na kutenda"!! aaaah wacha masihara Muzee; hiyo miujiza ni ya enzi za Nabii Issa Muzee mwanakijiji!! Wangapi wametamka na wakashindwa kufuatilia kauli zao kwa vitendo!! to talk is one thing; Mzee Mwana kijiji; BUT to walk the talk is quite a different creation Muzee wangu!!!

Hebu rejea kauli hizi: Ari mpya; Nguvu mpya na kasi mpya; tafsiri yake rahisi ni nini?!; Nina list ya Wauza mihadarati wote; wanapeta nje nje! Kinara wa ujangili yuko pale Arusha; lini alikamatwa?!; Tanzania bila Ukimwi inawezekana; Ukimwi uliisha lini?! Maisha bora kwa kila Mtanzania; yako wapi?! Kura ya maoni ya katiba pendekezwa ni April 2015; iko wapi?! Kura ya maoni iko pale pale; iko wapi?; tutakomesha mauaji ya watu wenye Albinism!; robo ya kwanza ya mwaka huu tumeshuhudia mauaji ya kutisha ya Albinos!

Nimetangulia kusema awali kwamba do not jump the gun! huyu EL ni wa kumsubiri kwenye campaign trail ikiwa atateuliwa kupeperusha bendera ya CCM: hapo abanwe kulia na kushoto kuhusu ufisadi na tuhuma mbali mbali za ufiadi zinazomzunguka yeye mwenyewe, wanahabari wacheze sehemu yao, wananchi kwenye mikutano ya kampeni; ndani ya midahalo na mitandao ya kijamii, atwambie kinaga ubaga agenda yake pana akiwa Rais; ufisadi included; mikakati ya utekelezaji wake na time frame.ni lazima pia atwambie mahusiano yake na watu wanaomzunguka ambao wana tuhuma lukuki za ufisadi pia na jinsi atakavyotnganisha kazi zake Ikulu na urafiki wakwe na watu hao!

tukifika mahali tukakubali as a nation mtu akatoa kauli tukashangilia tu kama mazuzu ili mradi katamka; bila kuhoji, kuuliza maswali magumu na kudai taarifa za utekelezaji na majibu husika tutakuwa tumekwisha kabisa na hilo ndilo lililotufikisha hapa tulipo!!

Elimu kwanza; yees! Elimu inajenga kujiamini kwa sababu mtu anakuwa anajua anachokisema kwa sababu amekifanyia kazi! anajua wapi kwa kupata taarifa sahihi; Elimu hiyo ndio itakayotuwezesha watu wetu kudai elimu ya uraia; kuhoji matumizi mabaya ya raslimali za umma; viongozi wetu kupenda starehe na kuishi nje ya uwezo wao (ostentation!); kudai nafasi yao sahihi katika uopngozi wa nchi yao; kukataa kufanywa watwana na viongozi wao; kusisitiza haki sawa kwa wanachi wote; kukemea usiginwaji wa haki za binadamu na demekrasia; watu wasio na elimu ya kutosha; elimu bora sio bora elimu katu hawawezi kuhoji ufisadi kwa sababu hawajiamini na hawana taarifa sahihi; kwa hiyo ni waoga ni rahisi kudanganywa na kukubali vizawadi zawadi vya kanga duni na fulani cheap na kazi yao ni kupiga makofi tuuu!

Muzee mwanakijiji; hebu vipange vipaumbele vyako vizuri zaidi, ufisadi ni mbaya ndio, EL huenda sio msafi ndio! lakini "wrong diagnosis leads to a wrong perscription"; dakitari akikosea kutambua ugonjwa lazima atatoa dawa ndivyo sivyo! mgonjwa atakufa mwana kijiji.
Mzee mwanakijiji; nina maoni mazito; (strong opinion) kwamba katika maswala nyeti ya nchi; You have your priorities TOP SIDE DOWN!!!!; hakuna kama elimu; it is second to none! Elimu hujenga kujitambua; kujiamini; kuweka vipaumbele sawasawa; kuwa na maono mapana kuhusu maisha na dunia kwa ujumla; not vice versa.

Kwa nilivyokuwa namjua/kumfahamu mwanakijiji miaka miwili iliyopita angepaswa aandike kama ulivyoandika MTK, kwa bahati mbaya vijana wengi tunaharibiwa na makundi. Siamini kama mwanakijiji hajui kuwa "education is everything and second to none"
 
ndugu yangu kila nikiendelea kusoma hoja zako juu ya hili nnaona zaidi chuki na muhemko tu ndio inayokuongoza.ufisadi ni suali mtambuka, ni jambo ambalo lipo kwa mataifa yalio na yasio na elimu. yaliotoa kipaumbele kwa ufisadi ama la. hujaja na hata nchi moja ambayo imefanikiwa moja kwa moja na hamna ufisadi.pili hujanionyesha trend za nchi nilizokutolea mfano kua zimefanikiwa kwa kutoa kipaumbele kwenye hali ya ufisadi ilikuwaje kabla kuimplement hizo policy na baadae kwa nn ?jee huwezi kusema kua kwa kua wananchi wengi wanajielewa imekua rahisi sasa kuona ufisadi kwa macho mawili na kua na ujasiri wa kuusemea na kupambana nao kwa kua wana elimu na ujuzi wa kuutambua ?mheshimiwa lowassa kwa nilivyomfahamu kipao mbele chake kikuu ni elimu na sio kua hatopambana na ufisadi au kuhakikisha afya na bara bara haziko vyema. nilivyomuelewa taifa likiwa na knowledge base ilioandaliwa vyema ni rahisi sana kutatua matatizo yakeleo kwa ukosefu wa hilo ni rahisi kina mwanakijiji na wenzake kutulisha kasumba, kutuaminisha huyu fisadi huyu hapana.wale jana walitwambia cuf ccm b leo cuf jembe. wananchi kwa ukosefu wa elimu wamekuwa muhanga wa kutumiwa na wachache.hatutaki taifa la magoi goi, kina mwanakjj na wenziwe wachache wanatulisha kasumba na kutuchanganya, tunahitaji taifa ambalo watu wake wengi wanajielewa kuanzia vijijini hadi mijini. nchi ikiwa elimu iko juu, ni rahisi kupambana na mengi ikiwemo ufisadi, rahisi kutengeneza ajira, hata kuwa na kilimo kilicho imara. huwezi kupeleka matrekta na vifaa vya kilimo kwa watu wasio na uelewa na mbinu za kisasa.kwa hili lowassa yuko sawa, elimu kwanza mengine yanafuata.na kuhusu kupambana n ufisadi nani asiejua vp ktk kipindi kifupi alichokaa aliwanyoosha watendaji na kuzuia upotevu na utafunaji wa pesa za serikali, hivi hili pia hujaliona?ukiacha kesi ya richmond lete jambo lingine ambalo unaweza kumnyooshea kidole lowassa

Kaka "Mtu wa Pwani" ni heri ukajifunze kupanga hoja kwa kufuata mtindo wa paragraph...

Hoja zako sio kama ni very weak,pia mawazo yako hayapo organized.

Mtu akisoma jibu la MM kwako na your reply to him anaona wazi kabisa tembo anapambana na sisimizi

Ningekujibu hoja zako ila nimeangalia bandiko lako nimeona moshi tu,yaani hujui ulikua unaandika nini,no one can understand your madness!
 
Kwaio wewe unataka raisi awe nani labda
Tatizo sio mtu, Rejea speech za JKN.Nyie mawazo yenu yamejengeka kwa Watu, Kiongozi anayetakiwa ni yule anayejua Mustakabili wa Tanzania na Hasa Changamoto zinazoikabili nchi kwa sasa!!
Namnukuu Mwanakijiji,
1.Ufisadi
2.Ufisadi
3.Ufisadi
Lowasa hafai kwa sababu,
1.Amezungukwa na mafisadi kama watu wanamuunga mkono
2.Anatumia fedha nyingi sana kuwanunua watu ili akubalike
3.Ana element za ufisadi, hivyo hawezi kukemea ufisadi
4.Lowasa hana mawazo mapya, kumbuka akiwa PM Badala ya kuwahimiza wananchi waache kukata miti ovyo na wapande miti kwa ajili ya ustawi wa nchi baadaye, yeye alikuja na wazo la Mvua ya kutengeneza!! Umeshawahi kuisikia hiyo!!!
5.Kwa kumuangalia usoni (REJEA PICHA YA MWANKIJIJI HAPO JUU) Afya yake inahitaji kuangaliwa, na kazi ya urais kwa mtu mwenye maono si Starehe ni kuwatumikia watu. Namkarii JKN" Kila nikipita Barabarani Nikiona watu katika hali ya masikini, nahisi kuwa mimi kama rais sikufanya vizur mahali fulani" mwisho wa kunukuu, Je EL? Kiongozi kuwa masikini si dhambi, dhambi ni kutumia nafasi yako kama kiongozi ili kujitajirisha.
6.Lowasa hafai kwa sababu yuko tayari kuwanunua wajumbe wampe kula ili awe Rais!!! Hii ni Hatari kwa nchi, kwa hii tu ni disqualification kubwa sana kwa Kiongozi.
Nawasilisha,
cc: MUSSA ALAN, Lizabon.
 
Mwanakijiji umenena vyema kwani watanzania walio wengi wamekufa ganzi, uwezo wa kutambua adui hawana, wanashindwa kubaini kuwa kwa miaka mingi EL alikuwa waziri wa ardhi, kule kuna migogoro lukuki, alikuwa waziri mkuu, huko ndo aliacha madudu ambayo mpaka leo watu badala ya kulipia huduma ya umeme wanalipa matajiri walio leta huduma ya umeme.

Hizi ni dalili mbaya nchi ilipo fikia akipewa yeye itakuwa zaidi ya Somalia au Burundi. Tusipo jitambua watanzania wengi tutakufa kabla ya muda wetu kwa kuwa Rostam Azizi, Karamagi, mafisadi wakubwa ndio wamemzunguka, hivyo kama akiwa Rais kila mtanzania achonge jeneza lake mwenyewe, make misiba itakuwa mingi
 
kwa hili lowassa yuko sawa, elimu kwanza mengine yanafuata.na kuhusu kupambana n ufisadi nani asiejua vp ktk kipindi kifupi alichokaa aliwanyoosha watendaji na kuzuia upotevu na utafunaji wa pesa za serikali, hivi hili pia hujaliona?ukiacha kesi ya richmond lete jambo lingine ambalo unaweza kumnyooshea kidole lowassa


Mwaka gani huo alifanya hili? au unasahau ufisadi uliofanyika kati ya 2006-2008? naomba mifano mitatu tu ya watendaji aliowanyoosha na kuzuia upotevu wa hela. Labda tunaweza kupata mwanga wa jinsi atakavyopambana na ufisadi endelevu.
 
Kwa nilivyokuwa namjua/kumfahamu mwanakijiji miaka miwili iliyopita angepaswa aandike kama ulivyoandika MTK, kwa bahati mbaya vijana wengi tunaharibiwa na makundi. Siamini kama mwanakijiji hajui kuwa "education is everything and second to none"

You are confusing education with knowledge. Unafikiri elimu tu inaweza kumbadilisha mtu awe asivyo? kwamba unaweza kumfundisha mtu ubaya wa wizi halafu asiibe kwa sababu ameelimika?
 
Hili li nchi lilishalaaniwa.....Vinginevyo, watu wenye mawaa wangekuwa wanajichuja wenyewe.

Ila ukiangalia timu za baadhi ya wagombea basi hutapata shida kujua watakayoyafanya wakipewa nafasi ya kuingia ikulu.
 
Nilisahau nyingine ambayo ni muhimu. Kwenye Bunge wakati nchi inazizima kuhusu ufisadi wa Escrow hakusema chochote as if wale walio piga hela aliumia kuwa kwanini nayeye hakupiga hizo hela. Mtu kama huyu mtasema kuwa kweli awe Rais? anauchungu na wale wanao lala bila kupata liziki? kweli huyu jamaa akichukua nchi pesa zote zinazo kusanywa na TRA si zitakuwa zake? Sikiliza anavyo jieleza hata kujieleza hajui inaonekana ana hasira.

WATANZANIA TUTAKUWA TUMELOGWA LOWASA AKIWA RAIS
 
Mwanakijiji umenena vyema kwani watanzania walio wengi wamekufa ganzi, uwezo wa kutambua adui hawana, wanashindwa kubaini kuwa kwa miaka mingi EL alikuwa waziri wa ardhi, kule kuna migogoro lukuki, alikuwa waziri mkuu, huko ndo aliacha madudu ambayo mpaka leo watu badala ya kulipia huduma ya umeme wanalipa matajiri walio leta huduma ya umeme.

Hizi ni dalili mbaya nchi ilipo fikia akipewa yeye itakuwa zaidi ya Somalia au Burundi. Tusipo jitambua watanzania wengi tutakufa kabla ya muda wetu kwa kuwa Rostam Azizi, Karamagi, mafisadi wakubwa ndio wamemzunguka, hivyo kama akiwa Rais kila mtanzania achonge jeneza lake mwenyewe, make misiba itakuwa mingi

Spot on......!!

Kuna mtu aliwahi kusema kuwa, "ukinionesha sura yako (wajihi wako), nitakueleza jina lako....show me you face and I will tell your real name"

Laiti kama maombi yangeweza kusaidia katika wakati tete kama huu.... Ila akina Tomaso tutaendelea kupata shida!
 
Edward 'Fisadi' Lowassa awe ràis wetu?akili inagoma kabisa kukubali,na hasa nikiwafikiria akina Andrew 'kashfa ya radar' Chenge kwamba watakuwa washauri wake wakuu najisikia kutetemeka kwakweli.To hell with Mafisadi!
 
Tujifunze Nigeria,adui wao alikuwa Bokoharamu,walifanya mini?walimtoa rais. Watanzania adui mkubwa ni ufisadi,CCM wakifanya kosa wataisoma plate number Tz
 
huwezi kupeleka matrekta na vifaa vya kilimo kwa watu wasio na uelewa na mbinu za kisasa.kwa hili lowassa yuko sawa, elimu kwanza mengine yanafuata.na kuhusu kupambana n ufisadi nani asiejua vp ktk kipindi kifupi alichokaa aliwanyoosha watendaji na kuzuia upotevu na utafunaji wa pesa za serikali, hivi hili pia hujaliona?ukiacha kesi ya richmond lete jambo lingine ambalo unaweza kumnyooshea kidole lowassa

Unaijua story ay VodaCom na wadau wake? Unajua mambo ya ununuzi wa nyumba London?

Hebu jitahidi kutafuta maarifa kabla ya kuandika!
 
Back
Top Bottom