Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Kwanini unalenga mpaka Lowasa akatwe jina sio CCM itoweke kwenye ramani za siasa za Nchi yetu.

Mtiririko wenye mfuatano wa thread zako lengo kuu ni lowassa atupwe kwenye kinyang'anyiro.
Nini kimefochika nyuma ya pazia???

hujanunuliwa kweli wewe na Rz1!
Ninamashaka na wewe zaidi ya hapo una chuki tu na Eddo.

ulimwuuliza swali akakataa hatoshughulikia Ufisadi?
kama uko kwenye Propaganda za kuhakiki yule mwenye nguvu aliyetishia ndani na nje ya CCM amalizwe kabla ya kuvumika mipaka,basi,huenda ukaeleweka.
Ila kwa mtindo huu wewe naye ni FISADI ALIYEKUBUHU.

Hivi hujui kuwa ukishamuondoa Lowassa wengine hawa rahisi; wengine hawajaanza kujitetea na kutumia nguvu kubwa kuingia Ikulu.
 
Ni kweli EL anajaribu kujiosha.ni mwana CCM amefaidi CCM lakini hajawahi kusema juu ya Kilimo Kwanza anaona aliyemrithi kafanikiwa kulisha taifa na ziada tunasaidia wengine.Kama kweli EL ataleta ajira atwambie katika rasilimali zilizopo hatuonyeshe mifugo yake sijawahi kuona hilo mtoto wa mkulima afadhali kila kukicha anafundisha watu juu ya kilimo na ufugaji nyuki na shamba lake ni darasa kila mtu anakwenda kujifunza amweka asali ya Tanzania katika ramani niambie EL mifugo umefundisha nani kama si usanii. Sema ubunifu siyo nitafanya mambo haya mkinichagua usipofanya? Usidanganye watu huna jipya
 
Yanaendelea sirini kwa wataka urais walioko CCM ni magumu na mazito kuliko haya anayofanya Lowassa hadharani,ni bora huyu hajifichi sio mnafiki.
 
Watu wa Ukawa mbona mnapanic hvo na Lowassa ?? Nafikiri mngekaa mje na mgombea wenu tukutane uwanjani .... kwani nini kinawaogopesha kiasi hicho hadi mnakuja kuingiliz mambo ya CCM ? Nafikiri mnajidhalilisha hapa. Kama lowassa ni mchafu na fisadi si ndio faida kwenu october ...sasa ni nini kinawawasha sasa hvi...???
kwetu UKAWA mtu akishakuwa mwizi na fisadi, hata ile kuwazia tu kuikalia ikulu ya Tanzania, ambapo ni mahali patakatifu, ni kufuru kubwa sana. Tunawafundisha nini wanetu na wajukuu zetu? kwamba wizi na ufisadi wa mali za umma ni sawa?!! Kwamba mtu unaweza kuiba mali za umma na baadaye kutumia mali hizo hizo kununua uongozi wa juu kabisa wa umma kutoka kwa umma wale wale ulowaibia?!!

ccm ni chama la kifisadi ndo maana linaruhusu fisadi kujinafasi. hili likikundi la ccm lazima vijana tuling'oe sasa. limeoza kutoka juu hadi chini kiasi kwamba hakuna mwema yeyote atakayetoka mumo. wema hawapewi nafas ccm ndo maana hata mara moja hutawasikia watu wa kaliba ya warioba, nyerere, salim, butiku wakifikiriwa kuwa viongozi katika ccm. watu wa kaliba hiyo ni maadui wa ccm. akina rostam ndo marafiki wa ccm
 
edward-lowassa.jpg


Watanzania wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanaaminishwa kuwa ana maono ya kiuongozi ambayo yakitumika yanaweza kulinasua taifa letu toka hapa lilipo. Wanajaribu kuaminishwa kuwa Lowassa ni kiongozi bora ambaye Watanzania wanapaswa kumwangalia kwa matumaini - ndio maana ya "Safari ya Matumaini".

Wapo kati yetu ambao wameshazugika na pendekezo hilo na wamekuwa kama waliorogwa hivi. Wapo baadhi yetu kwa muda wote wa uongozi wa Lowassa (hasa baada ya kuwa Waziri Mkuu na baadaye) tuliona kile ambacho labda kimefichika kwa wengi - Lowassa hafai.

Hii si hukumu juu ya utu wake, heshima au ubinadamu wake; ni hukumu juu ya uongozi wake na maono yake kama kiongozi. Kumkataa Lowassa, maono yake, uongozi wake na fikra zake siyo kumchukia yeye kama Mtanzania mwenzetu au kama binadamu. Ni kuwa na tofauti naye na vile anavyowakilisha kiasi kwamba tofauti hizo hazijawezi kupatana (irreconcilable differences).

Katika siasa ni lazima tuheshimu uwepo wa tofauti hizi na tuelewe ndio msingi wa kutafuta viongozi bora zaidi au chama bora. Kwa kadiri yeye atakavyojaribu kujiuza ndivyo na sisi wengine tutazidi kuonesha kuwa hauziki au zaidi hanunuliki. Hii si chuki ni tofauti tu ya msingi (fundamental difference).

Pendekezo langu linatokana na hili; kwamba zipo na zimedumu tofauti za msingi kati ya maono ya baadhi yetu na maono ya mgombea huyu mtarajiwa kutoka CCM. Tanzania haihitaji maono na uongozi wa Lowassa kwa sababu nyingi tu; nitaanza na moja ya leo na nitaendelea kwenye mada hii hii kila ninapopata nafasi hadi jina lake litakapotupwa na NEC na yeye akaendelea kuwa Waziri Mkuu wa zamani.

Mara kwa mara baada ya sakata lake na katika jitihada za kujirudisha katika umuhimu (relevance) Lowassa amekuwa akizungumzia mwelekeo wa sera zake na kitu kitakachomuongoza. Aliamua kwenda kinyume na mwelekeo wa serikali ya chama chake ambayo iliweka mkazo kwenye "Kilimo Kwanza"; yeye ameamua kuja na hoja ya "Elimu Kwanza".

Alielezea kupinga kwake hoja ya Kilimo Kwanza miaka michache nyuma alipohojiwa katika kipindi cha Dakika45 (kinachorushwa na ITV). Alinukuliwa kusema "Mpango huu wa Kilimo Kwanza umekosa nguvu kwa sababu kuanzishwa kwake hakukuzingatia dhana ya ukombozi wa mwananchi wa kawaida. Tangu awali ndani ya chama (CCM) nilieleza kuwa sitaunga mkono hoja hiyo mpaka kuongezwe mashiko na kuwa Elimu Kabla ya Kilimo Kwanza"

Hoja hii ameirudia tena juzi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ambao bila ya shaka wengi wamekuwa 'charmed' na wingu la umaarufu wa Lowassa kiasi kwamba hakuna ambaye ameweza kumbana vizuri kwenye maswali. Anasema endapo atachaguliwa basi ataelekeza nchi kwenye "elimu kwanza"; kwamba hiki ndicho kipaumbele chake.

Ndio maana sisi wengine tunasema hafai; kwa sababu inaonekana siyo yeye wala chama chake ambao wamelielewa vizuri tatizo linaloikabili Tanzania; tatizo ambalo limeielekeza (orient) Tanzania kufuata njia ya Nigeria. Kwamba tunaweza kabisa kutengeneza uchumi wenye nguvu lakini wa taifa lenye umaskini uliokithiri, lisilo na usawa na la wasomi wasioweza kulipeleka taifa mbele. Tutakishia kujisifia wingi wa wasomi ambao wengi wataishia kwenda nje ya nchi kutafuta maisha. Taifa ambalo litakuwa limegawanyika sana kama Nigeria - licha ya kuwa na wasomi wengi.

Lowassa inaonekana ameshindwa kuelewa au hataki kukubali kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni la aina tatu:
1. Ufisadi
2. Ufisadi
3. Ufisadi

Lowassa hatopambana na ufisadi kwa uzito unaostahili kwani haoni kuelewa kuwa ni tatizo la hatari zaidi kwa taifa "kuliko vita wakati wa amani" kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Kutokuelewa kuwa Ufisadi ndiyo sekta haramu yenye nguvu zaidi katika nchi yetu ni kushindwa kuelewa tatizo letu hasa ni nini. Ufisadi umepenya (permeate) kwenye kila sekta nyingine zote (rasmi na zisizo rasmi). Umeathiri elimu, afya, usalama, na hata umoja wa taifa. Kutokulielewa tatizo hili kwa mtu anayetaka kugombea nafasi ya Urais (haijalishi anatokea chama gani) ni kutokuelewa namna ya kukabiliana na changamoto nyingine zote.

Kwa sababu hii peke yake Lowassa na mgombea mwingine yeyote ambaye haweki "ufisadi" kama ajenda yake ya kwanza na kubwa zaidi basi hafai. Kwa sababu atatuzungusha kwenye madudu mengine yote isipokuwa kwenye kumkoma nyani giledi.

Kikwete - kwa wanaokumbuka - alishabikiwa na wengi si kwa sababu ya "Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya" bali zaidi kwa kuwapa Watanzania matumaini kuwa atashughulikia ufisadi vikali. Hotuba yake ya kulifungua Bunge na ile ya Ngurdoto na zile ziara zake za kutembelea Wizara ziliwafanya watu waamini kidogo kuwa hatimaye "kipele kimepata mkunaji". Leo hii miaka tisa baadaye ripoti ya CAG imeonesha kidogo tu kuwa tatizo hili la ufisadi halijapata mtatuzi ndani ya CCM na hata mtu anayeshabikiwa sana kuwa ati anaweza kuwa Rais inaonekana tatizo hili limempita kabisa.

Nikisema "hafai" simsingizii; nasema kilicho dhahiri; I'm just stating the obvious.

Wanaomtaka Lowassa - wapenzi, mashabiki na waumini wake - watuambie vita dhidi ya ufisadi ina umuhimu na uzito gani katika agenda za Lowassa. Wakituambia kuwa "ni mojawapo" ya mambo atakayoyashughulikia tuendelee kumkataa kwa sababu bado atakuwa hajaelewa tatizo letu hasa ni nini kama taifa.

Nitandelea...

NB: Kwa wageni wa hoja hizi warejee mada yangu ya 2007: Kikwete Siyo Safi, Yes I said it


Wewe ufe na uzikwe hukohuko Ulaya - ufisadi ni hoja yako huwezi kumlazimisha Lowassa abebe tatizo lako;pia ikiwa unadai kuwa Kikwete alipendwa kwa sababu ya ahadi ya kupambana na rushwa aliyoitoa wakati akihutubia bunge,kwanini usisubiri Lowassa naye atoe ahadi hiyohiyo wakati atakapokuwa anahutubia bunge?Natamani nikutukane kabisa
 
Naam Mzee Mwanakijiji niliwahi kusema huko nyuma kuwa katika taifa hili si rahisi kuitoa CCM madarakani kupitia sanduku la kura na sababu kuu ni UFISADI. Ni Tanzania tu mafisadi wanalaani ufisadi, wala rushwa wanapiga vita rushwa, wauaji wanalinda amani, wapokea rushwa ndio wanatoa haki na wachezaji ndio waamuzi.

Katika hali kama hii haki hiyo itapatikana wapi? Utawala wa sheria utawezekana vipi? Imefikia wakati ufisadi ni sifa mojawapo wa kuupata uongozi ndani ya CCM. Ndani ya CCM kiwango cha ufisadi ndicho huamua nani ateuliwe na nani aachwe na sidhani kama kuna mtu msafi huko na, kama yupo anayedai hivyo, anafanya nini huko?
 
Wewe ufe na uzikwe hukohuko Ulaya - ufisadi ni hoja yako huwezi kumlazimisha Lowassa abebe tatizo lako;pia ikiwa unadai kuwa Kikwete alipendwa kwa sababu ya ahadi ya kupambana na rushwa aliyoitoa wakati akihutubia bunge,kwanini usisubiri Lowassa naye atoe ahadi hiyohiyo wakati atakapokuwa anahutubia bunge?Natamani nikutukane kabisa

lowasa nimwizi wa mali za umma, hatuwezi kumkabidhi ofisi kuu ya umma mtu fisadi. marafiki zake ni kina karamagi rostam bashe...hii haikubaliki kundi la wapiga dili lipewe ikulu ya nchi. ni kazi ya ukawa kuwafundisha ccm, kama ambavyo imekuwa ikiwafundisha siku zote, kuwa ufisadi wa mali za umma haukubaliki.
 
Ukimuona mtu mchafu ukasema ni mchafu utakuwa umemchafua au umeeleza kilicho dhahiri. Kumchafua mtu kuna presume kuwa mtu huyo alikuwa msafi kwanza. Vinginevyo, asingejitahidi sana kujaribu "kujisafisha". Ukiona mtu anaenda mtoni kuoga mara kwa mara ujue...
Ukiona unahangaika na kulazimisha fulani mchafu ujue Kuna tatizo... Kama ni mchafu basi kauli moja tu yatosha

Why so much efforts kumsiriba mmoja wakati kapu LA ccm halina msafi?
 
Ukiona unahangaika na kulazimisha fulani mchafu ujue Kuna tatizo... Kama ni mchafu basi kauli moja tu yatosha

Why so much efforts kumsiriba mmoja wakati kapu LA ccm halina msafi?
ndo anayejitia kimbelembele zaidi. isitoshe shetani hatumkemei mara moja tu bali kila tukisali tunakemea pepo.
 
Eddo hawezi kukwepa lawama na wala mukuu wake aliyemtelekeza kwenye kadhia ile ya Richmond. Lakini kutelekezwa kwake hakumfanyi yeye msafi.
Pili, nakubaliana kabisa na mwanzilishi wa uzi huu. Mapapa yote ya juu hayaachi mirija yao ikaonekana moja kwa moja kwamba wanachota mali yetu. Tunakumbuka tu wakt mmoja, kwa mfano, mwakilishi wa Dowans alikuwa mtu mkubwa serikalini. Na ni mtu ambaye ana connections zote na Eddo na JK. Sasa wanatuambia nini kwamba hawahusiki.
Watanzania tusiwe watu wa kuburuzwa na wajanja wajanja kama hawa. Ni bora tuanze upya.
 
Dawa ya ufisadi ni elimu... Tukielimika hakuna wa kutuibia
 
Kama siyo mchafu, kwa nini anatumia mabilioni ya pesa ili kudai kuwa ni msafi. Je, huoni kwamba wewe ndiyo huna mantiki katika hilo?
Hatujaona msafi bado katika hao wote. Yeye na mkulu wake aliyemtoa yeye kafara walikuwa kwenye dili pamoja. Lazima Watanzania tuamke sasa. Watu hawa hawafai. Wewe unayefaidika kivyako ukatiwa upofu usione jinsi ambavyo nchi inakwenda kombo na watu hao, huwajui wananchi na taabu zao, taabu ambazo zingeweza kupunguzwa na viongozi wenye nia ya kuliendeleza taifa.
Tatizo kubwa ni ufisadi, ufisadi, ufisadi.

Ukiona unahangaika na kulazimisha fulani mchafu ujue Kuna tatizo... Kama ni mchafu basi kauli moja tu yatosha

Why so much efforts kumsiriba mmoja wakati kapu LA ccm halina msafi?
 
ndo anayejitia kimbelembele zaidi. isitoshe shetani hatumkemei mara moja tu bali kila tukisali tunakemea pepo.

Amewapreempty... I kifala July hii single inaexpaya.. Ufisadi wa wengine utaibuka
 
Wewe ufe na uzikwe hukohuko Ulaya - ufisadi ni hoja yako huwezi kumlazimisha Lowassa abebe tatizo lako;pia ikiwa unadai kuwa Kikwete alipendwa kwa sababu ya ahadi ya kupambana na rushwa aliyoitoa wakati akihutubia bunge,kwanini usisubiri Lowassa naye atoe ahadi hiyohiyo wakati atakapokuwa anahutubia bunge?Natamani nikutukane kabisa


sasa kinachokuzuia kutukana nini; kichwa kama sahani ya pilau! Na wewe usife kabisa.
 
sikiliza clip hiyo hapo chini na kwa umakini zaidi hasa kuanzia 9:20 - 9:38
"What we do is, when we are called, having being so empowered, we buy what one call the tuk tuk from India and expect it to behave like a mercedence benz. How does that happen because what we do is to elect thieves, we elect hyenas to take care of goats and when the goats are consumed we wonder why???!!!" By Prof PLO Lumumba.
clip hii hapa chini
https://www.youtube.com/watch?v=JiItrWwBbiM
 
Ukimuona mtu mchafu ukasema ni mchafu utakuwa umemchafua au umeeleza kilicho dhahiri. Kumchafua mtu kuna presume kuwa mtu huyo alikuwa msafi kwanza. Vinginevyo, asingejitahidi sana kujaribu "kujisafisha". Ukiona mtu anaenda mtoni kuoga mara kwa mara ujue...
...........kinachotia shaka baadhi yenu (..kama wewe) katika hoja zenu ni pale mnapoona wasiofaa tu, hamthubutu kuonesha nani anafaa, ndo maana hoja kama hii zinatiliwa mashaka, shida yetu ni moja, kwa mtu kama wewe mwenye hoja zenye mantiki (...lakini siyo hii), watu ni rahisi sana kuwaaminini, pia ni rahisi sana kutumika kwa upande moja kupotosha watu walio wengi kulingana na uwezo wao mdogo wa kuchanganua mambo.......
 
...........kinachotia shaka baadhi yenu (..kama wewe) katika hoja zenu ni pale mnapoona wasiofaa tu, hamthubutu kuonesha nani anafaa, ndo maana hoja kama hii zinatiliwa mashaka, shida yetu ni moja, kwa mtu kama wewe mwenye hoja zenye mantiki (...lakini siyo hii), watu ni rahisi sana kuwaaminini, pia ni rahisi sana kutumika kwa upande moja kupotosha watu walio wengi kulingana na uwezo wao mdogo wa kuchanganua mambo.......

Siyo lazima wote tuseme; tuwaache wengine waseme anayeona anafaa. Wewe unaona nani anafaa na nani hafai? ndio maana ya kutoa maoni na kubadilishana mawazo.
 
nimesoma hoja yako kaka yangu mkjj nikagundua kaka kumbe ww ndio unaehemkwa na.kujikokoteza hoja zisizo na mashiko ili uaminishe watu kua mtu unaemchukia bila sababu hafai


umeeleza kua kilichomfanya JK kukubaliwa na watanzania wengi ni hotuba yake inayozungumzia ufisadi. na mwisho serikali kushindwa kupambana na ufisadi. suali kwa nn walishindwa? kama hutokua mbabaifu utagundua ukosefu wa elimu umechangia sehemu kubwa.

umetoa mfano wa nigeria na kutaka kuaminisha watu.kua ati elimu haitoweza.kuinua hali za watu bali itazalisha zaidi wasomi ambao mwisho watamalizia jela au kuikimbia nchi. mbona hutoi mifano ya nchi nyingi.ambazo zimefanikiwa kama uk malaysia singapore south korea na nyingi kwa kuweka mbele elimu kwanza.


naamini unajua elimu ndio msingi wa kupambana na kila kitu. bila elimu bora wananchi hawatakua na nyenzo sahihi za kuelewa ufisadi unaofanyika na kuuzuia. bila elimu sahihi utendaji wa kubabaisha utaendelea lkn ili utendaji ulio imara lazima elimu kwanza itangulie.

lowassa yupo sahihi katika kupambana na ufisadi alikuwa waziri mkuu wetu kwa mda mfupi tuliona alivyoisimamia.serikali iwajibike. hakuridhika na ripoti anazoletewa tu ofisini kwake. alikua akifatilia na kuchukua hatua.

mm sioni dosari ya lowassa ila kwenye sakata la richmond na hili linasemwa kua ilikua ni njama ya kumvunja kasi ukweli utajulikana.

ww kumkataa una sababu zako naamini ulikuq ukimuona lowassa kama.arrogant person na alikua akiwadhalilisha watendaji kwa maamuzi kitu ambacho mm nilikikubali mwanzo baadae nikaona alikuwa sahihi. ili awajenge hofu wengine kula mali ya umma. na jengine nnarejea kutaka kufanya naae mahojiano akakataaa hilo.limekuganda na inaonekana umeapa kummaliza.kwa.kalamu.yako.

ila jua watanzania wa leo.sio jana
 
Back
Top Bottom