Mzee Mwanakijiji ametimiza wajibu wake... kilichopo ni kwamba, endapo mathalani MM angepewa uwezo wa kupiga kura 25 million peke yake na kura hizo pekee kuamua mustakabali wa rais wetu, basi kwa mujibu wa MM ni kheri kura hizo zote aziharibu kuliko kumpa Lowasa! Kinyume chake, kuna wengine endapo wangepewa uwezo huo wa kuhodhi kura 25 million peke yao, basi haijalishi Lowassa anasimama na nani... zote hizo wangempa Lowassa! Haidhuru, kura hizo 25 million tunaweza kuziita a powerful veto vote yenye uwezo wa kuamua nani awe rais bila kuhitaji kura ya yeyote ya ziada... ni tofauti na ile ya UN yenye uwezo wa kukataa peke yake! Hapa ndipo unaposimama umuhimu wa hoja ya MM, haidhuru hata kama Lowassa, hatimae atashinda kwa kishindo hata kama ni kwa 95% na zaidi... bado haitaondoa ukweli wa Lowassa kwamba hafai; si tu kwa mujibu wa
Mzee Mwanakijiji bali kwa mwingine yeyote yule ambae hana amtakae kwenye kinyang'anyiro hiki; iwe kutoka chama tawala au upinzani!
I hate to say this lakini ukweli ni kwamba, hata kama JK nae alikuwa fisadi kabla ya hata kuingia magogoni but JK was smart enough as compared to EL! He's smart enough coz' huku mtaani haikufahamika hivyo kwa wengi... Kama alikuwa na tuhuma zozote za ufisadi basi tuhuma hizo ziliweza ku-circulate only among few people... sina shaka hata chembe kwamba hili lilichangiwa sana na zama zenyewe... hazikuwa zama za free flow of information kama ilivyo sasa! Katika hali ya ajabu kabisa, Lowassa anaonekana kuwa the most stupid accused corrupt leader seeking the highest position in the country... YES, I repeat,
the most stupid accused corrupt leader seeking the highest position in the country!!! He's top of the stupid accused as a corrupt leader because, pamoja na kwamba kila mtu anafahamu tuhuma za ufisadi dhidi ya Lowassa lakini bado ame-opt ku-side or team up with ALL other accused corrupt leaders! Sitamtaja Serukamba kwa maana yeye ni mganga njaa anayeweza kutumiwa na yeyote yule lakini hakuna nchi hii asiyefahamu tuhuma chafu za ufisadi dhidi ya Rostam Aziz lakini pamoja na yote hayo huyo ni one of the insiders or probably Master-minder wa Lowassa katika kuingia Ikulu! Hakuna hata mmoja Tanzania hii anayefuatilia siasa za Tanzania asiyefahamu tuhuma za ufisadi wa Andrew Chenge... lakini huyu nae ni insider au bila shaka ni Senior Tactic Team Member wa EL katika mbio zake za urais! Hakuna anayefuatilia siasa za nchi hii asiyefahamu tuhuma za ufisadi dhidi ya Nazir Karamagi! Huyu nae ni insider au bila shaka nae ni one of the Senior Tactic Team Member wa EL katika mbio zake za Ikulu! JK hata kama alikuwa na tuhuma za ufisadi, hakuwa mpumbavu kiasi cha upumbavu unaoneshwa na Lowassa na ndio maana wala hakuona taabu wala aibu kumkwepa EL na kumwacha afe peke yake kwenye tuhuma dhidi ya Richmond!
Swali ambalo sijapata ni jibu ni message anayokusudia Lowassa kui-deliver kwa Watanzania hususani wale wanaofuatilia siasa za nchi hii! Kwamba, yeye binafsi, Rostam Aziz, Andrew Chenge, Naziri Karamagi wote hawa kwa umoja wao wanasingiziwa na hivyo wameamua kusimama pamoja ili , pamoja na mambo mengine they mean to reveal their innocence to the public? Au labda anataka kutuma ujumbe kwa wafuatiliaji wa siasa za nchi hii kwamba, fuc'k ya'll (fuc'k ya Tanzanians) we don't care what you think or know about us na kwamba kwa umoja wetu we'll stand firm and fight for this post?! Ni ujumbe gani hasa EL anaokusudia kuuwasilisha kwa Watanzania?!
Akili, busara ukichanganya na uungwana wa kawaida hautamfanya mtu kuhoji kwamba, let's say huyu Mheshimiwa EL anasingiziwa... ni mazingira gani yanayosababisha awe ni yeye tu wa kusingiziwa tena wakati mwingine kwenye official platforms kama vile bunge!