Lowassa anasafishwa!

Lowassa anasafishwa!

sIKU AKIREJEA SERIKALINI ETI KAMA RAI MJUE KABISA HAKUNA TZ YENYE AMANI TENA KUTAKUWA KAMA ELDORET KULE KENYA.hAO WAANDISHI WALOHONGWA NDIO TUMEANZA KUWAONA NA SIE HATUWEZI KUKUBALI KUWA RAIS YEYE LOWASA NI MPAKA WATZ TUAMUE WENYEWE.Jamanieee ccm si wamnyang'anye uanachama aache kukisumbua chama na hao akina RA PIA.Ataishia kusema kaonewa kwann hakwenda kuwaeleza kamati ukweli alioujua yeye kama waziri mkuu?Sitaki kusikia kabisa etii kamati haikunihoji.

CCM yenyewe wamekaa kimya na wala sitashangaa kuona wakimpitisha kama mgombea mmojawapo wa kiti cha urais,si umeanza kusikia minong'ono ndani ya chama kuwa utamaduni wa kumwachia kiongozi aliye madarakani vipindi viwili umepitwa na wakati.Swali langu ni kuwa CCM wakimpitisha wananchi mnacho cha kufanya si atapita tuu kwa wingi wa kura kama sio asilimia 65 na zaidi katika uchaguzi mkuu ujao.

Mimi yangu macho na ikumbukwe pia kuwa huyu EL ni mtu wa visasi,akipata nafasi hii atafanya mambo ya ajabu kwani ameshasema kuwa wabaya wake watamtambua na kama hivyo ndivyo ilivyo basi tujue kuwa watu wengi sana wataumia.
 
hii kaaaazi kweli kweli jamani, hivi pale ikulu kuna nini kitamu kila mtu apatolea macho?
 
Uvccm (Bukoba) tayari wamenchangia JK kiasi cha 1 milioni kwa ajili ya kampeni mwakani
 
HAKUNA wakumzuia EL ,hatokubali kufanya kosa alilofanya February 2007.

Nguvu ya "EL na kamati yake" ya 2005 anaifahamu BWM au SAS waulize watakwambia.

Advantage ya EL ni kwamba tayari anaUZOEFU wa 2005 kutokana na kazi yao waliyofanya kama "kamati" na yeye akiwa Mwenyekiti,lakini this time ni yeye ndiye MWALI.

Nikifikia hilo napata PICHA MOJA YA KUTISHA.

Busara ni KUMSIHI tu achane na hiyo biashara,LAKINI SIYO SAHIHI KUSEMA HAWEZI.

WATANZANIA KESHENI........
 
Bhagosha,

Ivi kweli kama huyo mkuu anawazia urais kweli ndipo ntakapojua kweli sote watanzania hatuko kwa maslahi ya nchi yetu na kamwe mapinduzi ya ki democrasia hayatokuja mapema kama nilivyo kuwa nategemea kutoka kwenu vijana,

kwani nilijua fika kuwa 2010 vijana wengi mtajitokeza kugombea nafasi nyingi tu huko ndani ya CCM ila kama mambo ndio hayo msemayo ni tetesi angalieni msije mkawa mwaumba maneno hapo na likaja tokea na EL akachukuwa form.

maana tanzania yetu hii ni shida na njaaaa kwa wapiga kura ndio zaturudisha nyuma na kuja kujikwamua sijui ni mpaka watu washikiane mtutu na si kitu chema ingawa maendeleo ya nchi zingine ni mpaka mtutu upite hapa kwetu ni kuona kwa macho na kuamua huyu hafai na huyu anatufaaa period, ila utakuta mijitu kwa ajili ya njaaa inakubali kuuza kura jamani wapi twaenda bhandugu.

Huyu EL profile lake liko nje hatakama kuna jambo amepakaziwa ni kiungwana basi yeye mwenyewe aka kaaa kando kuonyesha uungwana kuwa hagombei chochote na asitake kuta ku prove kwetu ati anaweza wapi hukooo tena.

Waziri gana anakubari pitisha mikataba mibovu ilihali anakubli kabisa kuwa watu wake walio mpigia kura wata pata mateso huko mbeleni kwa tatizo lakutojari mkataba na maslahi ya nchi kweli huyo ndie anataka kuchukua fomu leo.

Me nampa big nooooooo na hasijaribu pia kutumia njia za panya kwni huko tuendako watakuja mweka madhabahuni kwa makosa alio yatenda miaka iliopita ngojeni mtakuja ona siku tuko hapa,

Na huuu ushabiki wa kupatia huyo EL kichwa ili akachukuwe fomu ni Makanisa kadhaaa kwani wao wananguvu sana huko kwa washirika wao na hapo ndipo watakapo roba step.

EL dont even think of Run for the Presidency, u'l be a biger time looser
 
Gustanza_The: naomba unitumie hata kwenye PM, ile link ya Kasori, maana nina hamu ya kusoma makala zake. Asante sana kwa kutuhabarisha kuhusu this piece of history. Huyu jamaa hatafika mbali!
Waberoya: what you said is true, tusimlaumu individual, it is the collective guilt because we feed and keep a corrupt system alive. lakini hata kama hatujampigia kura Kikwete, mimi na wewe bado tuko guilty kwa sababu tunaangalia tu wakati nchi inazidi kuangamia.

Samwel. H. Kasori Katibu mstaafu wa J.K.Nyerere 0754 372141
 
Mkuu DUA naomba unijuze wana JF wapi waliofungwa hao?tafadhali wantia mashaka mie
 
Ni vizuri iwapo atagombea urais kwani anayo haki kama mtanzania, mi naamini kugombea sio dhambi au jinai kwake lakini iwapo atapata nafikiri itakuwa laana yetu siye wananchi
 
Maneno yenu ni very hurt feeling kwa mzee sumaye, kila akiskia mtu anasogelea ile nyumba yetu magogoni anaona da sio kabisa kule. Yaani kajinyima raha zoteee harafu asiwe rais , punguzeni jamani
 
Nchi inahitaji RAIS ambaye ni semi dikteta.

EL ni semi Dicteta. EL ameshakusanya mali. Inachobakia ni kuongoza nchi. Mimi nitampigia kampeni za nguvu 2015
 
Mungu apishe mbali! Utabiri wangu ni kwamba huyo mtu na mwenzie RA watakuwa jela kwa makosa makubwa ya ufisadi. Nchi hii haiwezi kuongozwa na Lowassa wala mtu yeyote atakayemuandaa-
 
Nchi inahitaji RAIS ambaye ni semi dikteta.

EL ni semi Dicteta. EL ameshakusanya mali. Inachobakia ni kuongoza nchi. Mimi nitampigia kampeni za nguvu 2015

Ume sikia wapi mtu aka tosheka na hela alizo nazo? Kuna asiye taka zaidi? Kama kasha tajirika una juaje hataki kuongeza zaidi? Mki chagua watu kwenye uongozi kisa tu wana pesa mka tegemea ndiyo kuzuia rushwa basi tuta chemsha.
 
Achukue tu... he is the only one available who will make TAnzanians (wazee wa amani) kuingia msituni in 6 months za utawala, labda baada ya hapo tutaheshimu haki na usawa
MMMM msituni yale mabomu mawili ya mbagala yalipolipuka ulizimia jee kasheshe kama ya iraq,gaza au lebanon utaiweza?
 
Nani anamdanganya huyo Mamvi kuwa anaweza kuwa Rais wa nchi hii? Kwa sifa gani hasa? Huyu jamaa kwanza kichwani hakuna kitu, halafu ni mwizi mkubwa. Angetafuta shughuli nyingine ya kufanya badala ya kuendelea kuota ndoto za urais. Watanzania sio wajinga hivyo kama anavyodhani. Wameamka na tayari wanajua kutofautisha pumba na mchele. Tunafahamu jinsi yeye na swahiba wake RA walivyokusanya fedha kwa ajili hiyo. Lakini nafasi ya kunua tena urais haitakuwepo tena asilani!
 
Nani anamdanganya huyo Mamvi kuwa anaweza kuwa Rais wa nchi hii? Kwa sifa gani hasa? Huyu jamaa kwanza kichwani hakuna kitu, halafu ni mwizi mkubwa. Angetafuta shughuli nyingine ya kufanya badala ya kuendelea kuota ndoto za urais. Watanzania sio wajinga hivyo kama anavyodhani. Wameamka na tayari wanajua kutofautisha pumba na mchele. Tunafahamu jinsi yeye na swahiba wake RA walivyokusanya fedha kwa ajili hiyo. Lakini nafasi ya kunua tena urais haitakuwepo tena asilani!

MIMI nasema anaweza kuwa RAIS, tena mzuri tu!
 
Duh! Mkuu Jmushi1 una macho aisee!

Haha! Mkuu statement kama hiyo hapo chini haita raise you eyebrow? Sasa kama kuna mwana JF asiyejua tofauti kati ya fisadi na asiye fisadi,duh! Once again...Kaazi,na wewe hukuwa na macho hapo aisee!


Hata mimi namuunga mkono agombee, tofauti ya fisadi na asiyekuwa fisadi mimi siioni.
 
Back
Top Bottom