Kwa ufupi sana naomba kukubali kutokubaliana na baadhi ya watu katika hoja hii.
Kwanza kabisa hoja hii imechanganywa changanywa hasa kwa kuingia kwa suala la Sakina, ambalo naona kama halihusiani kabisa na hoja ya Richmond. Kama kuna hoja ingeweza kuletwa jamvini kwa mahali mwafaka ikajadiliwa kwa kuungwa mkono ama kukosolewa kwa hoja. Hii imeonyesha wazi kwani hata baadhi ya wachangiaji wameiona kama vile Sakina yumo katika operesheni safisha Lowassa. Pamoja na kuwa naweza kutofautiana na Sakina kwa mambo fulani fulani (si ya msingi), hoja ya Richmond isichanganywe naye.
Kuhusu hoja ya msingi ya Majaji na kusafisha ama kutomsafisha Lowassa, nadhani mtoa hoja ana haki kutoa maoni yake japo alipaswa kuepuka kuchanganya mada na kuegemea kwenye hisia zaidi na alipaswa kutoa mifano kama hana ushahidi wa wazi wazi. Lakini pia ameonekana kuwa mwoga maana kama si ujasiri wa Zitto kujitokeza, wengi humu JF wasingejua hadi siku ya siku kwani baadhi humu huwa hawafuatilii mambo mengi kwa wakati.
Lakini pia, sidhani kwamba Zitto anaweza kukubali kubeba gunia la misumari katika upara wake, maana Lowassa ni mzigo mzito sana kwa sasa, japo wako wanaoubeba kwa gharama kubwa, gharama ambazo zitakuwa kubwa zaidi 2010-2015, kwani wapo wanaoweza kupoteza nafasi zao kwa kupokea kazi hiyo.
Kuhusu suala la majaji, nakubaliana na wengi humu JF kwamba inawezekana kuna taratibu nzuri tu kuundwa kwa jopo hilo, lakini hoja hapa si kusafishwa ama kutosafishwa kwa Lowassa. Naamini suaa la kusafishwa kwa Lowassa, Mkapa na wengineo ni gumu sana kwa sababu nyingi sana, moja ikiwa ni "ALAMA ZA NYAKATI" kwamba. Lowassa ama Mkapa wangekuwa na umri wa Zitto, Ngeleja ama Nyalandu wangeweza kujipanga na kufanya maajabu, lakini kwa sasa Wananchi watajiuliza, kama yalipita (ya Richmond) si apumzike? Kwani hakuna Watanzania kama yeye ili na "wao wale"? maana "kila zama na walaji wake", baada ya Mkapa, akaja Lowassa, sasa ni zamu ya mwingine "kula".
Tunao utamaduni wa ajabu wa kifikra, fikra za kihalifu fikra ambazo mhalifu akiwa maendeleo "hata ya kuwanunulia bia wenzake" anasifiwa kwa kuitwa "mjanja", "ana akili sana ya kutafuta".
Nitaendelea baadaye, lakini tujadili hoja bila kutanguliza kwanza matokeo ya HOJA yenyewe kabla haijaanza kuwasilishwa ama kujadiliwa. Kwa yaliyotokea nyuma hakuna anayeweza kubeba tenga la samaki waliochina na kutembea nalo kichwani akijua majimaji yanukayo yatamvujia. Wao wenyewe (Lowassa na wenzake) hawawezi kusimama mahali kama "Tarime", "Busanda" ama "Biharamulo" na kuhutubia jukwaani ama hata kuvinjari mitaani bila ulinzi mkali. Tumuombe Mungu atunusuru, lakini Lowassa akishika nafasi ya juu ya uongozi PATAKUWA HAPATOSHI.