Ndugu zangu wa JF, hii ni breaking news: Sasa imethibitika kuwa yule waziri wetu mkuu ambaye aliamua kuachia ngazi kwa kuhusika; iwe moja kwa moja au vingevyo, anatarajia kurejea serikalini kwa nguvu zote na kwamba ameanza kujifananisha na alhaj Ali Hassan Mwinyi, yule rais wetu wa awamu ya pili.
Lowassa kasema atarejea kwa nguvu zote na hakika wabaya wake watakiona cha mtema kuni. Nadhani ana uhakika huo na habari zinasema ameshamueleza Kikwete, kumbukeni ni shwahiba wake mkubwa na ni jicho lake- elewa hajaomba ametaka. Na atapewa.
Miongoni mwa mikakati ya kurejea kwenye serikali ni eti kuhakikisha kuwa nia yake ya kuiongoza Tanzania inafanikiwa kwa njia yoyote ile. Kumbuka amekuwa na nia hiy siku zote mara baada ya kuingia kwenye siasa baada ya kuwa amechuma fedha nyingi kutoka AICC na maeneo mengine, ikiwemo kipato kikubwa kutoka kwenye nyumba zake nyingi Dar na Arusha ambazo zote ziko kwenye prime areas.
Endapo atakosa nafasi hiyo, amemuandaa mtu ambaye Kamanda wenu ameanza kumtafuta ili kuzungumza naye na baadaye kuweka maelezo yake JF.
Waandishi wa habari ni miongoni mwa watu waliotengewa fedha nyingi kwa kazi hiyo. Miongoni mwa mikakati ya awali ni kugeuza mwelekeo wa kumtengeneza Lowassa rais wa mwaka 2015 na kumsafisha kwanza kwa kutumia magazeti ya Mtanzania, Rai, The African, Tazama na huenda fedha hizo zikapenyezwa kwenye vyombo vingene.
Haya kazi kwenu wana JF- huenda tukampata Rais Lowassa, rais Rostam au Rais Msabaha miaka michache ijayo.
Tuinusuru Tanzania yetu kwa nguvu zote.