Lowassa anasafishwa!

Lowassa anasafishwa!

Mkuu sio Mandela tu alisema hayo, hata Nyerere Pia.
Movement we need to put words into action, tuwe na action Plan na tuanze kuimplement mara moja! Wazo la movement ndio wazo la kulipa kipaumbele.

Nakushauri usome Steve Biko " I write what I Like" na Vitabu vya Taylor Branch 1. Parting the Waters, 2. Pillar of the Fire 3. At Canaan's Edge. These books have changed my Life and they have streghthened my belief on a real movement must impower and involve the community afflicted at large. Let us start Now!

Mkuu nakupa TANO !

Mkuu wangu mbogela,

Nashukuru sana kwa reference books ulizonipa.Bravo bro,more credit kwako mkuu
 
Nina mashaka na Attachment za Kolokiro waungwana, nway midhari zipo jamvini ngoja tuzisome tu.
 
Mtandao wa Rostam, Karamagi na Lowassa umeanzisha magazeti mapya manne: NYUNDO, MTANDAO, UMMA na TAIFA kwa lengo la kuwasafisha mafisadi hao na kumtisha Kikwete aone kuwa Urais wake uko hatarini kuporwa na kundi linalopigana kufa na kupona dhidi ya ufisadi Serikalini. Magazeti hayo mapya manne yanaungana na magazeti yao mengine manne ya RAI, MTANZANIA, TAZAMA na ASUMIN kuendeleza mkakati huo wa kumfanya Lowassa Rais mwaka 2010. Wanaposema 2015 ni geresha tu, danganya toto. Tayari kikao chao cha KALOKIRO kimemteua Lau Masha kugombea Urais ikiwa kazi ya kumsafisha Lowassa itashindikana kufikia mwaka 2010.
Jopo kubwa la wandishi mamluki, likiongozwa na Prince Bagenda,Charles Charles, Deodatus Balile, Mhingo Rweyemamu na Manyere Jackton, linayaendesha magazeti hayo kwa malipo makubwa. Lazaros

Umesahau MAJIRA

Asha
 
wana JF,nimefanikiwa kupata baadhi ya minute za vikao vya KALOKIRO,hi itatusaidia kuwaelewa hawa mafisadi vizuri zaidi.
angalia attachements
hizo minutes zako ni za uongo mkubwa kwa sababu zifuatazo......kwanza ni kuwa tarehe 10/05/08 hicho kikao kilifanyika wapi?mimi najua tarehe hio mh Rostam alikuwa yuko ziara nzega, mh lowasa alikuwa yuko UK,mh Masha alikuwa kanda ya ziwa kwa ile ziara ya siku tatu.mh nchimbi alikuwa yuko ktk kikao cha mawaziri wa ulinzi wa sadec kilifanyika Angola.
Pili hakuna namna unaweza kusema kuwa mzee wasira anaweza kuwapinga kina Rostam.huo ujanja hana kwa kuwa ana thamini urafiki wao.Pia huwezi kuwaunganisha pamoja Wasira na Sita.si kweli ni marafiki ata kidogo.
Mwisho ni kuwa ata siku noja hawa jamaa wakikaa huwa hawaandiki andiki minutes, kama hawakuwa wakiandika wakati wa kikao cha mtandao wataandika now?...pia hakuna kikao kama hicho hayo ni mambo ya watu wajinga ambao hawana mkakati wowote wenye ushindi....unapomuongelea Rostam ujue unaongelea kichwa chenye akili mara kumi ya vichmwa vyenu wote hapa jamii forums
 
Nakubaliana na wewe 100 per cent. Uandishi wa magazeti haya ni wa kitoto, haufichi maslahi ya wazi ya mafisadi hao. Lakini, kama Mbunge mmoja alivyosema hivi karibuni, Watanzania si mabwege wa kuendelea kuchezewa na wajinga wachahche waliolewa kwa utajiri wa kupora. Hivi Lowassa kweli anadhani anaweza siku moja kuwa Rais wa Tanzania, Karamagi Waziri Mkuu na Rostam Waziri wa Fedha? Wajaribu tuwashikishe adabu.

Ikitokea nahama nchi
 
Utawajua tu watu wanaolipwa na mafisadi, shame, shame shame!
 
Nakubaliana na wewe 100 per cent. Uandishi wa magazeti haya ni wa kitoto, haufichi maslahi ya wazi ya mafisadi hao. Lakini, kama Mbunge mmoja alivyosema hivi karibuni, Watanzania si mabwege wa kuendelea kuchezewa na wajinga wachahche waliolewa kwa utajiri wa kupora. Hivi Lowassa kweli anadhani anaweza siku moja kuwa Rais wa Tanzania, Karamagi Waziri Mkuu na Rostam Waziri wa Fedha? Wajaribu tuwashikishe adabu.

Nionavyo mimi JK ndiyo anawapa pumzi kutokana na uoga wake na kuendekeza ushkaji na hiyo itamgharimu sana na ni wazi kuwa anaweza akapoteza Urais mwaka 2010.

Watz wengi na baadhi ya Wabunge makini wa vyama vyote ikiwemo CCM wamejitolea sana sana kumpa clue ali achukue hatua dhiid ya hao Marafiki zake Mafisadi lakini wapi na sasa wanamgeuka!

Akitaka anusurike lazima achukue hatua ili imani ya WaTz kwake irejee na tutam-support kikamilifu vinginevyo tutamtosa na kumweka kundi moja na hao Manyang'au na Mafisadi.
 
1. Sina ufahamu mzuri kuhusu Badra.
Naomba tafadhali nitengenezewe chain yake hapa hapa mtandaoni.

2. Mafisadi wana mbinu nyingi sana. Msikurupuke kutoa hukumu dhidi ya hoja yoyote iliyotelewa dhidi ama kuwalinda mafisadi. Jipangeni vizuri zaidi.
Wanaweza kuwapotezea muda mwingi mkijadili jambo fulani ili wawe huru kwenye eneo lao nyeti zaidi.
 
1. nawaombeni sana muweke hiyo issue inayomhusu Badra hapa mtandaoni. Mimi sina habari ya kutosha kuunganisha dots zake.

2. Ninalazimika kuwapa tahadhari mnapojadili hoja ya kuwaponda au kuwaunga mkono mafisadi kwani wanatumia mbinu nyingi sana kuendeleza udhalimu wao. yawezekana hoja ikatolewa (tena Nzito) lakini nia kamili ya hoja hiyo ni kuwaweka busy wanazuoni ili wao mafisadi wawe free kuendelea na uharamia wao mwingine.
Ndivyo pia wanavyofanya wanapoona kuwa mijadala inaelekea kuingilia sana maslahi yao.
 
Kuhusu uanzishaji wa magazeti hiyo hainitishi sana.
Wacha waanzishe. Wananchi wanachagua wenyewe pumba na mchele!!
MSIOGOPE madanganyo haya yana mwisho
 
Nina mashaka na Attachment za Kolokiro waungwana, nway midhari zipo jamvini ngoja tuzisome tu.

Hata mimi nina wasiwasi nazo ... hao jamaa siwapendi kwa sababu ya "udhalimu" wao, lakini sidhani kwamba ni "wapumbavu" kiasi hicho!
 
Kwani maisha ni mpaka uwe kiongozi?. Kwanini wasifanye kazi nyingine kama watu wengine?. Kuna kitu gani hasa wanatafuta katika huo uongozi?.

Wana JF nani anaweza kunipa namba za simu za watu hao (Karamagi, Rostam na Lowassa) ili niwapigie na kuwaeleza ukweli?. Wasijione miungu watu hata kidogo.
 
Watanzania wengi wana njaa na wamezoea kununuliwa wakati wa uchaguzi kwa kikombe cha uji na pea ya kanga. Fikra ziko kwenye mtungi na wala sio maendeleo ya nchi na jamii.
 
Kwani maisha ni mpaka uwe kiongozi?. Kwanini wasifanye kazi nyingine kama watu wengine?. Kuna kitu gani hasa wanatafuta katika huo uongozi?.

Wana JF nani anaweza kunipa namba za simu za watu hao (Karamagi, Rostam na Lowassa) ili niwapigie na kuwaeleza ukweli?. Wasijione miungu watu hata kidogo.

Kwa Tanzania ya CCM, UONGOZI ni UWEKEZAJI. Tena uwekezaji usiohitaji mtaji au mkopo kutoka benki.
 
Kama wenyewe wanakiri kuwa wanataka 'kusafishwa' basi kwa namna nyingine wamekiri kuwa 'wamechafuka.' Tuanzie hapo
 
Back
Top Bottom