Lowassa afunika dar

Lowassa afunika dar

Nape akae mkao mzuri naona fisadi anakuja kwa kasi! Lowassa ni maarufu kuliko CCM. Ukweli ndio huo

umenifurahisha mkuu, huyo ndio next president...wakubali ndio hivo hivo wakatae ndio hivo hivo..
 
Hivi huyu mamvi akigombea 2015 magwanda watamsimamisha nani ashindane nae? Mbowe? au Slaa?

kwi kwi kwi teh teh teh!

cc Pasco, Ben Saanane, Yericko Nyerere, Godbless J Lema, Dr.W.Slaa, Josephine
FF, Siasa hazitabiriki, EL anaweza kuwa ndie mgombea wa Chadema kama CCM ispomsimamisha kwa maana mimi naujua msimamo wa Dr.W.Slaa kuhusu kugombea 2015, na nimeusikia kwa masikio yangu mwenyewe, tena wakati anautoa msimamo wake, na Josephine alikuwepo!, ila kwa vile aliutoa tukiwa katika mazingira ya off the record, hivyo siwezi kuuweka humu!
Pasco.
 
CCM itafanya kosa kubwa sana kumsimamisha Lowassa kuwa mgombea wa Uraisi kwa tiketi ya CCM. Lowassa ana machafu na mabaya mengi ambayo yanaweza kumuangusha vibaya sana. Hii ni ishara ya kuiachia Chadema kuingia Ikulu.

Tukumbuke katika uchaguzi wa jimbo la Arumeru mashariki jinsi Lowassa alivyouumbuka wakati akijaribu kumpigia kampeni mkwe wake dhidi ya mgombea wa Chadema.

Kuna watu safi na wazuri ndani ya CCM ambao wanakubalika nje na ndani ya chama. Hawana doa la ufisadi na ni waadilifu, wana uzalendo wa kweli na Tanzania yetu na wana uwezo wa kujenga na kupangua hoja.

Kwa maoni yangu ninamuona Mh Wassira tu ndiye mwenye uwezo wa kusimama na kupeperusha bendera ya CCM katika kugombea kiti cha Uraisi.

chadema kushika nchi?? no way out u r not serious
 
Laigwenan noma....kaeni chonjo.

Aliingia kichwa kichwa Arumeru akapigwa mweleka, akaingia kichwa kichwa Arusha akapigwa mweleka. Tunamsubiri kwenye uchaguzi.

Lowasa amekuwa kiongozi hapa nchini for ages na nchi ni moja kati ya masikini duniani japokuwa inaongoza kwa rasilimali duniani. He is a failed leader who knows how to manipulate the minds of those whom he has stolen their wealth.
 
FF, Siasa hazitabiriki, EL anaweza kuwa ndie mgombea wa Chadema kama CCM ispomsimamisha kwa maana mimi naujua msimamo wa Dr.W.Slaa kuhusu kugombea 2015, na nimeusikia kwa masikio yangu mwenyewe, tena wakati anautoa msimamo wake, na Josephine alikuwepo!, ila kwa vile aliutoa tukiwa katika mazingira ya off the record, hivyo siwezi kuuweka humu!
Pasco.

Nahisi kuna kitu kinapikwa jikoni hapa ambacho ni hatari sana kwa CDM na dr slaa!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Urais unaotafutwa kwa hela mingi hivi akiukosa atafanya nini??
 
alichoweza lowasa ni kuwanunulia vifulana hao bodaboda, lakini hana mpango nao. angekuwa na mpango mzuri angeanzisah kiwanda kikubwa kwa pesa alizotuibia ili atoe ajira.
 
Kipindi hiki kila mtu atafunika. Nafikii hatana mimi ngoja niende nikafunike kule kwenye kijiji changu nilipokulia.
 
FF, Siasa hazitabiriki, EL anaweza kuwa ndie mgombea wa Chadema kama CCM ispomsimamisha kwa maana mimi naujua msimamo wa Dr.W.Slaa kuhusu kugombea 2015, na nimeusikia kwa masikio yangu mwenyewe, tena wakati anautoa msimamo wake, na Josephine alikuwepo!, ila kwa vile aliutoa tukiwa katika mazingira ya off the record, hivyo siwezi kuuweka humu!
Pasco.

La kugombea chadema naamini inawezekana wakati wowote ule, maana wakishikishwa wanamwachia hata shetani agombee.
 
Atawajibishaje wezi wakati yeye ndiye fisadi Mkuu (papa).
Alifisidi Richmond, EPA, KAGODA wakishirikiana na Rostam.
Kwa sasa anakurudishieni pesa aliyoiba.

Lokissa:
wamrudishie basi uwaziri mkuu wake
bora yeye ana uthubutu na sio Pinda
JK umebakiza muda mfupi mpe Lowassa uwaziri mkuu afanye kazi
huyu ana hela hatakuwa na tamaa za kuiba,atawawajibisha wezi na wazembe
 
Huyu jamaa ni kiboko.cdm wakisikia jina lake kitu kinagonga chupi

Ndiyo upumbavu tulionao sisi watanzania, nimeamini akili ya kufikiri au kutizama mbali hatuna kabisa. Nakumbuka kipindi kile wakati Lowasa natuhumiwa kwa masuala yake ya rushwa mpaka akifikia hatua ya kujiuzulu karibia asilimia yote ya watanzania tulimchukia sana huyu muheshimiwa na tliunga na kufurahia ile kamati ya akina Mwakyembe ya kufichua mafisadi. Nashangaa leo tena hata sijui inatokea wapi nakuta watanzania tunatokea kumpenda Lowasa na kuona kama ndiye mkombozi wetu, hivi najiuliza huyu jamaa kuna kitu gani ameifanyia nchi mpaka inafikia kupendwa kiasi hiki wakati tulimchukia sana ?. Nkumbuka pia Jakaya tulimpenda sana na tukaona ndiye atakuwa mkombozi wetu lakini leo hii hatutaki hata kumskia jina lake kwenye maskio yetu, hii kitu ya kumpenda mtu kulingana na uwezo wake kifedha, muonekano wake ya kimaumbile, dini yake na hata kabila ndiyo vigezo ambavyo watanzania wengi wapumbavu, wasiojielewa, wasiokuwa na future pia wavivu kufikiria ndio wanavitumia katika kumchagua mtu awe kiongozi wao bila kujali vile vigezo stahiki ambavyo mgombea yoyote wa uongozi awe navyo. Sisemi kama Lowasa anataka kugombea ila nimefikiria mbali kidogo kwamaba endapo itatokea huyu jamaa akasimama kwenye uchaguzi nina uhakika atashinda tu maana ameshateka wapumbavu wengi na ndio ambao wengi wana kadi za kupigia kura
 
La kugombea chadema naamini inawezekana wakati wowote ule, maana wakishikwa wanamwachia hata shetani agombee.
Kwenye politics hakuna permanent friends wala enemies only comon interest, Adui wa CCM ni Chadema, na adui wa Chadema ni CCM. El amepania lazima agombee kupitia CCM, ikitokea CCM isipomsimamisha 2015, EL atakuwa ndio adui number 1 wa CCM. Kwa vile Chadema inautaka urais na zaidi ya Zittto hawana mtu mwingine yoyote, the adui wa adui yako ni rafiki yako!, na ndipo hapo itakapomkumbatia EL na kumbeleza, akikubali ku cross, CCM itameguka pande kubwa nono na ndipo litatimie lile neno, "rais bora wa Tanzania, lazima atatoka CCM!" na hapo ndipo akina sisi tutajiunga siasa na ndio the only way kwa Chadema kutinga ikulu!, there is no any other way!. Fuatilia kwa makini viongozi wa Chadema kama wanathubutu kumsakama EL!.
Pasco.
 
Mtaji wa CCM ni wajinga kama hawa..Tena wanaonekana vijana..Tuendelee kushabikia matokeo tutayaona...

Wa-Tanzania mnasikitisha..Hata kama ni ugonjwa wa kusahau..

Huu ni Ukichaa..

Afrika hii ni nani aliye mjanja? labda wewe peke yako.
 
Kiongozi Kama Luwasa hatufai Tanzania maana ni mtu ambae anautafuta Urais kwa njia yeyote ile, bwana luwasa usilamishe jambo huenda halina kheri na wewe,vipi kiongozi msomi kama yeye anaweza sema haya mabodaboda ni ajira kwa vijana wakati akijua huu usafiri nia madhumuni yake si chombo cha kubeba abiria na ni sawa kutumia kwasababu ameona liberia na Uganda wanatumia usafiri huo, amekuwa kama yule dereva anapita barabara ambayo hairuhusiwi kupita lakini kwasababu dereva mwengine kapita na yeye anamufauata.Luwasa anaona mbele ya macho yake jinsi vijana na wananchi wanavyo kufa na kuwa vilema na hayo maboda boda na pia zinavyotumika kwa vitendo vya wizi kwa kukosa kazi, lakini anaona ni sawa kwasababu ya kiu za kupata kura.Serikali inabidi iwatafutie ajira ya kweli hawa vijana siyo kuwadanganya hiyo ni ajira ili mradi apate kura zao, semeniukweli mumewashindwa vijana sasa wakiendesha boda boda au wakiwa machinga sawa na mwisho wengi wao wanaishia kuwa wezi.
 
Ndiyo upumbavu tulionao sisi watanzania, nimeamini akili ya kufikiri au kutizama mbali hatuna kabisa. Nakumbuka kipindi kile wakati Lowasa natuhumiwa kwa masuala yake ya rushwa mpaka akifikia hatua ya kujiuzulu karibia asilimia yote ya watanzania tulimchukia sana huyu muheshimiwa na tliunga na kufurahia ile kamati ya akina Mwakyembe ya kufichua mafisadi. Nashangaa leo tena hata sijui inatokea wapi nakuta watanzania tunatokea kumpenda Lowasa na kuona kama ndiye mkombozi wetu, hivi najiuliza huyu jamaa kuna kitu gani ameifanyia nchi mpaka inafikia kupendwa kiasi hiki wakati tulimchukia sana ?. Nkumbuka pia Jakaya tulimpenda sana na tukaona ndiye atakuwa mkombozi wetu lakini leo hii hatutaki hata kumskia jina lake kwenye maskio yetu, hii kitu ya kumpenda mtu kulingana na uwezo wake kifedha, muonekano wake ya kimaumbile, dini yake na hata kabila ndiyo vigezo ambavyo watanzania wengi wapumbavu, wasiojielewa, wasiokuwa na future pia wavivu kufikiria ndio wanavitumia katika kumchagua mtu awe kiongozi wao bila kujali vile vigezo stahiki ambavyo mgombea yoyote wa uongozi awe navyo. Sisemi kama Lowasa anataka kugombea ila nimefikiria mbali kidogo kwamaba endapo itatokea huyu jamaa akasimama kwenye uchaguzi nina uhakika atashinda tu maana ameshateka wapumbavu wengi na ndio ambao wengi wana kadi za kupigia kura
Siku zote nabii huwa hakubaliki nyumbani!. Sometimes you can never know what you have until when you loose it!. JK alipoingia na ile timu yake ya askari wa miamvuli, watu walikuwa na too great expectations, hivyo EL aliposingiziwa kuboronga, alitishwa msalaba ili kwa kuteswa kwake CCM iokoke!. Kilichofuatia hapo ni majanga na majanga kila siku iliyopita ilikuwa ni afadhali ya jana!, ndipo watu wakaujua uwezo wa huyu jamaa!. JK alishine mwanzo kwa kusafiria tuu nyota ya EL, na baada ya kumuengua, nuru ilitoweka!. Watanzania sasa wanajua wanataka nini na nani anayeweza kuwapatia kile wanachotaka!. Sio vyama tena bali ni watu!.

Hili la Watanzania kuwa ni wapumbavu nalo neno!, kwani CCM imetifanyia nini tangu uhuru na kila siku tunaendelea kuichagua na mwaka 2015 tutaichagua tena!. Tulipomchagua JK 2005 na 2010, tulimchagua kwa sifa zipi zaidi ya sura?!. Kwani Watanzania huwa tunachagua nini haswa?!, hivyo kutuita wapumbavu inaweza kabisa ukawa hujakosea, ila kwa 2015, itategemea kama tutaendeleza upumbavu ule ule au tumeeruvuka sasa tutachagua watu wa ukweli?!.
Kwa wote waliopo, hakuna yeyote anayemkaribia EL kwa karibu labda Magufuli ila ni kwa mbali sana!.
Pasco.
 
Hivi kinacho endelea ni nini hapa? Mambo/tukio la kawaida linakuzwa out of proportion au ndio wanamtandao wapya wanajaribu ku-jump guns kabla ya kampein za Urais kuruhusiwa rasmi - je hii ni bahati mbaya au ni a well organised scheme ya kutaka kuwazidi kete wenzake wenye nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya CCM come 2015 - kama ningekuwa mimi ningewambia wapiga debe wangu wa-hold fire wasubiri D-Day. Inashangaza sana kuona baadhi ya wana JF walivyo pania kuweka chumvi mno kuhusu wasifu wa muhusika, wanayasema hayo wakati hawana uhakika kama chama tawala kitampendekeza yeye? Mimi naona ushabeki huu uliopitiliza mipaka wa kujaribu kumpamba pamba ndio kunaweza kumuharibia chance ya kuteuliwa - tuwe na subira tusilazimishe mambo.
 
Back
Top Bottom