Kwa maoni yangu, kwa mfumo wetu wa utawala wa demokrasia hii ya kurukia, yenye kujaa fitna, umbeya, ushabiki na chuki, hakuna mwenye uwezo wa kuthubutu atakayesimaa. Maige alithubutu kuwanyima wazungu vitalu. Maige alithubutu kufunga biashara ya wanyama hai na hivyo kuokoa twiga wetu. Walioathirika na maamuzi hayo wakampiga fitna na kwa nguvu ya mchezo mchafu kwa kamati, yakamkuta yaliyomkuta na leo watanzania wanaitikia chorus hiyo kuwa Maige alisafirisha twiga wakati yeye ndiye aliyewaokoa.
Kwa hakika, tusipokuwa na mfumo mzuri wa kuchunguza tuhuma kabla ya hukumu zinazoratibiwa kwa mob bungeni, kwa kushadidiwa na wabunge ambao wengi wao wamethibitika kuwa si waadilifu (kwani wapo wanaochukua posho bila kusafiri na wengine wanaiba hata mikufu!!!), hakuna atakeyesimama.
Maamuzi yoyote magumu huumiza watu. Lazima uwepo mfumo wa kujiridhisha pale tuhuma zinapozuka kwa mtu, kwani mara nyingi wengi wanaoathirika na maamuzi hayo ya viongozi wazalendo hupanga njama za kuwaangamiza wachapakazi.
Leo tunamkumbuka sana Sokoine (kwa vita ya uhujumu uchumi na ulanguzi) na Mzee Kawawa kwa operesheni vijiji. Wote hawa walisababisha madhara makubwa kwa watu. Wapo watu waliotupa mali zao kwa kumwogopa Sokoine. Kama mfumo ungeruhusu majungu, Sokoine angepigwa jungu moja tu na asingesimama tena!!
Kawawa kadhalika, watu waliliwa na simba porini na wengine waliteseka kwa kuvunjiwa nymba zao na kuishi chini ya miti wakinyeshewa mvua, lakini kwa kutokuwepo akina Hellen Kijo Bisimba, alipona. Ajaribu leo tuone!!! Hatamaliza wiki.
Kwa kuwa nyakati zimebadilika, nasi lazima tubadilike, vinginevyo, wazuri wote wataisha, watabaki wasanii wenye kwenda na wakati na upepo!! Pale wazee wakitaka gesi yote ivunwe na wageni wataimba wimbo huo kwa nguvu zao zote, lakini akija mtu akasema anataka watanzania wapate kipaumbele kwenye gesi yao, nao watageuka na kuimba wimbo huo kwa nguvu zao zote!!
Tunahitaji watu ambao they are solid na wazalendo wa kweli!??
lakini kumbukeni
Wungwana....katika nchi ambayo kila mtu hata Mawaziri na W/mkuu aliyepo anailaumu SERIKALI...ni jambo la kushangaza na kustabisha kabisa.
Hata huko Ulaya au America walikopiga HATUA za maendeleo.... UONGOZI, USIMAMIZI SAHIHI au EFFECTIVE MANAGEMENT ndio SILAHA YAO KUU. Waweza kuwa na kuwa na MIPANGO BORA KABISA NA FEDHA ZA KUFANYA YOTE MAZURI...kama HII Serikali ya CCM ilivyo na mipango BORA na fedha....LAKINI KAMA HATUA NIDHAMU YA KAZI NA MATUMIZI YA HIZO FEDHA NI KAZI BUREEEEEEE.
Ni ajabu kumwona Waziri, au Mkurugenzi wa Halmashauri au wa shirika eti analaumu Serikali kwa kushindwa. HIVI SERIKALI NI NANI HASA?????
Kinachohitajika HAPA TZ ni KIONGOZI THABITI mwenye UWEZO wa KUVUNJA MFUMO HUU WA KUJUANA SERIKALINI na kuogopana uliodumu kwa zaidi ya miaka 50.
Hata akija Lowasa/Dr. Slaa/ Migiro /Mwakyembe au hata NANI UNAYEMJUA...bila KUVUNJA MFUMO HAKUNA KITU.
JK ameshindwa...coz anateua watu kwa kuangalia mtandao/urafiki/undugu/ujirani/uchama n.k Hana uwezo wa kuwakemea kama alivyokuwa anafanya NYERERE na Sokoine.
Nchi inahitaji KIONGOZI JASIRI anayeweza kufanya maamuzi SAHIHI kwa wakati sahihi bila kuangalia mtu/urafiki/uchama n.k
Namkumbuka sana SOKOINE. Alikuwa mwananchi mzalendo sana.
Ni mtazamo wangu tu.