Lowassa afunika dar

Lowassa afunika dar

Watanzania walio wengi wanafikiri kwa matumbo... Mafisadi lazima wawaburuze..
 
Siku zote nabii huwa hakubaliki nyumbani!. Sometimes you can never know what you have until when you loose it!. JK alipoingia na ile timu yake ya askari wa miamvuli, watu walikuwa na too great expectations, hivyo EL aliposingiziwa kuboronga, alitishwa msalaba ili kwa kuteswa kwake CCM iokoke!. Kilichofuatia hapo ni majanga na majanga kila siku iliyopita ilikuwa ni afadhali ya jana!, ndipo watu wakaujua uwezo wa huyu jamaa!. JK alishine mwanzo kwa kusafiria tuu nyota ya EL, na baada ya kumuengua, nuru ilitoweka!. Watanzania sasa wanajua wanataka nini na nani anayeweza kuwapatia kile wanachotaka!. Sio vyama tena bali ni watu!.

Hili la Watanzania kuwa ni wapumbavu nalo neno!, kwani CCM imetifanyia nini tangu uhuru na kila siku tunaendelea kuichagua na mwaka 2015 tutaichagua tena!. Tulipomchagua JK 2005 na 2010, tulimchagua kwa sifa zipi zaidi ya sura?!. Kwani Watanzania huwa tunachagua nini haswa?!, hivyo kutuita wapumbavu inaweza kabisa ukawa hujakosea, ila kwa 2015, itategemea kama tutaendeleza upumbavu ule ule au tumeeruvuka sasa tutachagua watu wa ukweli?!.
Kwa wote waliopo, hakuna yeyote anayemkaribia EL kwa karibu labda Magufuli ila ni kwa mbali sana!.
Pasco.

Mkuu Pasco may be wewe tupo pamoja ila tunatofautiana kitu kidogo sana, mimi sijampinga moja kwa moja huyu Lowasa ila mara nyingi sana huwa napenda kusikiliza mijadala ya kisiasa sehemu mbalimbali hasa kwa wananchi wa kawaida kwa mfano vijiweni, kwenye vyombo vya usafiri vya umma na sehemu nyingi zenye mkusanyiko wa watu wengi, sasa utakuta mtu anamsifia Lowasa na mara nyingi huwa napenda kumuuliza mtu anaielezee japo kwa ufupi sifa alizonazo huyu muheshimiwa mpaka aoanekane kama ndio mkombozi wetu, utakuta mtu tena baba mzima na anafamilia nyumbani anakupa sababu za kipumbavu ambazo kwa mtu mwenye akili timamu utaona kabisa unaongea na mtu asiyejielewa kiakili. Mimi kitu ambacho nilikuwa napenda watanzania tubadilike ni kwanza kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kufanya uamuzi wa kupiga kura yako bila kushwawishiwa na mtu mwingine kwa maneno matamu eti mtu fulani anafaa kwa sababu ni mkristo/mwislamu, kabila hili, ana utajiri sana n.k. Nimetumia kauli ya sisi kujiita wapumbavu maana ni watu tusiojielewa kuanzia wananchi mpaka viongozi wa juu, huu upumbavu wetu ndio unaotughalimu mpaka sasa, inauma sana nchi iliyojaa rasilimali nyingi kuliko nchi yoyote duniani lakini bado tumezidi kuwa masikini zaidi wa kutupwa duniani.
 
Mtaongea weee ila ss watanzania ndo tutaamua kama anafaa au hafai!!
 
Kiongozi Kama Luwasa hatufai Tanzania maana ni mtu ambae anautafuta Urais kwa njia yeyote ile, bwana luwasa usilamishe jambo huenda halina kheri na wewe,vipi kiongozi msomi kama yeye anaweza sema haya mabodaboda ni ajira kwa vijana wakati akijua huu usafiri nia madhumuni yake si chombo cha kubeba abiria na ni sawa kutumia kwasababu ameona liberia na Uganda wanatumia usafiri huo, amekuwa kama yule dereva anapita barabara ambayo hairuhusiwi kupita lakini kwasababu dereva mwengine kapita na yeye anamufauata.Luwasa anaona mbele ya macho yake jinsi vijana na wananchi wanavyo kufa na kuwa vilema na hayo maboda boda na pia zinavyotumika kwa vitendo vya wizi kwa kukosa kazi, lakini anaona ni sawa kwasababu ya kiu za kupata kura.Serikali inabidi iwatafutie ajira ya kweli hawa vijana siyo kuwadanganya hiyo ni ajira ili mradi apate kura zao, semeniukweli mumewashindwa vijana sasa wakiendesha boda boda au wakiwa machinga sawa na mwisho wengi wao wanaishia kuwa wezi.

aisee nchi hii tatizo kubwa tulilonalo ni WATANZANIA napo waona watu wazima wenye akili zao na upeo wanamshabikia Lowasa, Lowasa machozi yananitoka..... Nchi yetu haimalizwi na kina lowasa, rostam wala mafisadi wengineo... tunaoimaliza ni WATZ wenyewe mimi na wewe.

kwa aidha kujitoa ufahamu, na kusapoti watu ambao wazi kabisa wanaonekana.kuwa ni majanga.
 
Naomba kila siku ccm wampitishe huyu bwana kuwa mgombea 2015. Kazi ya mabadiliko iwe rahisi sana.
 
wajinga ndo waliwao..

Ni kweli wajinga ndo waliwao ... Watanzania tunashuhudia jinsi Lowasa anavyomwaga pesa zake kwenye harambee mbalimnali. Huyo si bure ana plani zake. Amepiga hesabu kuwa pesa hizo anazotoa sasa atazirudisha akiwa rais... Sijasikia Bakhresa au matajiri wengine Tanzania wakichangia kama yeye! Huu uzalendo huyu mwizi Lowasa akupata wapi leo hii? Watanzania hii hatujiulizi! Aliuacha wapi uzalendo wakati alipofanya dili la Richmond?

Leo Watanzania mnashabikia pesa za shetani? Kumbukeni Wajinga ndo waliwao!!
 
Kwa hili alieandaa hii kitu ni fisadi zaidi ya mafisadi yaani kamnunulisha mafulana kibao kisha kakusanyia maboda boda hadi washikaji wa vijiweni ilimladi tu watu wajae na yeye apige pesa yake fursa imetumiwa ipasavyo hapo
 
Kama kundi hilo lote limekusanyika kwa kupewa pesa basi kazi iliyo mbele yake siyo kubwa.

Hao wote wamepewa pesa (japo uchungu wangu ni pale vipesa vyenyewe wanavyopewa havilingani na kudhalilika kwao - are Tanzanians that cheap?)!
 
nyie wa jukwaani mmekula shilingi ngapi ,boda boda najua wamekunywa full tank kila mmoja.
 
wakati jk anapitishwa kugombea urais na NEC ya ccm nilikua kidato cha nne, tulishangilia sana mwalim wetu akatuasa kuwa tutajutia furaha yetu. saivi nawaasa vijana wenzetu tusijejuta kwa ushabiki unaoponzwa na njaa zetu za sikumoja au mbili, hawa watu watafidia pesa yote wanayochezea. mfano mzuri ni jk, leo anamiliki rasilimalizetu kias gan
 
wakati jk anapitishwa kugombea urais na NEC ya ccm nilikua kidato cha tano, tulishangilia sana mwalim wetu akatuasa kuwa tutajutia furaha yetu. saivi nawaasa vijana wenzetu tusijejuta kwa ushabiki unaoponzwa na njaa zetu za sikumoja au mbili, hawa watu watafidia pesa yote wanayochezea.
mfano mzuri ni jk, leo anamiliki rasilimalizetu kias gan
 
ZZK your career is over like Mike anyone Tyson,Jackson,Jordan.

....malizia mzee "ridiculous!!!!"......mzee umanikumbusha mbali sana na strong lines za one of the greatest mc to ever grace the m.i.c ,the one and only biggie smallz!RIP
 
Ndiyo upumbavu tulionao sisi watanzania, nimeamini akili ya kufikiri au kutizama mbali hatuna kabisa. Nakumbuka kipindi kile wakati Lowasa natuhumiwa kwa masuala yake ya rushwa mpaka akifikia hatua ya kujiuzulu karibia asilimia yote ya watanzania tulimchukia sana huyu muheshimiwa na tliunga na kufurahia ile kamati ya akina Mwakyembe ya kufichua mafisadi. Nashangaa leo tena hata sijui inatokea wapi nakuta watanzania tunatokea kumpenda Lowasa na kuona kama ndiye mkombozi wetu, hivi najiuliza huyu jamaa kuna kitu gani ameifanyia nchi mpaka inafikia kupendwa kiasi hiki wakati tulimchukia sana ?. Nkumbuka pia Jakaya tulimpenda sana na tukaona ndiye atakuwa mkombozi wetu lakini leo hii hatutaki hata kumskia jina lake kwenye maskio yetu, hii kitu ya kumpenda mtu kulingana na uwezo wake kifedha, muonekano wake ya kimaumbile, dini yake na hata kabila ndiyo vigezo ambavyo watanzania wengi wapumbavu, wasiojielewa, wasiokuwa na future pia wavivu kufikiria ndio wanavitumia katika kumchagua mtu awe kiongozi wao bila kujali vile vigezo stahiki ambavyo mgombea yoyote wa uongozi awe navyo. Sisemi kama Lowasa anataka kugombea ila nimefikiria mbali kidogo kwamaba endapo itatokea huyu jamaa akasimama kwenye uchaguzi nina uhakika atashinda tu maana ameshateka wapumbavu wengi na ndio ambao wengi wana kadi za kupigia kura
Wewe usiongelee watanzania wote, sema ulimchukia sio watanzania walimchukia. Halafu kutuhumiwa sio kosa. Akisimama atashinda sio kwa sababu ya pesa yake bali ni kiongozi pekee anae kubalika kwa takriban watanzania wote hata kwa wapinzani. Hivi umewahi kuwasikia CDM wakimsema vibaya huyu jamaa?Au na wao hawasemi kwa sababu ya pesa yake?
 
Huyu jamaa anasema Lowasa kafunika mie nasema hivi Lowassa hata akifunua kamwe hawezi kuwaongoza watanzania labda misukule wake kama wewe mleta uzi na familia yako mlozoea kula vya waume wenzenu bure

Haujiulizi pesa anayokuonga wewe kaitoa wapi? na ili iweje?
 
Huyu jamaa anasema Lowasa kafunika mie nasema hivi Lowassa hata akifunua kamwe hawezi kuwaongoza watanzania labda misukule wake kama wewe mleta uzi na familia yako mlozoea kula vya waume wenzenu bure

Haujiulizi pesa anayokuonga wewe kaitoa wapi? na ili iweje?

Kwani we umezoea kula vya wanavyotafuta wanawake?????? Chakula ww?
 
sasa unalia liaa nn,manake hata familia yenu inamkubali lowassa,sema tu ww ndo umekuwa kicnwa ngumu,lakin hatushangai,manake ili jamii itwe jamii lazma watu kama ww wawepo
Wewe mkono wako ni wa mjinga. Unaandika popote na lolote. Wewe familia yangu unaijua? Tumkubali Lowassa kwa lipi? Huyu angekuwa China angeishanyongwa, angekuwa Marekani, angekuwa jela na asingeingia kwenye siasa tena. Hapa Tanzania anategemea huruma ya watu kama wewe and the likes.

Najua unalipwa kuandika hivi ila watoto wako hawatalipwa na watakuwa watumwa kwenye taifa lao endapo huyu mtu atapata anachokitafuta. Natumia maneno ya waziri mstaafu, Fredrick Sumaye, "watanzania msipokuwa makini mtawakabidhi nchi wauza msdawa na mitandao yao" hels wanazogawa kwenye nyumba za ibada wanazipata kwa njia hizo na watazirudisha pindi wakimweka mwenzao. Sasa mimi na familia yangu tukubali nini hapo?

Kumbuka huyu mtu alishajiuzuru kwa kukubali kuliingiza taifa gizani hili ajipatie hela, ndugu yangu wewe ndo unaona ni mtu shujaa huyo?

Lakini si nyie nyie mlopewa kofia na kanga mkaona JK anawapenda? Endeleeni kuchimba ksburi. Kumbuka yupo Mungu pia.Kwa Mungu, Anayeliibia taifa mammilion kwa siku, anayepokea kofia na kanga, anayepewa boda boda, wote ni sawa....hivyo msidhani mtamnyooshea kidole Lowassa baada ya mambo kugeuka. Kama Mungu akimwadhibu Lowassa, hatawaacha ninyi pia.

Nchi ya Haiti maovu ya kushabikia ujinga kama huu yalikuwa yamefika mwisho. Watu kama Lowassa, wewe walikuwa wamejaa huko. Ilitumia sekunde 35 tu kuleta kilio kwa taifa lile. Sekunde 35. Si mtoto, si baba, si mama, si mzee....hakukuwa na kuchagua. Wote waliangamia.

Si huko tu, taifa za Burundi na Rwanda. Hawa nao ujinga wa chuki uliwafikisha kukatana mapanga na hakuna taifa lililoingilia kuwaokoa mpaka wakachoka.

Rafiki yangu, sidhani kama unaelewa naandika nini kwa jinsi ninavyokuona. Kina Lowassa wakishaipata nchi wataweka watu wao kuabzia usalama taifa hadi balozi wa nyumba kumi. Kama alivyofanya JK. Angalia usalama ulivyo sasa hivi.

Wakishafanya hivyo, hiyo pesa yao itarudi na wewe na mimi ndo tutailipa. Hutalalamika kwa sababu wao hawatatoa kucha na meno tu, watakuwa wanaua live hili hela yao irudi. Umeme tutalipa kwa bei wanayoitaka wao. Haitakuwa nchi tena. Kama unadhani sasa hivi nchi yetu inasifika kwa kuuza madawa, subiri hawa nashujaa wako waje. Watakuwa wanayasafirisha wenyewe na kwa sababu hiyo, tofauti kati ya tajiri ja maskini itakuwa kubwa muno. Hii ndo italeta machafuko nchini kwa sababu hata ukipewa buku 7, hazitakusaidia lolote kutokana na mfumuko wa bei. Utawala wa Lowassa hautakuwa na wapinzani. CDM, CUF na wengine, mkifanya mchezo huu ndo mwisho.

Sasa mimi na familia yangu kama unavyosema, tujue haya na tumkubali Lowassa? Hata inchi moja. Naipenda nchi yangu, napenda watu wake na zaidi naipenda familia yangu na kumwogopa Mungu, hivyo namkataa Lowassa kaka.
 
Back
Top Bottom