Loose ends Kifo cha Martha Towo

Loose ends Kifo cha Martha Towo

FROM WADAU MUINE UZITO WA HII KESI

Ni hivi;

1. Kuna tetesi zinasema alikuwa amtambulishe mchumba wake kesho yake tu

2. Alivyokuwa kanisani alipigiwa simu na kwa jinsi Mzee alivyoongea ni kama hao watu wabaya waliiga sauti ya boyfriend wake.

3. Alivyotoka kwenda kuitikia wito wa aliyedhani ni boyfriend wake, ndio akatokomea mazima.

4. Martha alikuwa na fahamu mpaka akataja namba za baba yake, so yawezekana pia kabla hajapoteza fahamu kabisa alitoa abc kwa familia ndio maana Mzee anaongea kwa confidence kabisa

5. Wauaji ni watu smart sana, walijua kanisani kuna CCTV so wao walikaa nje mbali kabisa ili hiyo CCTV isiwaone wala kuona usafiri wao.

6. Martha aliachishwa kazi mwezi mmoja nyuma, yawezekana kulikuwa na uchunguzi unaendelea na Martha angeweza kuwa mtoa ushahidi muhimu kwahiyo.

7. Kwa Scenario ya mauaji haya, hii ni dhahiri sio wivu wa mapenzi ila ni mambo ya kazi. Wauaji ni Professional killers na lazima wamekodiwa na watu wenye mpunga mrefu kuficha traces zozote za ushahidi.

8. Branch Manager na staffs wa BOA Kahama kazi mnayo

Mkuu, umeshasema hapo kwamba "presumably"...that means inawezekana polisi walizungumza naye au hawakuzungumza naye. Lakini pia, zingatia kwamba ukiwa hai tena ICU haimaanishi kwamba ni lazima uweze kuzungumza, pengine alikuwa anapumua tu lakini hoi bin taaban.

Aidha, hata kama aliweza kuzungumza, ushahidi wa huyu mgonjwa hauwezi kuaminiwa kama ulivyo kwa kuzingatia hali yake. Lazima ushahidi huu uhusianishwe na ushahidi mwingine ili kuupa nguvu.

Sheria ni sayansi. Shahidi namba moja akishakufa huwa kuna mambo mengi ambayo yanafifisha uzito wa ushahidi wa watu wengine.

In criminal litigations the standard of proof is BEYOND REASONABLE DOUBTS. Ishu inakuja hapo kwenye kuthibitisha bila kuacha shaka. Ndiyo maana watuhumiwa wengi wa makesi ya namna hii huwa wanaachiliwa huru hata kama ni kweli wametenda kosa.
"walimchoma moto akiwa hai na kumuacha afanikiwe kutoroka ili aweze kuongea maneno yatakayopelekea upeleleza kuhama mbali kabisa na sababu ya tukio hilo"

Unaweza kuelezea kidogo hapa mkuu. Kitu gani kingelisababisha aongee maneno yanayoweza kuondoa ushahidi wa tukio baada ya kufanikiwa kupona kifo?
Kuna uwezekano wauaji walimfuatilia mienendo yake na kumfahamu na kum mark vya kutosha.
Inawezekana, baada ya kumteka wakawa wanampiga biti kwamba siku nyingine iwe fundisho kwa wanaopenda kuingilia either mahusiano ya watu au mambo yasiyomhusu kitu ambacho kinakuwa rahisi kwa marehemu ku connect dots na kujua watu hawa watakua ni akina fulani au wametumwa na fulani (hapo wauaji wanazidi kujijengea kinga ya jata kuhisiwa)
Kitu ambacho kitapelekea vyombo vya uchunguzi vilivyomhoji kuelekeza nguvu zao ambako maelezo ya marehem yameelekeza.

Wakati kiuhalisia kifo cha marehemu kitakua kinahusiana na tukio la yofauti kabisa na maelezo ya marehemu.

Cha kufanya, wajaribu kufanya tracking katika biashara za marehemu tangu akiwa Babati hadi alipohamia Kahama.

Waangalie manunuzi aliyowahi kuyafanya na malipo yake yalikuaje.

Waangalie mazingira ya kuacha kazi yalikuwaje, na mahusiano aliyokua nayo na wateja wa bank kote alipowahi kufanyia kazi.

Waangalie mahusiano na wafanyakazi wenzake, hasa wale wafanya kazi wenzake ambao ni 'Partners in Crime' ambao huku uswahili huwa tunapenda kuwaita 'Pika pakua'. Lazima kuna issue ya mgao iwe inahusika hapo.

Nina uhakika mpaka sasa wana taarifa za kutosha kuhusiana na jinsi alivyoondoka kanisani.
Pale Kahama lazima kutakua na eneo pendwa ambalo marehemu alikua akipenda kutembelea akiwa na watu fulani, ni muhimu sana kuipitia nayo.
Mkuu umeeleweka vyema, Proof beyond any reasonable doubt sio swala la mchezo. Wanaweza kuwakamata lakini kuthibitisha uhusika ni kazi nyingine. Japo sijaifatilia na pia siijui hii kesi, ila maneno yako yana ushawishi. Nitaifatilia Mkuu
 
Familia iko kwenye msiba mzito. Tunawapa pole. Ni kifo kinachotokana na mauaji hivyo hakiwezi kukosa mijadala na msingi wa hiki kifo cha mauaji lazima kiwe na sababu, kiwe na viashiria.

Kiwe na mhusika/wahusika wakuu
Kiwe na bajeti
Kiwe na watendaji/watimiza lengo. Kwa msingi huu wauaji
Kiwe na mpango kazi
Kiwe na fool proof
Kusiwe na dosari kuanzia kupanga, kutekeleza na hatimaye kutawanyika na kumalizana kama kuna malipo ya mwisho yalikuwa bado

Uchunguzi wa kifo hiki ni rahisi sana na si chini ya watu 20 wanaweza kuhusishwa nacho, ambapo watachujwa mpaka watabaki si chini ya watano .. Na ni uchunguzi rahisi kutokana na makosa mengi waliyofanya wauaji.. Hawakuwa wajuzi maana wajuzi huwa hawaachi alama! Japo kuna kosa moja dogo sana hufanya na kufumua mpango wote.

Uchunguzi wake utaanzia kazini kwake, maisha yake nje ya kazi, marafiki zake, wateja wake, mishe na dili zake, mawasiliano yake pamoja na mahusiano.. Hapa ni kwa ajili ya ku 'establish' Msingi wa kesi na 'motive' ya muuaji/wauaji.

Uchunguzi wa pili ni eneo lilikofanyika tukio.. Pori la Mitamba linalosifika kwa matukio ya mauaji, Mitamba halina tofauti sana na Mabwepande na kama linaweza kuchunguzwa vizuri kuna maiti ngingi mule zinaweza kuwa zimezikwa.

Mitamba liko Kibaha njia ya kwenda Bagamoyo eneo linaitwa Pangani.. Sehemu kubwa ya pori la Mitamba ni eneo la wizara ya mifugo na uvuvi na kuna kipindi matapeli wa viwanja Kibaha walilivamia na kuwauzia watu viwanja mpaka serikali ikaingilia kati.

Marehemu ni mkazi mwenyeji wa Kibaha Kwambonde kakulia hapo, kosoma Tumbi nknk. Wazazi wake wanaishi hapo mpaka sasa na ni watu unaoweza kuwaita maarufu eneo hilo na hata kanisani kwao Tumbi. Kwanini muuaji/wauaji wakachagua kuja kummaliza 'nyumbani kwao'?

Marehemu alisafiri salama salimini toka kituo chake cha kazi Shinyanga mpaka nyumbani Kwambonde Kibaha. Pengine alitumia ndege, usafiri binafsi au wa jumuiya lakini alifika salama.

Je, wauaji walikuwa wanamfuatilia kote huko?
Je, wauaji ndio walimuita aje Kibaha?
Je, lengo lake la kuja nyumbani Kibaha lilikuwa ninini?
Je, mpango wa kummaliza Kibaha pori la Mitamba ulikuwa mpango plan A au B?

Marehemu siku ya tukio alikuwa kanisani na ndugu zake.. Ni wazi alipata wito wa kuitwa nje mara moja ama kwa ishara ya mtu alikuwa ndani ya kanisa ama kwa simu kwakuwa mikoba yake aliacha alipokuwa kaketi. Hakurudi!

Ni wazi walimuita walikuwa nje kabisa ya kanisa barabarani! Kanisa la KKKT Tumbi liko pembezoni mwa barabara ya kuelekea Tumbi hospital. Ni wazi kulikuwa na gari ambalo ama alipanda kwa hiari ama kwa lazima/Kutekwa.

Ni wazi safari ilianza kuelekea Pangani pori la Mitamba.. Macho ya marehemu yata 'reveal' kilichotokea ndani ya gari kwa hicho kipindi chote mpaka kufika Mitamba kumwagiwa Petrol na kuchomwa moto!



Ukurasa wa pili juu ya mpango kazi ambao ninaamini ndio plan A.

Wauaji waliona eneo salama la kummaliza ni eneo la nyumbani alikozaliwa. Wauaji ni wenyeji wa Kibaha wanaofahamu vema jiografia ya Kibaha hasa eneo la Mitamba Pangani ambako hakuna doria za polisi, kuko kimya na mbali na makazi ya watu. Pia ni eneo lenye gate away nzuri kwahiyo ni rahisi kupoteza maboya mtu anayekufuatilia.

Unaweza kutokea Kimara
Unaweza kutokea Baobab
Unaweza kutokea Kibaha maili moja eneo la shell
Unaweza kutokea NIDA
Unaweza kutokea picha ya Ndege
Unaweza kutokea Loliondo nk na kote huko mtu asijue umetokea Mitamba Pangani

Kwa vyovyote mwenye mpango wake alikodi watu wa kumsaidia kuutimiza
  • Dereva
  • Mfuatiliaji aliyekuwa kanisani
  • Mtu aliyempatia sindano ya sumu
  • Backup
  • Hapa kuna watu wa kati hawakosekani
  • Malazi, kama watekeleza mpango walitoka mbali ni wazi walilala gesti za maeneo ya Kibaha ama jirani na Kibaha.
Loose ends/makosa ya kiutendaji yasiyotarajiwa
Wajuzi hufanya rehearsal hata zaidi ya mara tano kutegemeana na mlengwa na bajeti na kila rehearsal hugundua makosa kadhaa na kuyarekrbisha.

Je, makosa makubwa kwenye hili tukio ni yapi?

1. Mtandao wa mawasiliano simu na jumbe za sauti na maneno
2. Kuhusisha watu zaidi ya mmoja
3. Kutochagua wajuzi wa kazi
4. Kutofanya rehearsal
5. Kumchoma sindano ambayo haikuwa na sumu kali au ambayo haikuchomwa kwa usahihi
6. Kudhani amekwisha kufa hivyo kutengeneza fool proof ya kumchoma moto uliomzindua
7. Pengine kuondoka eneo la tukio haraka bila kuhakikisha ameungua vizuri
8. Macho kubaki salama, yalirekodi kila kitu

Kwa dondoo hizo hii kesi ni nyepesi kuliko ya bilionea Msuya ana yule mzungu wa tembo. Marehemu alibaki kuwa hai kuanzia tarehe 3 march mpaka 9 alipoaga dunia. Siku sita ni nyingi sana kuweza kupata na kujua mengi

Damu ya mtu ni nzito na inanuka! Harufu hukoma haki ikitendeka
Hakuna ulicho kiacha kama ni haki pasina konakona,wiki ni nyingi sana kupatikana hao watu.Ikumbukwe Huyo ni mhasibu ana kalia koneksheni nyingi za watu,lakini usije shangaa zikaja story za wivu wa mapenzi.
Ni maoni tuu
 
MPAKA WATU WANAIGIZA SAUTI YA BOYFRIEND NA KUMWITA NNJE YA KANISA AISEE YANGU MACHO KAMA ATASHIKWA MTU HAWA NI PROFESSIONAL KILLERS AMBAO HAWAJAWAHI SHUHUDIWA KATIKA NCHI YA TANZANIA TOKA UHURU
 
Huyo huyo aliiba mamilioni bank fulani nusu afungwe,mumeww ni mfogo wake na kavishe wa TBL wanaendesha landrover discovery,hao madada ni noma kwenye hela tusimtetee sana marehemu maana dada yake alichokifanya miaka iliyopita mmmm
Vyovyote vile, ule unyama aliofanyiwa hauvumiliki..

Hatutakiwi kupotezea vitendo kama hivi, lazima wahusika wasakwe na wachukuliwe hatua Kali.
 
Yaani uwe Afisa Mahusiano Airtel ulafu usipate Salary ya 4m?? Mkuu jaribu kuwa serious basi.. Na alitoka Airtel kwenda Barclays baada ya kupandiwa dau huko
Unataka nikwambie kuwa nimefanya nao kazi ndio uridhike
Nimedaka nao sana simu za call center chini ya CEO steve torode na manager Naimi,supervisor fred mwanry,
 
Back
Top Bottom