Loose ends Kifo cha Martha Towo

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,883
Familia iko kwenye msiba mzito. Tunawapa pole. Ni kifo kinachotokana na mauaji hivyo hakiwezi kukosa mijadala na msingi wa hiki kifo cha mauaji lazima kiwe na sababu, kiwe na viashiria.

Kiwe na mhusika/wahusika wakuu
Kiwe na bajeti
Kiwe na watendaji/watimiza lengo. Kwa msingi huu wauaji
Kiwe na mpango kazi
Kiwe na fool proof
Kusiwe na dosari kuanzia kupanga, kutekeleza na hatimaye kutawanyika na kumalizana kama kuna malipo ya mwisho yalikuwa bado

Uchunguzi wa kifo hiki ni rahisi sana na si chini ya watu 20 wanaweza kuhusishwa nacho, ambapo watachujwa mpaka watabaki si chini ya watano .. Na ni uchunguzi rahisi kutokana na makosa mengi waliyofanya wauaji.. Hawakuwa wajuzi maana wajuzi huwa hawaachi alama! Japo kuna kosa moja dogo sana hufanya na kufumua mpango wote.

Uchunguzi wake utaanzia kazini kwake, maisha yake nje ya kazi, marafiki zake, wateja wake, mishe na dili zake, mawasiliano yake pamoja na mahusiano.. Hapa ni kwa ajili ya ku 'establish' Msingi wa kesi na 'motive' ya muuaji/wauaji.

Uchunguzi wa pili ni eneo lilikofanyika tukio.. Pori la Mitamba linalosifika kwa matukio ya mauaji, Mitamba halina tofauti sana na Mabwepande na kama linaweza kuchunguzwa vizuri kuna maiti ngingi mule zinaweza kuwa zimezikwa.

Mitamba liko Kibaha njia ya kwenda Bagamoyo eneo linaitwa Pangani.. Sehemu kubwa ya pori la Mitamba ni eneo la wizara ya mifugo na uvuvi na kuna kipindi matapeli wa viwanja Kibaha walilivamia na kuwauzia watu viwanja mpaka serikali ikaingilia kati.

Marehemu ni mkazi mwenyeji wa Kibaha Kwambonde kakulia hapo, kosoma Tumbi nknk. Wazazi wake wanaishi hapo mpaka sasa na ni watu unaoweza kuwaita maarufu eneo hilo na hata kanisani kwao Tumbi. Kwanini muuaji/wauaji wakachagua kuja kummaliza 'nyumbani kwao'?

Marehemu alisafiri salama salimini toka kituo chake cha kazi Shinyanga mpaka nyumbani Kwambonde Kibaha. Pengine alitumia ndege, usafiri binafsi au wa jumuiya lakini alifika salama.

Je, wauaji walikuwa wanamfuatilia kote huko?
Je, wauaji ndio walimuita aje Kibaha?
Je, lengo lake la kuja nyumbani Kibaha lilikuwa ninini?
Je, mpango wa kummaliza Kibaha pori la Mitamba ulikuwa mpango plan A au B?

Marehemu siku ya tukio alikuwa kanisani na ndugu zake.. Ni wazi alipata wito wa kuitwa nje mara moja ama kwa ishara ya mtu alikuwa ndani ya kanisa ama kwa simu kwakuwa mikoba yake aliacha alipokuwa kaketi. Hakurudi!

Ni wazi walimuita walikuwa nje kabisa ya kanisa barabarani! Kanisa la KKKT Tumbi liko pembezoni mwa barabara ya kuelekea Tumbi hospital. Ni wazi kulikuwa na gari ambalo ama alipanda kwa hiari ama kwa lazima/Kutekwa.

Ni wazi safari ilianza kuelekea Pangani pori la Mitamba.. Macho ya marehemu yata 'reveal' kilichotokea ndani ya gari kwa hicho kipindi chote mpaka kufika Mitamba kumwagiwa Petrol na kuchomwa moto!



Ukurasa wa pili juu ya mpango kazi ambao ninaamini ndio plan A.

Wauaji waliona eneo salama la kummaliza ni eneo la nyumbani alikozaliwa. Wauaji ni wenyeji wa Kibaha wanaofahamu vema jiografia ya Kibaha hasa eneo la Mitamba Pangani ambako hakuna doria za polisi, kuko kimya na mbali na makazi ya watu. Pia ni eneo lenye gate away nzuri kwahiyo ni rahisi kupoteza maboya mtu anayekufuatilia.

Unaweza kutokea Kimara
Unaweza kutokea Baobab
Unaweza kutokea Kibaha maili moja eneo la shell
Unaweza kutokea NIDA
Unaweza kutokea picha ya Ndege
Unaweza kutokea Loliondo nk na kote huko mtu asijue umetokea Mitamba Pangani

Kwa vyovyote mwenye mpango wake alikodi watu wa kumsaidia kuutimiza
  • Dereva
  • Mfuatiliaji aliyekuwa kanisani
  • Mtu aliyempatia sindano ya sumu
  • Backup
  • Hapa kuna watu wa kati hawakosekani
  • Malazi, kama watekeleza mpango walitoka mbali ni wazi walilala gesti za maeneo ya Kibaha ama jirani na Kibaha.
Loose ends/makosa ya kiutendaji yasiyotarajiwa
Wajuzi hufanya rehearsal hata zaidi ya mara tano kutegemeana na mlengwa na bajeti na kila rehearsal hugundua makosa kadhaa na kuyarekrbisha.

Je, makosa makubwa kwenye hili tukio ni yapi?

1. Mtandao wa mawasiliano simu na jumbe za sauti na maneno
2. Kuhusisha watu zaidi ya mmoja
3. Kutochagua wajuzi wa kazi
4. Kutofanya rehearsal
5. Kumchoma sindano ambayo haikuwa na sumu kali au ambayo haikuchomwa kwa usahihi
6. Kudhani amekwisha kufa hivyo kutengeneza fool proof ya kumchoma moto uliomzindua
7. Pengine kuondoka eneo la tukio haraka bila kuhakikisha ameungua vizuri
8. Macho kubaki salama, yalirekodi kila kitu

Kwa dondoo hizo hii kesi ni nyepesi kuliko ya bilionea Msuya ana yule mzungu wa tembo. Marehemu alibaki kuwa hai kuanzia tarehe 3 march mpaka 9 alipoaga dunia. Siku sita ni nyingi sana kuweza kupata na kujua mengi

Damu ya mtu ni nzito na inanuka! Harufu hukoma haki ikitendeka
 
Usicheze na kahama na kahama kuna matajiri alafu wenye roho za ajabu? Pili, huyu dada alikuwa mapepe? Tatu, kabla ya kwenda kibaha alifukuzwa kwa sababu za kiofisi ijulikani ni utovu au mengine kiofisi. Nne hakuwa na cheo hiko ni Afisa mikopo.

Tano, matukio ya kahama kesi za kufanyiana unyama zipo sana sio mapenzi, sio biashara na n.k. Uzuri wa huyu dada inaonyesha alikimbia kuofia vitisho kwa mwanamke mwenzake au mapenzi?
 
Nipo nje ya mada nisamehewe!

Jamiiforums sijui wamebadili nini tena kwa tunaotumia browser imezidi kuchukiza,nipo nasoma main post mtu ana-reply uzi inanipeleka kwenye new post wakati sijamaliza hata kujua maudhui ya mleta mada.

Hiyo namna ya ku-like sasa,wameweka vijiboksi boksi mtu hata hujui ufanyeje bora ile ya emoj kuliko hii.
 
Ukurasa wa pili
Juu ya mpango kazi ambao ninaamini ndio plan A
Wauaji waliona eneo salama la kummaliza ni eneo la nyumbani alikozaliwa
Wauaji ni wenyeji wa Kibaha wanaofahamu vema jiografia ya Kibaha hasa eneo la Mitamba Pangani ambako
hakuna doria za polisi, kuko kimya na mbali na makazi ya watu
Pia ni eneo lenye gate away nzuri kwahiyo ni rahisi kupoteza maboya mtu anayekufuatilia
Unaweza kutokea Kimara
Unaweza kutokea Baobab
Unaweza kutokea Kibaha maili moja eneo la shell
Unaweza kutokea NIDA
Unaweza kutokea picha ya Ndege
Unaweza kutokea Loliondo nk na kote huko mtu asijue umetokea Mitamba pangani

Kwa vyovyote mwenye mpango wake alikodi watu wa kumsaidia kuutimiza
Dereva
Mfuatiliaji aliyekuwa kanisani
Mtu aliyempatia sindano ya sumu
Backup
Hapa kuna watu wa kati hawakosekani
Malazi, kama watekeleza mpango walitoka mbali ni wazi walilala gesti za maeneo ya Kibaha ama jirani na Kibaha..

Loose ends/makosa ya kiutendaji yasiyorarajiwa
Wajuzi hufanya rehearsal hata zaidi ya mara tano kutegemeana na mlengwa na bajeti na kila rehearsal hugundua makosa kadhaa na kuyarekrbisha..

Je makosa makubwa kwenye hili tukio ni yapi?
1. Mtandao wa mawasiliano simu na jumbe za sauti na maneno
2. Kuhusisha watu zaidi ya mmoja
3. Kutochagua wajuzi wa kazi
4.kutofanya rehearsal
5. Kumchoma sindano ambayo haikuwa na sumu kali au ambayo haikuchomwa kwa usahihi
6. Kudhani amekwisha kufa hivyo kutengeneza fool proof ya kumchoma moto uliomzindua
7. Pengine kuondoka eneo la tukio haraka bila kuhakikisha ameungua vizuri
8. Macho kubaki salama, yalirekodi kila kitu

Kwa dondoo hizo hii kesi ni nyepesi kuliko ya bilionea Msuya ana yule mzungu wa tembo

Marehemu alibaki kuwa hai kuanzia tarehe 3 march mpaka 9 alipoaga dunia.. Siku sita ni nyingi sana kuweza kupata na kujua mengi

Damu ya mtu ni nzito na inanuka! Harufu hukoma haki ikitendeka..
 
Back
Top Bottom