FROM WADAU MUINE UZITO WA HII KESI
Ni hivi;
1. Kuna tetesi zinasema alikuwa amtambulishe mchumba wake kesho yake tu
2. Alivyokuwa kanisani alipigiwa simu na kwa jinsi Mzee alivyoongea ni kama hao watu wabaya waliiga sauti ya boyfriend wake.
3. Alivyotoka kwenda kuitikia wito wa aliyedhani ni boyfriend wake, ndio akatokomea mazima.
4. Martha alikuwa na fahamu mpaka akataja namba za baba yake, so yawezekana pia kabla hajapoteza fahamu kabisa alitoa abc kwa familia ndio maana Mzee anaongea kwa confidence kabisa
5. Wauaji ni watu smart sana, walijua kanisani kuna CCTV so wao walikaa nje mbali kabisa ili hiyo CCTV isiwaone wala kuona usafiri wao.
6. Martha aliachishwa kazi mwezi mmoja nyuma, yawezekana kulikuwa na uchunguzi unaendelea na Martha angeweza kuwa mtoa ushahidi muhimu kwahiyo.
7. Kwa Scenario ya mauaji haya, hii ni dhahiri sio wivu wa mapenzi ila ni mambo ya kazi. Wauaji ni Professional killers na lazima wamekodiwa na watu wenye mpunga mrefu kuficha traces zozote za ushahidi.
8. Branch Manager na staffs wa BOA Kahama kazi mnayo
Mkuu, umeshasema hapo kwamba "presumably"...that means inawezekana polisi walizungumza naye au hawakuzungumza naye. Lakini pia, zingatia kwamba ukiwa hai tena ICU haimaanishi kwamba ni lazima uweze kuzungumza, pengine alikuwa anapumua tu lakini hoi bin taaban.
Aidha, hata kama aliweza kuzungumza, ushahidi wa huyu mgonjwa hauwezi kuaminiwa kama ulivyo kwa kuzingatia hali yake. Lazima ushahidi huu uhusianishwe na ushahidi mwingine ili kuupa nguvu.
Sheria ni sayansi. Shahidi namba moja akishakufa huwa kuna mambo mengi ambayo yanafifisha uzito wa ushahidi wa watu wengine.
In criminal litigations the standard of proof is BEYOND REASONABLE DOUBTS. Ishu inakuja hapo kwenye kuthibitisha bila kuacha shaka. Ndiyo maana watuhumiwa wengi wa makesi ya namna hii huwa wanaachiliwa huru hata kama ni kweli wametenda kosa.
"walimchoma moto akiwa hai na kumuacha afanikiwe kutoroka ili aweze kuongea maneno yatakayopelekea upeleleza kuhama mbali kabisa na sababu ya tukio hilo"
Unaweza kuelezea kidogo hapa mkuu. Kitu gani kingelisababisha aongee maneno yanayoweza kuondoa ushahidi wa tukio baada ya kufanikiwa kupona kifo?
Kuna uwezekano wauaji walimfuatilia mienendo yake na kumfahamu na kum mark vya kutosha.
Inawezekana, baada ya kumteka wakawa wanampiga biti kwamba siku nyingine iwe fundisho kwa wanaopenda kuingilia either mahusiano ya watu au mambo yasiyomhusu kitu ambacho kinakuwa rahisi kwa marehemu ku connect dots na kujua watu hawa watakua ni akina fulani au wametumwa na fulani (hapo wauaji wanazidi kujijengea kinga ya jata kuhisiwa)
Kitu ambacho kitapelekea vyombo vya uchunguzi vilivyomhoji kuelekeza nguvu zao ambako maelezo ya marehem yameelekeza.
Wakati kiuhalisia kifo cha marehemu kitakua kinahusiana na tukio la yofauti kabisa na maelezo ya marehemu.
Cha kufanya, wajaribu kufanya tracking katika biashara za marehemu tangu akiwa Babati hadi alipohamia Kahama.
Waangalie manunuzi aliyowahi kuyafanya na malipo yake yalikuaje.
Waangalie mazingira ya kuacha kazi yalikuwaje, na mahusiano aliyokua nayo na wateja wa bank kote alipowahi kufanyia kazi.
Waangalie mahusiano na wafanyakazi wenzake, hasa wale wafanya kazi wenzake ambao ni 'Partners in Crime' ambao huku uswahili huwa tunapenda kuwaita 'Pika pakua'. Lazima kuna issue ya mgao iwe inahusika hapo.
Nina uhakika mpaka sasa wana taarifa za kutosha kuhusiana na jinsi alivyoondoka kanisani.
Pale Kahama lazima kutakua na eneo pendwa ambalo marehemu alikua akipenda kutembelea akiwa na watu fulani, ni muhimu sana kuipitia nayo.