Tangu mzunguko wa pili wa msimu uliopita, Sadio ndio amekuwa moyo wa ushindi wa Liverpool hata km hatofunga goli kwenye mechi.
Na hadi sasa, mchango wa Sadio ni mkubwa zaidi ya yeyote kwenye ile front three yetu.
Salah amepoteza target kidogo, na ndio maana kiwango Cha ufungaji wake kimepungua. Si ajabu kuona anakosa magoli ambayo alikuwa anafunga msimu wa kwanza alipofika lfc.
Bobby amepoteza target pia, licha ya kuaminiwa na Jurgen, lkn ukweli utabaki kujadiliwa, amepoteza target.
Kitu pekee kinachomfanya aendelee kuanza ni namna anavyoweza kufany organisation ya mashambulizi na kuwasaidia wenzake wafunge, basi.
Diogo anaonekana mwenye kismati na nia ya ku-shine haswa. Na hapa ndipo anapoumiza vichwa vyetu kujadili hili.
Binafsi namuona Diogo km Louis, ana usongo wa goli, ari ya kufanikiwa na kuwa mchezaji mahiri zaidi.
Kwa mchezaji wa namna hii, huwezi kumuanzisha bench afu umuanzishe Bobby, haiwezekani.
Uzuri ni kuwa Diogo anaweza kucheza 9 na 7 tena kwa kiwango cha kufanana, na hapa ndipo Salah anaonekana kuja kufunikwa
Pamoja na hayo, hawa wote wanahitajika lfc, lazima tuwe na kikosi kitachoweza kupindua matokeo muda wowote ikiwa walioanza wameshindwa, na hapo ndipo tutapotawala soka la epl na uefa.