Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Siku mtakuja kuamini slot ni tapeli itakuwa too late... huwezi tumia £500m window moja alafu timu haijui inataka nini uwanjani ..... mmesajili injury prone (isak) tuliwaambia huyu hawez kuwapa mechi kumi consecutively, frimpong average player, kerkez kuvaa tu jezi yenu ni matusi...hana levo hio... writz Epl inamshinda miguu inatetemeka.... Bora Hugho walau ........Virgil na Salah maji ya jiooni.... safi sana
Euro M 500 mbona ndgo hio, nyie Man city na Chelsea mnaotumia mpaka Euro billion 2 Kwa msimu mmoja wa usajili na ht kudanganya baadhi mahesabu muwekwe kundi gani
 
LIVERPOOL IN THE UCL THIS SEASON
IMG-20260129-WA0073.jpg

Udhibiti wa Mechi (Control): Tofauti na "Heavy Metal Football" ya Klopp iliyokuwa na chaos nyingi, Liverpool ya Slot inacheza kwa utulivu zaidi. Takwimu za pasi (89% passing accuracy) na umiliki (52.88%) zinaonyesha timu inayotafuta kutawala mchezo kupitia muundo (structure) badala ya mbio pekee.
 
IMG-20260129-WA0072.jpg

Liverpool imefunga mabao 20 katika mechi 8 (wastani wa mabao 2.5 kwa kila mechi). Ushindi mnono wa 6-0 dhidi ya Qarabağ na 5-1 dhidi ya Frankfurt unaonyesha kuwa timu bado ina makali mbele ya lango.

Takwimu zinaonyesha Liverpool imekuwa hatari zaidi ugenini, ikifunga wastani wa mabao 2.3 na kuruhusu mabao 0.5 pekee, jambo linaloashiria mbinu bora za "counter-pressing" na nidhamu ya kuzuia wanapokuwa nje ya dimba la Anfield.
 
Defensive Vulnerability Liverpool imeruhusu wastani wa mabao 2.0 ikiwa nyumbani Anfield kwenye UCL. Kipigo cha 4-1 kutoka kwa PSV nyumbani ni ishara ya wazi kuwa mfumo wa Slot wa kupandisha mabeki (Inverted Full-backs) wakati mwingine unaacha mianya mikubwa inayotumiwa na timu zinazoshambulia kwa kasi.

Kukabiliana na Mbinu za "High Press": Takwimu za recoveries na tackles zinaonyesha kuwa timu inapata shida inapokutana na wapinzani wanaobana kwa nguvu (high pressing). Kupoteza kwa 1-0 dhidi ya Galatasaray na shida dhidi ya PSV kulionyesha udhaifu katika kujenga mashambulizi kuanzia nyuma (build-up under pressure).

Mbinu za Slot zimetoa ishara ya "Evolution" (Mageuzi) badala ya Mapinduzi:

Muundo wa 4-2-3-1/4-2-4: Slot anatumia viungo wawili wakabaji (double pivot) kama Gravenberch na Mac Allister kutoa ulinzi zaidi, huku akimruhusu mchezaji kama Florian Wirtz au Szoboszlai kucheza kama namba 10.

Mabeki wa Pembeni (Inverted Full-backs): Tofauti na Trent aliyezoeleka kupiga krosi, sasa mabeki wanazama zaidi katikati ya uwanja kutengeneza "numerical superiority" (idadi kubwa ya wachezaji katikati), hali inayosaidia kumiliki mpira.

Slot ameleta aina ya washambuliaji wanaoweza kushiriki kwenye mchezo (link-up play), tofauti na mshambuliaji wa kukaa tu ndani ya box.

Mwelekeo wa timu ni mzuri, Slot anahitaji kurekebisha nidhamu ya ulinzi akiwa Anfield na kuhakikisha kuwa "Controlled Possession" yake haipotezi makali ya kasi (verticality) yaliyoijenga Liverpool kwa miaka mingi.

Ynwa
 
Kikosi cha Liverpool kilichobeba ubingwa chini ya Arne Slot ni kikosi kilichojengwa na Jürgen Klopp.

Hili halina mjadala.
Wachezaji wakuu ni walewale:

Alisson
Van Dijk
Trent Alexander-Arnold
Andy Robertson
Mohamed Salah
Konaté
Mac Allister
Szoboszlai
Darwin Núñez, n.k.
Pia:
  • Mtindo wa kucheza kwa nguvu (intensity)
  • Pressing ya juu
  • Akili ya kushinda (winning mentality)
Vyote hivi ni urithi wa Klopp.
Slot hakujenga timu upya.
Alirithi timu ambayo tayari ilikuwa imekomaa na iko karibu na kilele cha ubora wake (peak cycle).

Kwa nini Liverpool ya Klopp haikubeba ubingwa msimu wa 2023–24?

Sio kwa sababu timu ilikuwa mbovu, bali kuna mchanganyiko wa sababu kadhaa.

(a) Muda haukuwa sahihi (Timing & Team Cycle)

Liverpool ilikuwa imetoka kwenye rebuild kubwa:
Henderson aliondoka
  • Fabinho aliondoka
  • Milner aliondoka
  • Keïta aliondoka
Viungo wapya:
  • Mac Allister
  • Szoboszlai
  • Endo
  • Gravenberch
Walikuwa bado wanaizoea EPL.

Kwa lugha rahisi:
Msimu wa 2023–24 ulikuwa msimu wa mpito wa mwisho, sio msimu wa kilele.

(b) Uchovu wa akili kwa Klopp (Mental fatigue)
Hili watu wengi hawapendi kulisema, lakini ni la kweli.
Klopp alikuwa Liverpool kwa miaka 9: Alikuwa ni
  • Kocha
  • Kiongozi
  • Mhamasishaji
  • Kinga dhidi ya presha ya media
  • Mjenga utamaduni wa klabu
Msimu wa 2023–24:
Alitangaza mapema ataondoka
  • Kila mechi ikawa ya kihisia sana
  • Maamuzi yakawa ya tahadhari zaidi
Huu haukuwa udhaifu, bali ni uchovu wa kawaida wa binadamu.

(c) Majeruhi na mabadiliko ya wachezaji
  • Matip alikuwa nje
  • Thiago karibu msimu mzima nje
  • Jota na Konaté walikosa vipindi muhimu
  • Trent alikosa mechi muhimu
Matokeo:

Klopp alilazimika kubadilisha wachezaji mara kwa mara
Mac Allister alichezwa kama DM muda mrefu
Hii iliathiri mwendelezo wa matokeo, sio ubora wa timu.

(d) Tofauti ndogo sana (Fine margins)

Liverpool haikushindwa vibaya.

* Ilipoteza ubingwa kwa:
Droo chache
  • Mechi chache zilizopotea kwa tofauti ndogo
  • Maamuzi ya VAR (mfano Spurs ugenini)
Kwa nini walibeba ubingwa chini ya Slot?
Sio kwa sababu Slot ni bora kuliko Klopp,
bali kwa sababu mazingira yalikuwa tayari yamekaa sawa.

(a) Slot alipata timu iliyoiva
Midfield ilikuwa tayari imezoea EPL
Núñez, Díaz, Gakpo walikuwa wamekomaa
Quansah na Bradley walishapata uzoefu wa presha

Slot:
Hakujenga msingi aliukuta na kuutumia.
(b) Mabadiliko madogo ya mbinu
Slot alifanya marekebisho madogo:
  • Akapunguza presha kidogo
  • Akaongeza nidhamu ya nafasi
  • Akapunguza chaos zisizo za lazima
Hii ilisaidia:
  • Kushinda mechi mapema
  • Kuepuka droo zisizo muhimu
Lakini:
Msingi wa pressing wa Klopp bado ulikuwepo.

Ukweli ambao mashabiki wengi hawaukubali
Kama Klopp angeendelea msimu wa 2024–25,
kuna uwezekano mkubwa angechukua ubingwa pia.
Kwa nini?

Kikosi ni kilekile
  • Wachezaji walikuwa wamekomaa
  • Rebuild ilikuwa imekamilika
Tofauti ni :
Klopp angechukua ubingwa kama mbunifu wa jengo👏

Slot ameuchukua kama mtumiaji wa jengo lililokamilika😊
Kwa hiyo:

Klopp hakufeli
Slot hakufanya miujiza
Mafanikio ya Slot ni matokeo ya kazi ya Klopp + muda sahihi
Kwa nini Liverpool inasuasua licha ya kutumia £450m?

Kutumia pesa nyingi hakumaanishi timu itacheza vizuri mara moja.

(a) Pesa hazinunui mshikamano

* £450m zimeleta:
Wachezaji wengi wapya wenye mitindo tofauti ya uchezaji

Lakini:
  • Kuelewana hakuuzwi kwa pesa
  • Kunahitaji muda wa kuzoeana
Kama Klopp alivyosema:
“Football is not a PlayStation.

(b) Timu iko kati ya falsafa mbili
Klopp aliacha:
  • Gegenpressing
  • Kushambulia haraka
  • Chaos zilizo na mpangilio
Slot anataka:
  • Udhibiti wa mechi
  • Nidhamu ya nafasi
  • Kupunguza hatari
Matokeo:
Timu iko katikati

Haichezi kama Klopp wala haichezi kama Slot kikamilifu

Ndipo kunapotokea:
Kusuasua
  • Droo zisizoeleweka
  • Kukosa ukatili wa kumaliza mechi
(c) Wachezaji wanafikiri sana
Klopp:
“Ukiona nafasi, shambulia haraka”

Slot:
“Subiri mpangilio ukae sawa

Hii husababisha:
  • Kusita kwa sekunde chache
  • Kupoteza kasi
  • Mashambulizi kufa kabla hayajaanza
(d) Presha ya bei kubwa
Mchezaji wa £80–90m:
  • Hucheza kwa woga
  • Hufikiria media na mashabiki
Matokeo:
  • Kucheza kwa tahadhari
  • Kukosa hatari
  • Kucheza ili asikose badala ya kushinda
Data inaonyesha tatizo sio ubora, bali matumizi
  • Nafasi zinapatikana
  • Mpira unamilikiwa
  • Udhibiti wa mechi upo
Lakini:
  • Mabao hayapatikani
  • Nafasi muhimu hazitumiki
  • Mechi zinaishia droo
Hii inaonyesha:
Timu inafikiria sana badala ya kucheza kwa mazoea.
 
Kocha Slot sijui hata huko mazoezini anafundisha nn?
Liverpool iliyokua ina high pressing imeenda wapi?
Klopp alikua kocha jamani
 
Fanboys wa Arsenal msimu uliopita walisema tulibeba ubingwa kwasababu Timu nyengine zilikuwa mbovu.

Je, msimu huu wanasemaje? Wanahisi wanaongoza ligi kwasababu Timu nyengine ni mbovu?

Nadhani wameshajifunza kitu kuwa ni hali ya kawaida kubeba ubingwa pale wengine wanapokuwa hawapo vizuri hata kwa Leicester City kubeba ubingwa ilitokea hivyo.
 
Kocha Slot sijui hata huko mazoezini anafundisha nn?
Liverpool iliyokua ina high pressing imeenda wapi?
Klopp alikua kocha jamani
Virgil Van Dijk on Arne Slot getting Criticism: "Who gives him the disrespect? That's the question,"

"Is the disrespect being given by people that we shouldn't value their disrespect?”

"I can also think about players being disrespected, and who disrespects the players? Is that someone you value, is it a significant show of disrespect or someone you can just let slide and instead just focus on the task ahead to be successful as a Liverpool player?
 
Mashabiki mmetawanyika 😅 ama kweli
Anyways, mnatakiwa kufungwa angalu 2 ili muwape false sense City kwamba they can fight for the title. I want tge disappointment to be bigger and stronger
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom