Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Ni mzuri lakini kwenye suala la kuitendea haki namba 8 mhm hapana bado kabisa
šŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£šŸ˜€šŸ˜€Anaitendea haki hio namba vs Kieta....haha maana Ile jezi hua kwetu inatukumbusha home boy Gerrard na magoli yake amazing... sczbo hayo hana lakini always ndio akiwa na siku nzuri anafanya dirty work for Slot kimya kimya kuharibu rhythm ya opponent.

YNWA
 
🚨 | Kwa mujibu wa taarifa, Chelsea imepanga kuifata Liverpool kuidai kiasi cha pesa kwa kumchukua bure nyota kinda Rio Ngumoha ambaye usiku wa Jumatatu alifunga goli la ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Newcastle.

Taarifa inasema kwa kuwa nyota huyo hakuwa na mkataba wa mchezaji wa kulipwa sababu hakuwa amefikisha umri wa kupewa mkataba huo lakini baadae akajiunga na Liverpool na kuiacha Chelsea ikiwa imehuzunishwa na kuondoka kwake kwa kuwa tayari alishaanza kufanya mazoezi na timu ya wakubwa, Chelsea inaona kuna haki inaweza kupata kwa kulipwa walau pesa kidogo kwa kumkuza nyota huyo.

Dau la paundi milioni 4 linatajwa linaweza kutumika kulipwa Chelsea
Kumekucha. Lile goli lake moja vs Magpies is worth hio pesašŸ¤£šŸ¤“šŸ¤“...

YNWA
 
Ishu za majeruhi na dharura zipo kote Cha msingi ni consistency ya matokeo safi pointi 3..... Kimsingi hata nyie mkitazama hii misimu mitatu iliyopita hamjaamini kukosa ubingwa hata mara 1 ni dalili kwamba bado mna mapungufu na hili dirisha mmefanya biashara mapema na bado mko sokoni kuweka mambo sawa ili EPL itue Emirates .....
Tukumbushane Mei 2026 nani atacheka mwisho

YNWA
Majeruhi yapo kote, sawa, lakini ukumbuke tumeshindana na City iliyokuwa bora paka bench wakati sisi tukiwa na kikosi finyu, yaani akiumia Saka au Saliba timu inayumba, Kwa sasa tupo imara paka benchi, ndio maana tunajiamini.
 
šŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£šŸ˜€šŸ˜€Anaitendea haki hio namba vs Kieta....haha maana Ile jezi hua kwetu inatukumbusha home boy Gerrard na magoli yake amazing... sczbo hayo hana lakini always ndio akiwa na siku nzuri anafanya dirty work for Slot kimya kimya kuharibu rhythm ya opponent.

YNWA
kama ni vs Keita nakubaliana na wewe
 
Majeruhi yapo kote, sawa, lakini ukumbuke tumeshindana na City iliyokuwa bora paka bench wakati sisi tukiwa na kikosi finyu, yaani akiumia Saka au Saliba timu inayumba, Kwa sasa tupo imara paka benchi, ndio maana tunajiamini.
Upo sahihi. Manchester city ametutesa kwa kua ba depth ya kikosi chake lakini bado nae last season akafanye mistake ya kuuza kuacha baadhi ya wachezaji bila kumtazama vyema yajayo na mwishowe nae akala za uso na Liverpool haoooo wakasepa na ubingwa... Mashindano ni mengi sana aisee kuna Carabao, FA, UCL na mechi za Kimataifa hivyo kikosi kikiwa pungufu Ubingwa haiji aisee.

YNWA
 
Draw system – league phase

16.01

A draw, which may be conducted digitally, determines the pairings for the league phase. The 36 clubs are divided into four pots of nine clubs. The pots are composed according to the club coefficient rankings established at the beginning of the season (see Annex D) and with the UEFA Champions League titleholder being the top seed in pot 1.

16.02

The opponents of each team, as well as whether each match is played at home or away, are determined by means of a draw. Each team is drawn against two opponents from each of the four pots and plays one opponent from each pot at home, and the other away. In principle, teams from the same association cannot be drawn against each other and each team may play against a maximum of two opponents from any other one association, subject to Paragraph 16.03

16.03

The UEFA administration may determine alternative conditions for the draw in accordance with the principles set by the Club Competitions Committee and may adapt any of the conditions of the draw to avoid deadlock situations and/or take into account any relevant constraints in light of decisions taken by the UEFA Executive Committee.
 
1756376174943.jpeg
 
Maoni ya Arne Slot kuhusu ratiba ngumu na yenye msisimkoā€ ya Liverpool katika Ligi ya Mabingwa baada ya droo ya hatua ya makundi kufanyika leo.

Liverpool waligundua wapinzani wao nane katika hatua ya kwanza ya mashindano rasmi wakati wa taratibu za UEFA huko Monaco Alhamisi mchana.

Hii itawaona mabingwa wa Premier League wakicheza nyumbani dhidi ya Real Madrid, Atletico Madrid, PSV Eindhoven na Qarabag kwenye dimba la Anfield, na kusafiri kucheza dhidi ya Internazionale, Eintracht Frankfurt, Marseille na Galatasaray.

Muda mfupi baada ya droo hiyo kufanyika,

Slot aliiaambia Liverpoolfc.com:

"Nafikiri jambo la kwanza kusema ni kwamba kama msimu uliopita, hii ni droo yenye changamoto kubwa, lakini tulijua itakuwa hivyo kwa sababu katika Ligi ya Mabingwa, hasa kwa mfumo mpya, hakuna droo rahisi.

"Lakini pia ni wazi kwamba hii ni droo yenye msisimko mkubwa, yenye mechi kubwa nyumbani na ugenini.

"Kuweza kuwakaribisha tena Real Madrid Anfield ni jambo la kipekee. Mechi ya msimu uliopita, bila shaka, ilikuwa ya kukumbukwa – na ninatarajia vivyo hivyo pia mara hii. Yaani, nina hakika hii ni mechi ambayo dunia nzima itaiangalia.

"Kuhusu upande wangu binafsi, daima ni vizuri kucheza dhidi ya timu ya Uholanzi PSV Eindhoven, timu iliyoshinda ubingwa wa ligi miaka miwili mfululizo. Vivyo hivyo kwa Galatasaray, ambao wamechukua mataji matatu mfululizo nchini Uturuki, na kwa Qarabag, mabingwa wa Azerbaijan.

"Na pia kucheza dhidi ya timu zenye viwango vya Inter Milan, Atletico Madrid, Eintracht Frankfurt na Marseille inaonyesha nguvu ya mashindano haya.

"Hakuna mechi yetu yoyote ya hatua ya makundi itakayokuwa rahisi, hilo ni wazi, lakini nina hakika mashabiki wetu watafurahia mechi zote za nyumbani Anfield na zote za ugenini, ambazo zote zitachezwa katika viwanja vikubwa na mashabiki wenye shauku na ari.

"Watashangilia na sisi pia. Tuna ratiba yenye shughuli nyingi mbele yetu, ndani ya nchi na Ulaya, lakini tuko tayari na tunashughulika na changamoto zinazokuja."

Tarehe za mechi na muda wa kuanza zitathibitishwa kwenye kwenye mtandao wa Liverpoolfc.com ifikapo Jumamosi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom