Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Umemalizia vizuri...
Screenshot_20250812-221142.jpg
 
Haya ni yale aina ya mambo ambayo waswahili wanasema 'yasikie kwa jirani' ila yakikukuta ni noma. Sisi Fabregas naye alileta haya mambo mpaka akatumia pesa zake mwenyewe. Barcelona kulimshinda mpaka hata kurudi England aliona aibu kurudi Arsenal na akaenda Chelsea. Uzuri ni story ya Fabregas iliisha vizuri kwake maana mafanikio aliyopata Chelsea, asingepata kwetu.
Bila shaka kwetu kuhusu Coutinho ilikua pigo maana dogo alikua moto sana lakini wachezaji wa Brazil na La Liga hua ni Pete na kidole hivyo mauzo yake ndio kwa sehemu kubwa yamechangia mafanikio yetu sasa kwani kipindi kile policy ilikua noma sana kwa Klopp bila kuuza alikua hapati wachezaji top quality....
Wale waarabu wa Newcastle hawajasoma huu mchezo wa kuuza na kununua vizuri hivyo wataelewa tu kwamba ni mwimba kumbakisha mchezaji asie na hamu ya kubaki alipo.

YNWA
 
Mimi kiukweli siyo mshabiki wa mabeki wafupi, kuanzia enzi za A.Moreno nilijifunza mengi mno.
Aafu kipindi hiki ukitazama ma beki wengi wa pembeni LB na RB sio warefu kama zamani, wanachoangalia ni Uwezo wao kushambulia sana kuliko kuzuia ambapo kwa msaada mkubwa hio kazi anafanya DM.
Mpira umebadilika sana.

YNWA
 
Aafu kipindi hiki ukitazama ma beki wengi wa pembeni LB na RB sio warefu kama zamani, wanachoangalia ni Uwezo wao kushambulia sana kuliko kuzuia ambapo kwa msaada mkubwa hio kazi anafanya DM.
Mpira umebadilika sana.

YNWA.

Mfumo huo utakusumbua ukikutana na mashambulizi ya kushtukiza.

Una- expose team na kuiweka kwenye hatari ya kufungwa magoli mengi... Reference..Aston villa 7 Liverpool 2 (sarr)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom