Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Hawa wanawake wanaanza kuharibu psychologia za wachezaji wetu muhimu. Hili limalaya Camila lazima limetumwa na Man U
 

Attachments

  • Screenshot_20250620_173441_Instagram.jpg
    Screenshot_20250620_173441_Instagram.jpg
    329.4 KB · Views: 8
Mbona Bournemouth wanabomoa backline yao yote??

🚨🔴🔵 Paris Saint-Germain keep advancing in talks to sign Ilya Zabarnyi after personal terms agreed last week.

Negotiations underway for fee close to €55/60m as L’Équipé reported; not a done deal yet as Bournemouth insist on their conditions.
 
Wazazi wa Florian Wirtz kupokea Euro Milioni 8.6 kwa kumwakilisha Kijana wao!

Katika tukio la kipekee na lisilo la kawaida kwenye soka la kimataifa, Wazazi wa Nyota wa Ujerumani Florian Wirtz wanatarajiwa kupokea Euro milioni 8.6 (takriban Tsh bilioni 25) kufuatia uhamisho wa mwana wao kwenda klabu ya Liverpool FC.

Kwa mujibu wa gazeti maarufu la Bild la nchini Ujerumani, wazazi hao walifanya kazi ya uwakala kwa niaba ya Mtoto wao katika dili hilo kubwa.

“Wazazi wa Florian Wirtz wataingiza Euro milioni 8.6 kutokana na uhamisho wake kwenda Liverpool, kwa kuwa ndio waliomwakilisha kama mawakala wake,” limeripoti Bild.

Ni jambo adimu sana kuona Wachezaji wa kiwango cha juu Duniani wakiwa na Wazazi wao kama Mawakala, hasa kwenye makubaliano ya fedha kubwa kama haya.

Wirtz alikuwa Mchezaji wa Bayer Leverkusen, na uhamisho wake kwenda Liverpool umevutia hisia nyingi kwa sababu ya staili yake ya kiuchezaji, uwezo wa kufunga na kutoa pasi za mwisho akiwa bado na umri mdogo.

Hatua ya Wazazi wake kuchukua jukumu la uwakala inafungua mjadala mpya kuhusu nafasi ya familia katika uamuzi wa taaluma za Wachezaji, hasa katika soka ya kisasa yenye nguvu ya kibiashara. Kwa familia ya Wirtz, hili si tu ni mafanikio ya Mwana wao, bali pia ni ushindi wa Wazazi kama Wawakilishi wa ndoto za Watoto wao.
 
Naongea kama shabiki wa mpira, Wirtz mchezaji wa kawaida sana. Hana utofauti na Mount
 
Livapuli haikukaa vizuri na wana Yanga shauri ya vazi lake. Kwa nini tusiwashauri hilo wajirekebishe? Yellow Devils imekaa vizuri, au?
 
pesa za wirtz zilitosha kusajili kikosi kizima cha AUCKLAND FC na kukilipa mshahara miezi kumi na mbili pamoja na bonus kwa kila mchezo
 
Mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Liverpool na Konate yamekwama, huku mchezaji huyo akitaka mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki ambao Liverpool wanauona kuwa mkubwa.

Iwapo makubaliano hayatafikiwa kabla ya mwisho wa majira ya joto, Liverpool wako tayari kumuuza Konate kwa kati ya euro milioni 50-60 ili asiondoke bure mkataba wake utakapokwisha mwaka 2026.

Klabu inahofia kukumbana na hali kama ile ya Trent Alexander-Arnold, ambaye walimpoteza bila fidia. Klabu kama Bayern Munich, Al-Hilal, Real Madrid, na Paris Saint-Germain pia zimeonyesha nia ya kumsajili Konate.

Liverpool inamtazama Konate kama mchezaji muhimu na wanatumai kumbakisha huku wakijaribu kufikia makubaliano juu ya mshahara wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom