Captain Marvelous
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 15,313
- 32,605
Huyu mzee anatutafutia nywele ziote mvi mapema hivi maana pale tu ubao unasoma MF Elliott Fabinho Jones unajua hapa leo ni kuhenyeshwa balaa....Hahaha Klopp bana cv yake kaichelewesha mwenyewe tu.
Hata tukiandika tutarudia yale yale tu. Tuendelee kujionea nini kinakuja.
Kuna dogo hua anabeti hapa kitaa wakati mwingine hua anaomba ushauri nikamwambia kama kweli Thiago hayupo na Klopp kaanza na ile MF basi Liverpool tunachapika akaniambia sio rahisi kwa vile tumetoka kumfunga Manchester City eti winning attitude imerejea basi bhana akakomaa na Liverpool leo nakutakana nae ananiambia Liverpool imemnyima laki 4... Nikamwambia Liverpool hii ya sasa sio ya kubetia haitabiriki na bila Thiago hatuna stability pale kati...
Kimsingi mtaani Liverpool sasa imekua adui kwa wazee wa ku beti maana hawaelewi lini atashinda lini atapigika yaaani kazi ipo.
Klopp kama Klopp anakomaa anavyojua yeye.
I admire Pep hua hana huruma ikija ishu ya out of form player nakumbuka kuna kipindi Mahrez alisugua benchi sana basi Pep akaulizwa vipi mbona huyu umenunua £60m aafu anasugua benchi akajibu kwamba yeye anaangalia mchezaji anavyojituma mazoezini na gemu ya mwisho ali offer nini uwanjani hapo ndio anajua kama huyo mchezaji anafaa kupangwa mechi ijayo na kweli dogo Mahrez alisugua benchi haswa mpaka pale Pep aliona kama amejiimarisha kua starter... Hii inakupa picha Pep ana utajiri wa talent za kutosha lakini pia anahitaji workhorse players sio bla bla... Huku Klopp kajaza quantity wanacheza wanavyotaka they care less kuhusu kupangwa kesho maana wanajua benchi haina ubora kabisa..
Tuna safari ndefu sana. Hii 4 4 2 ya Klopp inatoa some new hope lakini bila wachezaji sahihi kuitekeleza basi tutajikuta kila wakati tupo pale pale ni sare ama kipigo..
Mechi ya juzi tuseme ukweli bila ubora wa kipa Dean Henderson ilikua ushindi upo.. Wakati mwingine tulifanya maamuzi ya hovyo kama pale VVD badala afunge alitaka kutoa assist utaona namna gani confidence iko chini sana kwa baadhi ya hawa wachezaji...
So here we are...
.. Out of form
.. Low confidence
.. Injuries
.. Poor team selection
.. Aging squad tupo nafasi ya 3 bora kwa kua na kikosi kilicho sheheni wazeee.
We need a miracle.
YNWA



....