Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Kwanza stevie G pamoja na kuujua mpira alikuwa ana spirit ya kupambana, si mtu wa kukata tamaa, anajua kuibambania beji ya timu kama ni ya baba yake mzazi, akifungwa unaona huyu kafungwa..
Kwake machozi, jasho na damu, kuleta furaha kwa mashabiki.

Yes, Henry was the best, ila angekuwa na roho ya GERRARD angekuwa zaidi ya pale. Gerrard ni mchezaji ambae angecheza kwa kila mwalimu mzuri, si PEP si Wenger, si fergie, mourinho ndio kabisaa alishajaribu kumsaini, hata kwa EL CHOLO angepata nafasi ya kudumu, kwa KLOP ndio kabisaa.

Nikiwa na mchezaji aina ya GERRARD kwenye timu yangu naanza kumpanga yeye kabla ya golikipa
Liverpool ilikua Gerrard na Gerrard alikua Liverpool kimsingi tangu mwaka 2004 dogo alikua anaibeba hii timu kama mali yake, alicheza kwa kuchomwo sidano ili mradi awe uwanjani kuwaamshaamsha wachezaji wenzie na mashabiki kusaka ushindi...

Ndio maana hua nikisikia eti anafananishwa na akina Henderson hua nabakia kutoa macho kama fundi saa maana ni kama maji na oili hawa wachezaji ni tofauti kabisa...

Alikua nebo ya timu ndani na nje ya uwanja akiwakilisha vyema klabu yake pendwa.

Mourinho hakuficha kiu yake kutaka kufanya kazi na Steve akiwa Chelsea na baadae Los Blonco.

Maajabu sasa hawa ma beberu walivyoinunua timu na kuja na mikakati mpaka kumtema Steve huku akiuliza nyongeza ya mkataba kwa msimu mzima bila Rodgers kumpa jibu hakika ilikera sana alivyoodoka Steve lakini ndio maisha na sasa katupa kete yake kwenye ukocha ana safari ndefu lakini ndoto yake ni kutua Liverpool 1 day kama gaffer pengine mridhi wa Klopp.

YNWA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom