Tumeanza kuwa Mashabiki wa hovyo sana Aisee,(tumeanza kuwa kama Mashabiki wa Manyumbu),mara nyingi tumekuwa watu waelewa sana ila sasa hivi tumeanza kuwa Mashabiki wa hovyo kuwahikutokea kisa tu tumerudi tu kwenye ubora wetu, hapo ni dhahili kuwa watu wanachuki binafsi mechi moja tu eti tumepigwa?.
Me naimani na Nunez 100%, sasa hivi tumekuwa kama wehu vile Mashabiki wa Liverpool ,Nunez atawaprove wrong tu.
Salah kunakipindi alicheza mechi 7 bila kufunga lakini bado tulimpenda lakini sasa kwa Nunez washabiki hovyo wa Liverpool watakuja kumlaumu,navyojua mimi Mashabiki wa Liverpool hatuko hivyo.
Wapinzani nashangaa kama tumepigwa sisi kuhusu Nunez sijui kwanini wanaumia?maana sisi hatujajisifia kama Nunez noma sana,sisi tumekuwa kimya tu wao ndio wanaongeA.
Hizo kelele zao zisije kutufanya sisi kujiona tumekosea wala kujiona timu ya kawaida,sasa hivi wapinzani wanaumia sana tunavyopata matokeo.
Sasa hivi tumeanza kuchukiwa sana na Mashabiki wa timu zingine zote.
Adui yako mwombee njaa ndio hawa wapinzani wetu walivyo ndugu... Tangu atue Klopp tupo ki ushindani kinoma yaaani hata majeruhi yakiwa kama msimu wa 2020 2021 bado tulitoka salama Big 4 tena kwa goli la karne la Allison vs The Baggies...
Hivyo hapana hakuna jipya wanaobeza usajili wa Darwin mapema hivi ndio hao hao walimdiss Fabinho kipindi hajaanza kucheza na kukamata namba pale kati. Klopp hua hakurupuki kwenye usajili ndio ana ma flop wachache sana kwenye kununua tangu ahamie Liverpool sababu usajili wake ni backed by data department na back ground check ya nguvu sana juu ya mchezaji husika.. Aliwai sema humu
MosDef usajili wa Bissouma kuja Liverpool unaweza kukwama sababu dogo ana kashafa fulani fulani na ishu ambazo Klopp na Liverpool wanachukulia serious kwa ustawi wa klabu...
Ina maana kusajiliwa Liverpool kwa sababu tu ya talent haitoshi mbali na ukachero kuhusu tabia, attitude nk zinafanya package ya mchezaji kua kamili.. Zaidi anatazama mchezaji alie humble, anaejituma nk... Sasa sio kamba huku Nunez wamekurupika kisa tu Manchester United walimtaka au Real Madrid au Bayern Munich hapana ki ufupi dogo alikua profiled siku nyingi ilikua ni muda mwafaka sasa Klopp kuingia sokoni kumnasa ndio maana hata hamzungumzii kutofunga kwani anajua fika atakaaa sawa tu baada ya drills, mazoezi, kuelewa mfumo na majukumu yake kuu ni suala la muda tu huyu wengine watakataa maneno yao humu kwamba ilikua utani...
Kule Benfica walipenda kutumia sana 4 4 1 1 na kwa mafanikio makubwa sana waliweza kuwazima Ajax na Barcelona UCL na pia sisi pale Anfield walitupa changamoto sana japo tukitoka salama lakini tuliona namana walivyotuvuruga...
Sasa alivyosajiliwa Liverpool ni waumini wa 4 3 3 au 4 2 3 1 ambazo kule Benfica zilitumika nadra sana ni dhahiri hapo lazima apate sessions kadhaa aelewe vyema majukumu yake uwanjani na hilo nalo bado ni changamoto kwani dogo ana kingereza cha kuombea maji tu hivyo muda mwingi aidha Pep ama Thiago wanafanya kazi ya utafsri anachotakiwa na Klopp afanye..
Ki ufupi kama mnakumbuka pre season ya mwaka 2019 tulichezea vipigo na msimu ulivyoanza wa Ligi hatukupoa zaidi ya ushindi na mwisho wa Msimu haoooo ma bingwa wa EPL. Pre season ya 2019 July tulifungwo mechi 3,tukashinda mechi 3 na kutoa sare mechi 1 na hatukufungwo tena The Hornets walikuja kuvuruga spidi yetu ya kua immortal pale Uingereza... . Hivyo ukitazama matokeo ya pre season sio kwamba inakupa uhakika wa yajayo kwenye Ligi ndugu sio rahisi ki hivyo...
Kila mmoja na uhuru wa maoni kwa vile ni jukwaa huru hivyo tuwe na subira maana ligi ipo kama wiki kadhaa tu ianze...
Nina imani na Klopp...
Nina imani na wachezaji wake...
YNWA