LIVERPOOL IJIANDAE KWA CAOIMHIN KELLEHER.
Miongoni mwa matatizo makubwa kwa kila timu, ni pale unapokuwa na walinda milango wazuri wawili.
Hii iliisumbua Chelsea. Kwa sasa tatizo lilelile ndio linaenda kuikumba Liverpool sio muda mrefu...
Kitendo cha Kelleher kuwa #1 kwenye timu ya taifa lake, kunatishia zaidi maisha yake ya Liverpool kama #2 nyuma ya Alisson Becker. Kwa akili ya haraka haraka, sidhani kama Alisson atashuka kiwango mapema sana na huenda akawa kama Edwin van der Sar, Gigi Buffon, Jens Lehmann au hata David Seaman.
Pasua kichwa ni namna ya kudili na Kelleher ambae miaka miwili mbele ataanza kudai kucheza mara kwa mara na sio kuwa #2 tena..
Chelsea walifanikiwa kwa kumpeleka Thibaut Courtois Atletico Madrid kwa mkopo wa misimu miwili mpaka pale Petr Cech alipoonesha tayari ameshuka kiwango ndio wakamrudisha. Hapa waliweza kudili na tatizo hilo.
Imebaki kwa Liverpool kufikiria namna nzuri ya kuweza kubaki na Kelleher ambae wamemtengeneza wenyewe.. Katika kulitatua hili, jambo la msingi ni mchezaji mwenyewe kama atakubali kuendelea kukaa benchi [jambo gumu sana] au kutolewa kwa mkopo wa muda mrefu kwenye timu ya ushindani mkubwa ili kumjenga zaidi.
Nategemea maneno kumhusu Kelleher kuanza hivi punde na nimetazama kwa jicho la kitaalam jambo hili✍️✍️