Imagine Mane adi anaingia mwaka wa mwisho kwenye mkataba wake ila jamaa hata kuboresha mkataba hawakulifikilia kabisa uko nyuma😢😢..Tukachukua ligi lakin wapi hawakutaka kufanya lolote kwa uyu mweusi kisa mkimya 😢😢 daah.
Acha aondoke zake ila club haijamtendea haki Mane ata Klopp kamsaliti mane😠😠
Kisa ngozi nyeusi au kisa nini? eti wage structure!! serious guyz?
Na pundts kibao leo wanasema waondoke tu mbadala wapo kibao daah
Baada ya kutupa makombe yote kutupa furaha baada ya miaka 30 na bado hawajachoka na top 5 ya wachezaji bora duniani wapo leo wamekua hawana maana.
Ndio maana Diof alimuonya mane kuwa makini sana apo liver wewe kama ngozi nyeusi.
Mkuu hawa wachezaji sio ma Scouser kwamba wanaipenda ile badge nadhani pale kwa sasa Scouser ni Elliott, Jones na TAA hao japo ni professional lakini pia wana mapenzi sahihi na Liverpool. Ukiwachana laivu wana damu ya Liverpool. Hawa wengine Mkuu ni wafanya kazi kwao mapenzi ni mpunga mbele mapenzi baadae regardless ya sisi mashabiki tunasema aje ndio maana kila goli kila ushindi kila pointi wana ma bonus ya kutosha kwa sababu wapo kikazi zaidi sasa ikitokea kazi hio hio anafanya Liverpool anaweza kufanya kwingine na akalipwa powa zaidi itakua ujinga wake kutokwenda hivyo suala la Mane, Salah nk lipo wazi wanataka walipwe kama wenzao kwenye timu zingine bora wanavyolipwa. Hawa wachezaji wanawashauri safi sana wanajua kazi ya wachezaji uwanjani imekuza Liverpool ndani ya miaka 6 kwa zaidi ya asilimia 100 hivyo wao kudai kulipwa powa is backed by data. Its simple success uwanjani imeleta success ya kukua kwa brand maradufu sasa wao watumike kuvutia wawekezaji aafu walipwe peanut mh hio sio sawa.
Mane rohoo safi kama Bayern watamlipa powa na marupurupu ya kutosha na asepe tu huko dogo analisha kijiji na umri ndio ule ebu angalau kwa hii miaka yake mitatu nae afaidi utamu wa 300k+ kwa wiki ambao Liverpool hawawezi kumpa maaana kwa wage structure ya FSG ni ngumu mchezaji atoke 100k apae mpaka 300k yaaani sio kwa hawa ma Yankees hivyo Mane tumuache asepe roho safi.
Katuletea makombe 6 safiii kabisa EPL, UCL, Super Cup, World Club Cup, Carabao, FA.
Ukweli ni kwamba huu ubahili wa FSG unakwenda kutupasua maana tunahitaji upgrade ya Mane mchezaji atakaecheza kati maana tangu Diaz atue amekua akitumiwa Winga wa kushoto hivyo sasa tunahitaji CF mmoja flexible kutokana na mfumo lakini ambae anaweza ku track kwa press kama ambavyo hali inahitaji.
Tunahitaji pia replacement ya Origi na pengine Takumi kama akiamua kwenda kutafuta changamoto mpya maana dogo sio mchezaji wa benchi kama anavyotumika Liverpool too bad wanaomtangulia wanafanya vyema sana.
Tunahitaji replacement ya Ox maana kwa Klopp kutomtumia hii miezi ya mwisho wa ligi nadhani alihofu asije umia akashindwa kumuuza. Kwa Ox labda replacement yake ni Fabio ambae Klopp kashasema hatamtoa kwa mkopo atabakia kikosini.
Henderson, Thiago, Fabinho hapa ipo shinda ya consistency na ndio maana Klopp kaamua asajili DM flexible kumsaidia kazi Fabinho hii ni sawa kabisa maana kwa sasa ni Morton tu ndio anaweza kumsaidia Fabinho ukiachana na Henderson ambae pale analizimishwa sio namba yake.
Milner asepe zake Leeds payroll ipumie.
Neco na Phillips wauzwe mpunga uje angalau wote tupate £30m itasaidia sana kuboresha kikosi. Ox angalau tunaweza kupata £10m.
Nwa ngoja tuone ndio kwanza dirisha mambo yanasetiwa.
YNWA