Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Kwani Pep alimfanya nini huyu jamaa?
 
Kwani Pep alimfanya nini huyu jamaa?
Hahahaha bhana hawa tangu wapo Barcelona ni kama walikua na bifu lao alivyotua tena Pep pale Ethad mambo yakawa ndio mambya zaidi sasa Wakala wa Toure hua hana brake ya mdomo akawavuruga sana pale mpaka Kipara akasema Toure ni wa kuodoka matokeo yake sasa wakala wa Toure mwaka 2017 kama sikosei akasema wachawi wa Africa wamekasirika na wamempiga kipapai Pep asishinde tena Uefa kwa sababu ya kumdharau Toure.

YNWA
 
Chanzo Cha kumnyanyapaa ni nini?
Rangi,dini au ni nini?
 


Tetesi ni kwamba Klopp alimtazama huyu dogo kupitia clip za YouTube akavutiwa mpaka anawastua ma boss wake ikawa too late Rea Madrid washamnasa mapema.

YNWA
 
Chanzo Cha kumnyanyapaa ni nini?
Rangi,dini au ni nini?
According to Toure ishu ni kama vile Pep hakuwapenda wachezaji wenye asili ya ki Africa hivyo kumpelekea Toure kukwaruzana nae mpaka kufikia Ethad kutompa mkataba huku bado akiwa na kiwango kizuri tu.

Toure alisema shinda ilianzia pale Barcelona kwa Pep kuwatenga Eto, Deco, Toure, Gaucho nk na mwishowe wote waliodoka. Kingine ni kwamba kwa vile Pep hakua straika enzi za uchezaji wake hao wachezaji walikua wanamdharau kama vile hana cha kuwapa pale mbele hivyo wakawa wanapinga baadhi ya mbinu zake wazi wazi jambo ambalo kwa Pep haiwezekani zaidi ya kuuzwa tu na hao wote waliuzwa na Toure hapo aliuzwa shingo upande hakutaka kuodoka Barcelona hivyo aliodoka na kinyongo.
Mara pap Pep akatua Ethad akakuta Yaya ana influence kubwa sana na Pep ifahamike sio wale makocha design ya Klopp, Fergie nk ambao ni wazuri on one on one situation ku wa handle wachezaji to the letter. Pep yeye hua ni team work bila kuulizwa maswali na kufuata tactics zake na ikishidikana basi anauza huyo mchezaji ama kum bench yule ambae anaona anamchelewesha kufikia ubora. Pep haoni tatizo kuwaudhi wachache kwa kusaka makombe hilo amefanikiwa sana huku pia akikwaruzana na Eto, Zlatan, Toure, Aguero, Jesus, Deco nk

Pazuri mwaka jana Toure ameomba radhi kwa Pep na kwa Manchester City kwa kumuita mbaguzi na kuomba aonane na Pep lakini mpaka sasa Pep hajajibu wala hajaonyesha nia ya kuonana na Toure labda sasa baada ya kipigo cha Real Madrid atamsaka Toure wayamalize maana sioni akipata hio UCL πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…