Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Manure marahii watapigwa kwa Haaland.
Tetesi ni kwamba dogo anatua Manchester City... japo nao Barcelona walimtaka ishu sasa mpunga hawana.

Manchester United labda wapande dau kwa wakala maana tetesi ni kwamba yeye pekee hii dili anataka zaidi ya £1m kama negotiation fee.

YNWA
 
Milner abaki, Firmino auzwe.
 
Milner abaki, Firmino auzwe.
Aisee ngoja tuone mpaka Juni 2022 itajulikana wanaodoka na kubaki.

Milner kwangu aodoke tu maana kasi ya EPL kwa sasa inampa changamoto sana.

Firmino bado akiwa fiti anachakuleta uwanjani japo sio kama zamani lakini magoli yake msimu yamekuja gemu muhimu sana. Kingine dogo sio mlalamishi aidha akitokea benchi ama akiwa uwanjani hua yeye ni full smile.

YNWA
 
Keita na milner nao wabaki... milner kwa ajili ya dressing room nasikia Ni kiongoz hasa...keita ameanza kuonesha thaman yake..abaki aisee
 
Nampenda Bobby ila naona tumuachie, keita abaki hata kwa mkataba wa 2 yr, Gomez still anamuda wa kurudi kwenye kiwango chake, milner hata leo aondoke tunashukuru kwa kazi yake.
 
Nampenda Bobby ila naona tumuachie, keita abaki hata kwa mkataba wa 2 yr, Gomez still anamuda wa kurudi kwenye kiwango chake, milner hata leo aondoke tunashukuru kwa kazi yake.
Aisee Babu Milner kwa namna Klopp anavyokwenda nae atakuja kua staff pale Liverpool kama akisaini nyongeza mwaka mmoja tena akistaafu basi na ajira ni pale pale.

Kama kwa mfano akatua Darwin basi Bobby asepe tu akapate changamoto mpya aidha Atletico Madrid ama Barcelona tetesi ni wao wanamhitaji.

Keita duuh huyu dogo mechi 20 kwa msimu hawezi kukupa kwa vile majeruhi kwake hayachezi mbali aodoke tu nafasi yake aje mwingine damu changa mwenye uhakika wa mechi 40 kwa msimu design kama alivyokua Gini.

YNWA
 
Keita na milner nao wabaki... milner kwa ajili ya dressing room nasikia Ni kiongoz hasa...keita ameanza kuonesha thaman yake..abaki aisee
Ishu ndugu yangu ukumbuke Manchester United, Tottenham na Arsenal dirisha hii watazidi kujiimarisha na bila kuuza aua mchezaji asepe mwenyewe pale sioni FSG wakisajili hivyo ili kuweka space kwa wengine lazima baadhi ya hawa ma A list wasepe Keita ni bonge la talent lakini hio pekee haitoshi kama uzima wake ni wa mashaka tunahitaji mchezaji kama Salah alivyo tangu atue Liverpool amekosa mechi 3 tu na moja ya hizo ni aliumwo corona hivyo utaona dogo ni Mr Fit. Tunahitaji hio consistency ya kua na identity uwanjani kwa kikosi kamili kinvyohitajika.

Pia kwa kasi ya EPl Keita imemchemsha maana dogo hata mbio kwake ni mtihani sana na utaona muda mwingi hua anapoza mpira hii siwezi kumlaumu sana maana mfumo wa Klopp MF zinacheza tofauti na tumu zingine. Ingekua ni mfumo ule aliokua anacheza RB namba 10 naamini hata kwa hizi mechi chache anazokua mzima tungeona ubora wake. Fahamu sio wachezaji wote ambao wapo flexible ku adapt kwenye mfumo alioozoea na hili kwa Keita ni kikwazo sana. Ameshauriwa athari za injury zake zipo mental zaidi kuliko physical ndio maana unaona sasa hata tackling anapiga yaaani kajifungulia. Ilifika mahala uoga ukawa unamtawala sana.

Milner moyo unataka lakini mwili unagoma.

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…