Liverpool FC (The Reds) | Special Thread


Takumi rasmi hata mahojiano anafanya na kingereza sasa ina maana lugha ya Malikia kwake sio tena kikwazo hivyo Klopp na jopo lake la waalimu atawaelewa zaidi.

Mkumbuke huyu dogo hata Kijremani hakua anakijua kivilee. Lugha hua kikwazo wakati mwingine kupewa maelekezo aidha na walimu au wachezaji wenzake.

Jumapili huyu yupo uwanjani kuwavaa Chelsea hii Carabao yuko moto sana.

YNWA
 
View attachment 2130952

MF maestro mechi ya Leeds kafikisha rasmi mechi 50 kucheza tangu ametua Anfield.

Kwa sasa naona Klopp washajua namna ya kupangalia dakika zake uwanjani ili kupunguza majeraha ya mara kwa mara.

YNWA
Kocha kwasema Kovacic yupo available subiri mkutane na watu wa kazi pale Kati Kovacic na Kante na kizuri zaidi James amerudi sipati hiyo picha hiyo game
 
Hiyo kusema mkifunga goal 2 tumewamaliza tunaweza kuongeza zaidi unazungumzia Chelsea ipi Unaweza kufanya hivyo au ushajitoa ufahamu nyinyi si mlitufunga goal 2 ndani ya half ya 1 hiyo hiyo zikarudi zote na tukawazidi game mpaka mkatamani game iishe au sio nyinyi
 
baada ya ushindi wao dhidi ya leeds na inter basi vichwa vimevimba washajiona wao ndio wakubeba kila kombe😂😂😂
 
kante huwa anatukamia sana, yani fomu yake inakuwa juu sana akikutana na sisi, naamini tutamdhibiti
 
Kocha kwasema Kovacic yupo available subiri mkutane na watu wa kazi pale Kati Kovacic na Kante na kizuri zaidi James amerudi sipati hiyo picha hiyo game
Kovacic na Kante mzee baba ni MF makini sanaaa. Naona majeruhi kwako ni Chilwell.

Itakua fainali powa sana.

Ni zawadi kwa mashabiki.

YNWA
 
Hanna ubavu wakuchukua mbele ya chelseafc ya TT
Hivi kwani TT hahusiki kuchukua kombe la EPL...

Uzuri Chelsea mnacheza powa sana vile vile Liverpool tupo moto balaa hivyo pale ni upangaji wa kikosi na utayari wa wachezaji siku husika.


Head to head ndio hio hapo.

Thomas ameshinda makombe 10 almost nusu yake akishinda na PSG kule farmers league.

Klopp ameshinda makombe 9.

Itakua gemu ngumu sana upande wa tactics.

Uzuri hatuna visingizio mpaka sasa angalau timu zote zina majeruhi yanayovumilika.

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…