Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Adjustments.jpg
 
Nilivyokodoa Macho Kwa TV Yaani,

Apa Usingizi Mzuri Ila Huyu Diaz Simba tungekua Na Mpunga tungemchukua tu.
 
Hii gemu ya leo ilikua kipimo tosha sana kwetu mstakambali wa Mashindano haya ya Uefa msimu huu.

Bila shaka haijalishi gemu imechezwa vipi maana ugenini mechi ya mtoano kutoka na ushindi sio haba. Inter Milan sio timu rahisi lakini uvumilivu wetu umelipa sanaaa. Msimu huu tumerudi kulee kwa kuua mechi dakika 20 za mwisho hii inaonyesha ukomavu wenyewe enzi zile wakiita Fergie time haha.


YNWA
 
Namna alivyopiga kichwa kile na mpira ulipoingilia,duh me amenishangaza kwa kweli.
Huyu jamaa na Origi wana zali fulani hivi kwenye mechi za hivi kumbuka ile Club World Cup anawazima wa Brazil nadhani Flamengo dakika ya 99. Au ile mechi anawazima PSG tukashinda yaaani huyu bwana sioni hata Klopp akimwachilia labda yeye mwenyewe aseme anahitaji changamoto mpya.

YNWA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom