Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Ana miaka mitatu aisee kutuonyesha anastahili hii kazi..

Ni muhimu sana wakati wa kumpata mridhi wa Norbert Klopp tuwe makini tusifuate hisia mbali uwezo wa kocha mtarajiwa tuepushe yanayowakuta Manchester United na Arsenal kwa sasa wamebaki kutapatapa.

Ameanza vizuri sana Aston Villa tena anatumia mfumo pendwa wa Klopp 4 3 3 hivyo tumpe muda tuone uwezo wake pale atawafikisha wapi mpaka hio Mei 2024.

YNWA
 

Salah jana hakufurahia kutolewa kama ambavyo siku zote hua hafurahii kutolewa.

Upande fulani unamwelewa kwa vile dogo ni mpambanaji mpaka kipenga cha mwisho akitaka goli ama atoe assist.

Upande mwingine sasa nae ni binadamu anahitaji mwili uwe na utulivu kujiweka sawa akusanye nguvu upya kwani mechi kuanzia hii ya jana mpaka tarehe 2 kuna mechi 6 kali tunacheza EPL mpaka tarehe 2/1/22.

Upande mwingine pia sasa afahamu hata wanaosubiri kwenye benchi nao wanahitaji dakika kadhaa uwajani kupambana kwa ajili ya timu.

Najiuliza hivi akina Gomez, Origi, Tsimikas, Ox, Keita, Taikumi ambao muda mwingi hua hawapati namba kikosi cha kwanza hua wanajisikia aje kila siku ya mechi wakianzia benchi bila kua na uhakika wa kupata kucheza mpaka pale aidha itokee majeruhi ama sub kama jana vile.

Naona hii ni unspormanship way kwa kuzingatia tunakoelekea mpaka January 2 na mechi zilivyobanana na zikiwa zinatisha. Fair play muhimu kwa kujenga umoja wa kikosi na pale mwalimu anatoa ishara ya sub basi mchezaji yeyote awe tayari kutoka bila kuonyesha kama kukereka fulani. Wote kazi ni moja tu kuiletea klabu hii mafanikio na hii ni kazi ya wakiwa kama kundi sio mchezaji mmoja mmoja.

Klopp aa usual hanaga mambo ya kung'ang'ania jambo jana ile ile kaipotezea chap na kuanza mipango mechi ijayo dhidi ya Tottenham Jumapili.

YNWA
 
Jamaa ni mchezaji na mpambanaji mzuri sana though ana kaubinafsi fulani
 
Uwezo anao bwana[emoji1787]
Mimi ni timu mahaba...nampenda jamaa .
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…