Kuna makocha shida yao si usajili bali Walihitaji muda zaidi wa kujifunza kuliko kubeba majukumu waliyonayo.
Mfano Lampard:
Msimu uliopita Mashabiki wa Chelsea walilalamika kuwa wanafanya vibaya sababu wamefungiwa usajili! Tukawaambia sababu sio usajili bali uwezo wa kocha ni mdogo basi hawakuamini.
Hatimae Timu ilimaliza Ligi ndani ya Top Four.
Msimu huu wametumia takribani £220M kwenye usajili lakini ndiyo wamekuwa wabovu zaidi kuliko msimu uliopita, Lampard analalamika wachezaji Wavivu but nani responsible na uvivu wa Wachezaji? Jibu ni Kocha mwenyewe.
Kashindwa kuwatumia Harvertz na Werner, pia Joginho aliyeonekana ndiye Muhimili ambao Sarri alikusudia kutengeneza Timu kumzunguka yeye basi Lampard amemuua kiwango kwa 100%.
Lakini kwa Liverpool hali ni Tofauti, Sera ya Matajiri wetu ni Sell to buy!
Hivyo tunaweza kukaa na useless Player kwa muda mrefu na hatutoweza kununua mwengine mpaka tumuuze huyu useless player.
Na ndiyomana ni Vigumu kwa sasa kusajili CB na Mido mpaka tuondoshe Matip na Nat Phillips pale kwenye Backline yetu, na ni vigumu kusajili Mido mpaka tuondoshe Gini au OX au Keita while Milner his time inahesabika.