Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Mara nyingi huwa napenda kusema kuwa ile Timu ilipata yale mafanikio ya miaka 2 Fasta Fasta kwa sababu ya Makamanda Wanne tu ambao ndiyo walikuwa Key Players.

1) KDB
2) FERNANDINHO
3) LAPORTE
4) AGUERO

Hao ndiyo walikuwa Key Players na kiini cha mafanikio ya Man City.

- Yani misimu miwili ya mafanikio ya Man City KDB alipiga Mpira wa hatari na ajabu mpaka kila Tunzo basi lazima umuone! Na wengi tulimuhesabu kama Midfield bora wa wakati ule.

- Tukiangalia Aguero alikuwa anafunga mpaka kwenye Impossible angle kiasi ya kwamba beki zikimuona tu zinaweza kumuachia mpira kwa hofu tu ili afunge.

- Tukija kwa FERNANDINHO dah! Huyu Kiumbe siwezi kumsahau yani alikuwa akilikamata Dimba basi Mido zenu lazima zikimbilie Polisi! Nakumbuka kuna Game tulikutana nao akiwakusanya wote kina GINI, HENDO na MILNER akawawekea mfukoni akatawala Dimba la kati mwanzo mwisho.

- Ukija kwa LAPORTE huyu alikuwa ni zaidi ya Beki, Ilifika mahala ikawa kuna ubishani wa Magwiji wa Soccer kulinganisha Laporte na VVD ni nani zaidi. Kiukweli alikuwa Beki hatari sana kwa kipindi chake.

HALI YA SASA KWA MAN CITY:

- KDB: Baada ya injury za mara kwa mara zilizomkabili sasahivi ni wakawaida tu hana uwezo tena wa kuipatia Man City matokeo from nowhere.

- FERNANDINHO: Kwa sasa ni Veteran tu na Legend wa Man City lakini si mchezaji tena wa kucheza Timu kama Man City, ni heri aende Marekani akale Pensheni.

- AGUERO: Huyu ni ndugu na OX linapokuja suala la injury hivyo mchango wake kwa Man city haufiki hata asilimia 5%, kiufupi naye ameisha.

- LAPORTE: Huyu naye injury za muda mrefu na mara kwa mara zimefanya kuwa ni Maguire aliyechangamka.
Uwezo wake umeporomoka kwa asilimia zipatazo 50%.

Hivyo PEP ile Man City ya mafanikio inahitaji zaidi ya £500M kuitengeneza tena kwani kina Rodri, Ake, Mahrez, Jesus na Bernardo wameshindwa kabisa kuvaa viatu vya Hao Miamba niliyowaelezea sifa zao.
Silver alikua mtam sana kwenye kutafuta goli
 
YNWA

Game ya leo imekuja muda muafaka wa Liverpool kuwaonesha wapinzani kwamba sisi sio timu ya mtu mmoja!
Watu wanajaribu kututoa katika mbio za ubingwa, leo tunampiga Leicester then tunaongoza ligi rasmi na hakuna atayetutoa kileleni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom