Liverpool FC (The Reds) | Special Thread


Jana baada ya game niliingia website ya BBC, Match of The Day.

Kuna polls nadhani ilifanywa na BBC wenyewe kwa mashabiki wa Liverpool kuhusu Jota kuwa starter nafasi ya Bobby.

Around 5,000 wanataka Jota aanze, na ni 1,000 pekee wanaotaka aendelee kuanzia benchi.

Ninachokiona hapa kelele za mashabiki zinaweza kulipa, Klopp akafanya mabadiliko.

Pia interview ya Klopp (post match) alisema, "He's much better than I thought he would be and that's really impressive,"

"He's an exceptional talent. He has the speed, physicality, technique, and he's both-footed."

Hii ni indicator ya Klopp kuanza kumwelewa Jota na ikibidi afanye jambo nafasi ya Bobby.

La sivyo ni mpaka tupoteze poteze mechi kadhaa ndo mabadiliko yafanyike kama ilovyokuwa kwa Fabinho na Hendo (kumchezesha Hendo namba 6 kulitucost ubingwa msimu ule).
 

Yes, injuries imekuwa ni shida. Hata hivyo timu ilicheza kama mabingwa watetezi.

Tatizo langu kubwa ni kwa Firmino (ameisha), nikisema amechoka nitakuwa sijitendei haki, ameisha.

Salah na Mane waangalie jinsi wanavyoweza kucheza kama timu na siyo kama individuals. Wamekuwa hawapeani pasi au kumpa mwingine pasi haiwi ile ya kumalizia.

Thiago akipona, na kocha akaamua kucheza Fabinho nyuma; viungo Thiago, Hendo na Wijnaldum; mbele Jota, Salah na Mane, hakuna timu inaweza kutusumbua kwenye kutafuta ubingwa. Kama majeruhi yasipoongezeka.
 
Jana Money kapoteza mipira mingi sana pale mbele

Kwenye utafiti wangu mdogo nimegundua kuwa Kwenye Mechi Ngumu Mane ndiyo anakuwa 🔥 na ndiyo anayetubeba, Lakini kwenye mechi nyepesi ambazo tumezidhibiti mwanzo mwisho kama jana Mane anakuwa msanii tu uwanjani.
Subiri game vs Man City utaprove hilo.
 

Firmino huu ni msimu wa pili anacheza mauno tu kama Gwajima! Kwahiyo misimu miwili huwezi kusema mchezaji amechoka wakati alipumzika miezi 3 kipindi cha Corona.

Ukweli ni kwamba Bobby amekwisha muda wake, sasa ni kusubiri mkataba wake umalize aende sehemu ambayo atapata nafasi ya kucheza.
 
Ila hizi gemu za siku hizi tunaomba na mpira uishe, maana point tatu za tabu kweli.
Yaani tukishashinda tu tunaomba mpira uishe haraka kwasababu ya ulinzi,.maana mnaweza kuchezewa counter attack moja matata hata dakika ya 94 mkatoka suluhu
 

Jota kwasasa aanze tu hakuna namna, Na asichezeshwe Pembeni bali achezeshwe Striker.

MANE - JOTA - SALAH
 
Yaani tukishashinda tu tunaomba mpira uishe haraka kwasababu ya ulinzi,.maana mnaweza kuchezewa counter attack moja matata hata dakika ya 94 mkatoka suluhu

Hii Timu ikitengenea kwenye Ulinzi tu basi tunabeba tena EPL, na akipona Fabinho na Thiago tu basi ninaimani tunawezaje kubeba na UCL.


Kikosi changu cha Msimu huu.

MANE - JOTA - SALAH

THIAGO - FABINHO - HENDO

ROBBO - MATIP - GOMEZ - TAA

ALISSON​
 

Hiki kikosi kikiaminiwa, ubingwa ni asubuhi tu.
 
Naunga mkono
 
Salah ulimuonaje mkuu,amekua na touches za kijinga sana siku hizi utulivu umepotea kabisa

Salah na Mane mimi hata siwajadili tena uchezaji wao kwasababu huu ni msimu wa Tatu wanacheza vile! Hivyo inaonesha Kocha ameridhia au wanacheza vile kwa maelekezo ya Kocha.

Enewey! Hawa ni wachezaji wetu muhimu Mno kwani adui hajui ni muda gani watafunga.
 
Sawa mkuu nimekuelewa. Ila kwa wakati huu ambao front 3 yetu inaonyesha kusuasua klopp hana budi kuwatumia, Hivyo swala la kupata nafasi sina mashaka nalo na ndo maana unaona anajaribu kutengeneza mfumo utakao wawezesha Jota/Shaqiri wote kucheza.

Kwa Mtazamo wangu naona tunawategemea sana new player kuliko hawa waliopo maana niwachache mpaka sasa walio maintain viwango vyao. Wengi wao wame flop.
 
Hiyo pasi na hilo goli vinatosha kuturudishia internet.
Sana pass hata VPN haifai, nahati mbaya Shakir hapati sifa anazostahili anafaa sana hasa tukicheza na team wanao defend deep anauwezo wa pass fupi maeneo tight inaweza kuwa baadhi ya mechi asifit kama mnakumbuka mechi na Barca kwa style ile ya mpira wa chini anaweza sana kupenyeza mipira maeneo yake. Huyu sio wa kumuuza atatufaa sana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…