Wewe
Bengalisis na huyo mwenzako
Octa_dre96 wote mmekaza vichwa, ushabiki umewajaa mnaropoka tu!
Jamaa
Econometrician hajasema kama ile red card sio halali, ile ni straight hakuna anaipinga..
Lakini kama isingetokea ile ajali, ile game ingekuwa ngumu kwenu. Ukiangalia kabla ya Chelsea kupata umeme, ile game ilishaanza kuwa tight kwa timu zote 2.
Tukiweka ushabiki pembeni kipindi cha kwanza nawapa credit Chelsea, walicheza vizuri.. Mashambulizi yao yalikuwa ni hatari zaidi.
Hata kwenye ukuta wao Chelsea wakina Zouma waliweza kumzuia vizuri yule mwarabu wenu.
Kwenye back four yenu bado hakujakaa sawa.. Pamoja na kumrudisha chini Fabinho sijaona kama ile namba itamfaa msimu mzima.
Huyo Fabinho mwenyewe alivyokuwa nyonde nyonde vile tukisema zipigwe zile counter attack kutoka kwa timu pinzani halafu abakie yeye na straika kama Vardy au Auba tunahesabu chuma tu!
Kuna attempt moja aliifanya Timo Werner kwenye 1st half, nje ya dimba.. Alimgongesha mpira Fabinho usoni, ukamrudia tena akasogea akapiga ikaenda nje.
Nikiiangalia ile najisemea tu mwenyewe hawa Liverpool wakiendelea kumpanga huyu Fabinho kwenye position ile, sina shaka na yeye ataanza kuwa wakala wa assist kama mwenzake VVD.
LIts just matter of time!