The MoNA
JF-Expert Member
- Sep 19, 2014
- 4,264
- 10,503
STEVEN GERRARD, SEE YOU AGAIN MY FRIEND…
Siku Steven Gerrard anaagwa pale Anfield hakika machozi yalinilenga ila sikulia na niliwaza saana itakuwaje Liverpool bila yake , ni ukweli usiopingika inaanza klabu ndio anafuata mchezaji hakuna aliye mkubwa kuliko timu . Hakika mapenzi ni upofu na unachokiona wewe mimi sikioni kama umemuona Xavi mimi nimemuona Gerrard , kila kitu kina sababu duniani na mimi sababu ya kupenda mpira alikua Steven Gerrard niliamini naamini na nitaendelea kuamini huyu ndiye mchezaji bora wa muda wote ( the best there was , the best there is and the best ever will be)…
Steven Gerrard alinipa maana halisi ya soka la kipiganaji na mapambano bila kukata tamaa kuna muda naangalia mpira naona kivuli chake , Pogba alimkaba shingo Jordan Handerson tena katika North West Derby lakini Jordan alipotezea tu sijui Gerrard angefanya nini ?, Salah anavunjwa bega na Ramos tena anatoka analia lakini sikuona kisasi kutoka kwa kina Handerson na kina Lovren hakika angekuwepo Gerrard damu ingemwagika pale , Mechi na Olympiacos 2005 jamaa anapiga goli la 3 la ushindi ile namba nane haionekani vizuri imechafuka tope japo ni marudio lakini mwili unasisimka Mungu niletee Gerrard mwingine nakuomba , Gerrard alianza vurugu akiwa timu za vijana hadi viongozi wa Liverpool walijua kabisa akiendelea kuchezea timu za watoto watakua wanatwanga maji kwenye kinu ..
Nikikumbuka namna Gerrard alikua anapiga zile Sliding Tackle nafurahi sana yaani ule ujasiri wa kuingia uvunguni mwa Roy Keane nani angeweza ? , huyu Roy Keane ndio alikua anastaafisha watu kwa kuwavunja miguu , akiwa na miaka 20 msimu wa 2000/2001 aliingia kwenye kikosi cha msimu cha ligi kuu tena kama kiungo tunakumbushana tu enzi izo kiungo kilikua kiungo haswa Patrick Vieira , Roy Keane , Emanuel Petit , Paul Scholes , Nick Butt , Frank Lampard , David Beckam , . David Moyes aliwahi sema kwanini aiogope Liverpool wakati haina Gerrard , Michael Owen nae aliwahi kama atakwenda kucheza mechi yoyote duniani basi mtu wa kwanza atamchagua Gerrard , Patric Vieira alimshangaa Gerrard hamuogopi anampiga viatu tu , Klopp amewahi sema kau nahodha wa Liverpool ni kazi ya lawama sababu nahodha aliyepita alikua ni Gerrard….
Vita katika eneo la kiungo zinaamuliwa na watu wagumu kama Steven Gerrard kiungo bila ngumi , mateke , viatu , mashuti makali na ufundi ni sawa na bure , saivi mtu anakwenda hadi hatua kumi bado hajalazwa chini sasa unaachaje kuwakumbuka kina Gerrard na Roy Keane ? . Uongozi wa Liverpool ulikua katika mawazo ya kumtema sababu kijana sababu kila akiingia sub lazima alaze watu hata kama anacheza winga , kijana wa miaka 19 anapata kadi nyekundu tena bila onyo baada ya kumvunja Kelvin Campbell , baada ya kukabidhiwa unahodha 2003 kocha Gerrard Houllier alisema kijana alistahili kuwa nahodha tangu anapandishwa timu za wakubwa ila walisubiri akue kiakili maana muda wowote angeicost timu . Lampard amewahi sema kukutana na Gerrard Anfield ni hatari sana wala sio nzuri kiafya atakuumiza , UEFA wametoa kikosi bora chao kutoka 2000-2010 na Gerrard yumo , akiwa hajawahi beba EPL lakini kaingia kwenye kikosi cha msimu mara nane , naomba sana nikiwa hai aje Gerrard mwingine …
Moja ya kitu ninachopenda kutoka kwa makapteni wa kiingereza ni sura zao za kazi wanazoweka kipindi wapo kwenye korido , Messi anacheka cheka tu Ramos anabusu watu ovyo ovyo Ronaldo ndio kwanza anashikashika ndevu , embu mcheki John Terry au Steven Gerrard mwenyewe yaani raha tupu nakwambia ipo raha kwenye ukauzu .