Duu Manchester United wamekua kama Liverpool enzi hizo tunakamia gemu kubwa aafu tunakutana na QPR, Wigan nk tunachezea balaa..
Ile ilikuwa ni Small Team Mentality.
Kawaida ya Mentality ya Timu Ndogo atafungwa 5 - 0 uwanjani kwake na Kibonde mwenzake, Lakini atataka atoe japo Sare ugenini kwa Man city au Liverpool.
Sasa kipindi hicho tunamfunga Chelsea au Arsenal lakini tunapigwa Nje - Ndani na Stoke City.
Hiyo ilikuwa ndiyo Mentality yetu ya Small Team huku tukijilazimisha tuonekane eti sisi ni Miamba ya Ulaya.
Kiukweli kabla ya kuja Klopp tulikuwa ni Timu ndogo.
Sasa na Manure nawao rayari wameshakuwa na Small team Mentality ya kukamia Big Matches huku wakiliwa na Vibonde.
Karibu wataanza kujivunia Historia kama tulivokuwa sisi.
Kipindi hicho tulikuwa tukijitapa na usajili wa Wachezaji kama Maxi Rodriquez, Fabio Borini, Arbeloa, Balotelli, Kolo Toure, Mignolet, Lallana, Lovren, Voronini, Dosena, Coates, Lambart, Origi, Henderson, Adam, Riera, na Midocre wengi tu huku tukijipongeza kwa sajili hizo mbovu kabisa. Hii tulikuwa na Small Team Mentality.
Sasahivi tunatakiwa tuondoke kwenye Mentality hii ya kukumbatia Hawa Mediocre players ambao wanafaidi Matunda kupitia Jasho la Wengine.
But you'll see someone anasema Ameshaitumikia Timu, So tusisajili tena wachezaji wapya Bali tuwarudiahe kina Aggar, Carra, Gerrard, Skirtel, Alonso, Barros, Fowler, Owen waendelee kucheza kwasababu tu walishaitumikia Timu??