Ile ilikuwa ni Small Team Mentality.
Kawaida ya Mentality ya Timu Ndogo atafungwa 5 - 0 uwanjani kwake na Kibonde mwenzake, Lakini atataka atoe japo Sare ugenini kwa Man city au Liverpool.
Sasa kipindi hicho tunamfunga Chelsea au Arsenal lakini tunapigwa Nje - Ndani na Stoke City.
Hiyo ilikuwa ndiyo Mentality yetu ya Small Team huku tukijilazimisha tuonekane eti sisi ni Miamba ya Ulaya.
Kiukweli kabla ya kuja Klopp tulikuwa ni Timu ndogo.
Sasa na Manure nawao rayari wameshakuwa na Small team Mentality ya kukamia Big Matches huku wakiliwa na Vibonde.
Karibu wataanza kujivunia Historia kama tulivokuwa sisi.
Kipindi hicho tulikuwa tukijitapa na usajili wa Wachezaji kama Maxi Rodriquez, Fabio Borini, Arbeloa, Balotelli, Kolo Toure, Mignolet, Lallana, Lovren, Voronini, Dosena, Coates, Lambart, Origi, Henderson, Adam, Riera, na Midocre wengi tu huku tukijipongeza kwa sajili hizo mbovu kabisa. Hii tulikuwa na Small Team Mentality.
Sasahivi tunatakiwa tuondoke kwenye Mentality hii ya kukumbatia Hawa Mediocre players ambao wanafaidi Matunda kupitia Jasho la Wengine.
But you'll see someone anasema Ameshaitumikia Timu, So tusisajili tena wachezaji wapya Bali tuwarudiahe kina Aggar, Carra, Gerrard, Skirtel, Alonso, Barros, Fowler, Owen waendelee kucheza kwasababu tu walishaitumikia Timu??
Ni sahihi kabisa ndugu aisee enzi hizo tuliwafunga Chelsea ama timu yoyote ya Big four tulikua mtaani hatukamatika aafu tunakuja kuzimwa na Sunderland, Portsmouth, Birmingham nk huku ma super start wetu ni akina Insua, Glen Johnson, Downing, Nabil, Gonzalez, Palleta, Balotelli, Moreno, Zenden nk...
Ki ukweli ujio Wa Fenway Sports Group na akina Lebron James ulituokoa na wametutoa parefu japo mwanzoni hawakueleweka vyema wanavyofanya uwekezaji kiasi kuna mashabiki walisema hawatakiwi waondoke lakini baada ya kumpata Klopp na ku stabilise account za Klabu sasa tume waona na kuwaelewa zaidi na tunahitaji waedelee kuwepo klabuni wanatufaa mnoo..
Kuanzia msimu wa 2010 mpaka tunakuja kupata UCL 2019 ki ukweli tumepondwa, tumedharaulika, tumekejeliwa eti ni ma specialist in failure nk ndio sasa Tunatembea kifua mbele tupo kwenye laiti track na hatuyumbishwi na timu yoyote, wao wacheze mpira wao sisi tucheze wetu na kwa vile tumekomaa nafasi za ushindi zitapatikana tu.. Hakika najivunia kushabikia Majogoo kipindi hiki huliko kipindi chote kile nasema asante Klopp asante vijana Kwa kazi nzuri na kuwazima wapinzani wetu kabisaaa na ole wao tukichukua kubwa lao EPL hapo sasa wataibuka na maneno mengi mengi mara VAR na kadhalika...
Liverpool Kwa sasa sio tena stepping stone ya wachezaji kuja hapa kusudi wapate kutambulika na kwenda kwingineko kama akina Surez, Torres, Sterling, Owen nk,.. Kwa sasa tuna uwezo wa kushindana mashindano yoyote yale Kwa kikosi alichokijenga Klopp, pia tuna uwezo wa kuwavutia wachezaji bora kabisa kuja kijiunga na timu ya ushindi..
Klopp kuongeza mkataba ni mshale Kwa wapinzani japo nimesoma na Pep nae yupo tayari kuongeza endapo Uongozi Wa Citizens ukiona anafaa kuedelea kuwafundisha....
Tuna uhakika wa kuedelea na hii furaha kwa kazi nzuri sana ya Edwards kuzidi kum support Klopp na bila shaka Klopp hajawaangusha Kwa vile sasa value ya Klabu imeongezeka mara dufu na lengo ni miaka mitano ijayo tuwe 3 bora duniani kifedha Kwa timu za mpira...Takumi kaja pia kimkakati zaidi huku nako fursa zitakua nyingi...
Adidas walitutema mwaka 2012 Kwa kusema we are to risky.. Haha they wish..New Balance wakaingia ndani through their subsidiary Worrior, upande wa jezi na washirika wengine kama Carlsberg, Nivea, XAX nk bado wapo na sisi na wanaamini kibiashara wamewekeza mahala sahihi hii imewavuta na Titan waitwo Nike kuja kuwekeza na kua mshirika wetu Kwa kutoa ofa HATAREE, haya yote ni Klopp, wasaidizi wake, wachezaji na never dying passion ya mashabiki Wa Liverpool..
Together we have come far and now we are harvesting higherly believing in this drankard master who told us he will make us Great again and he has kept his word..
Bye bye mediocre players na wale tulionao siku zao zinahesabika klabuni... So far kashawatoa Sakho, Benteke, Ings, Balotelli, Aspas, Moreno, Kolo, Skertel nk