Hii ni moja ya Derby kali kabisa duniani, kwenye Derby hua anaejichanganya tu basi anapigwa mzee...
Hii mechi Kwa Manu ina umuhimu kuliko mechi yoyote ile msimu huu, kwanza akipigwa hati hati ajikute nafasi ya 17 au 18 endapo walio chini yake washinde wote, kingine pia wana matarajio makubwa mno Kwa kua kikosi pale nyuma kitakua kimekamalika Bin, Maguire, Lindlof, Shaw wote wanaweza kua in contention...
Pale mbele wanaweza kua na Maritial ambae amekaa nje muda tu, hao Wachezaji kwao wanaona wamerudi wakati mwafaka kutuharibia rekodi ya kushinda mechi 18 EPL consecutively na kumpa ari noisy neighbour Citi... Walituharibia msimu uliopita tuka draw mechi ile na ndio ilitunyima ubingwa na bila shaka na msimu huu wanajipanga tena kuharibu shughuli...
Kingine kwao pia wanaona hii mechi itawajenga kuanza upya ligi baada ya kupata matokeo mambovu kuliko wakati wote ule of late...
Kwa bahati mbaya hawatakua na Pogba wala Degea ambao waliwatarajia Sana mechi hii.. Degea ni pigo kwao na huyu jamaa sijui ana kisasi na sisi pindi tunapokutana hua anakua moto ajabu..
Na mwisho rekodi yetu OT hairidhishi miaka ya hivi karibu hua aidha tunatoa sare ama tunapigwa hilo nalo linawapa motisha kupigana Sana watuharibie kujikita kileleni na pia wajisaidie wenyewe kusonga nafasi za juu zaidi...
Klopp asipoamkia mvinyo na kutupangia akina Lalllana basi tutatoka kifua mbele na hatimae kumaliza hili gundu la kutotoka na point 3 OT....
Tukiwadhibiti ma winger wao basi kazi imekwisha mapema kabisa....
In Klopp I trust