Baba Swalehe
JF-Expert Member
- Jun 6, 2017
- 20,220
- 39,854
Hahahaha ... Alikua anawapa story za demu wake wa utotoni !'Mkiachia Video naondoka' .
Jurgen Klopp amesema kwamba ataondoka klabuni endapo Liverpool wataachia video akiwa anaongea na wachezaji wake wakati wa Mapumziko baada ya Salzburg kuachia video ya kocha wao Jesse Marsch akiwa na anaongea kwa hisia sana na wachezaji wake wakati wa mapumziko kwenye mechi ya UEFA dhidi ya Liverpool .
Klopp amesema kwamba hatovumilia kitendo kama hiko endapo Liverpool wakifanya hivyo.
.
.
. " Kama LFCTV wakiweka hadharani video yangu nikiwa nafanya hivyo, nitaondoka klabuni . Huo ndio ukweli na hilo ndio wanaweza kusema kuhusiana na hali hiyo ."
Trent alikua anacheka kinoma !


Hendo ndo alicheka mpaka akalia !


...#YNWA