Mwacheni Hendo apumue.
Ina maana hawa makocha wote waliompanga nao ni vilaza
1.King kenny
2.rodgers
3.Kloop
4.Southgate
Yaani wewe shabiki ndo ujue kila kitu kuliko hawa wanne. Kila mchezaji ana faida zake na hasara zake pia.
√ Nani aliyekwambia kumpanga mchezaji bovu uwanjani ni kuwa kocha kilaza?
√ Nani aliyekwambia kila mchezaji anayepangwa uwanjani ni mzuri?
√ Kwanini Lovren alikuwa Akichezeshwa Kila game na Klopp, Lakini sasahivi hachezeshwi game hata moja na Klopp huyuhuyu?
√ Hivi unaweza kunipa sababu kwanini Klopp huyuhuyu alipokuwa akimng'ang'ania kumpanga Lovren kila game sisi tulikuwa tukimkosoa Munasema Klopp anajua Kuliko sisi, Lakini Klopp huyuhuyu kaamua kumueka Benchi Lovren hatimae hamusemi Klopp hajui tena kwasababu hamchezeshi Lovren? Au Klopp anajua anapomchezesha mchezaji kwa lazima tu, Lakini asipomchezesha kujua na kutojua kwake hakuwahusu?
√ Unajuwa kuwa Tokea aondoke Alonso na Mascherano Liverpool haijawahi tena kupata Midfield zinazotambulika?
JUA HAYA:
1) Situation ya Lovren ni Sawa na ya Henderson:
- Hao Makocha wote uliowataja (Sir Keny, Rodgers, Klopp na Southgate) hawamchezeshi Hendo kwa kuwa anajua au kwasababu ya kuwa wao wanajua zaidi! Bali wanamchezesha Hendo kwasababu hawakuwa na Hawana wachezaji wa Maana katika Vikosi vyao kwenye eneo la Midfield.
* Keny, Rodgers walikuwa na vikosi kibovu ndiyomana Hendo akacheza
* Klopp Mido zake ni Gini, Milner, Fabi, Nabi, Lallana na OX, hapo anayecheza ni Gini na Fabi, Nabi na Ox ni sawa na Wahudumu wa Afya Wodini, Lallana na Milner hamna kitu! Sasa Hendo ataachaje kucheza hapo? Je nibkwasababu Mkali au kwasababu hatuna Mido ya maana?
Ni sawa na Lovren wakati anapangwa kila game Watu walidai Klopp anajua zaidi, Asinhelimpanga isipokuwa Lovren ni Beki Mzuri! Kumbe alikuwa Akipangwa kwasababu Klopp alikuwa hana Beki mwengine wa maana.
Alipoibuka Gomez tu, Matip kupona majeruhi na kuja kwa VVD yupowapi Lovren now?
Ule ubeki bora wake umeendea wapi?
Ile Klopp kumpanga kwasababu anajua zaidi imeishia wapi?
2) Kuondoka kwa Alonso na Mascherano:
Tokea waondoke hao jamaa Liverpool haijawahi kupata tena Midfield ya Calibre ya hao jamaa! Ndiyomana Hendo katawala kwasababu wote waliopo (Ukitoa Keita & Ox majeruhi) ni wabovu angalau yeye ana afadhali.
Kwahiyo Klopp kumchezesha Hendo sio Kilaza, Bali tunamlaumu kwanini hasajili upgrade ya Hendo!
Na wala Hendo kuchezeshwa sio sababu kuwa yeye ni Bora, bali ni kwamba Liverpool haina kiungo wa maana.
Hendo ni Kiungo mshambuliaji mbele ya Gini na Fabinho Lakini je Mpaka mwisho wa msimu hafikishi hata goli 5 na assists 5 sasa anafaida gani kwenye Timu?