Hivi wakati Klopp anamuita TAA kikosi cha wakubwa ni nani aliyetegemea TAA angefanya maajabu kama tunayoyashuhudia sasa? Klopp alipomnunua Robertson tulijua anatuletea mzigo tu lakini shughuli ya Robertson tunaiona sote ni mashahidi.. Hivi karibu kamnunua Van Den Berg nani anaujua uwezo wa huyu dogo?
Wakati Klopp akiwa Dortmund alitumia kiasi cha paund 22.37 million kununua wachezaji watano wa kiwango cha juu kabisa.
1. Shinji Kagawa bure
2. Piszeck bure
3. Lewandowsk paund 3.33 m
4. Aubameyang paund 9.1 m
5. Subotic 3.15 paund m
Kwa hiyo suala la kusema Klopp hasajili tuliache yeye anajua kuliko hata sisi tunaompigia kelele.
_Jumapili njema Kops

_
Nadhani bado hujajuwa nini kinajadiliwa kuhusu Usajili, Au hukukipitia ulichokiandika.
TAA na GOMEZ hawakuwa First choice takriban misimu miwili ya mwanzo.
Na kilichofanya TAA akaingia First XI ni kuumia kwa Clyne jambo ambalo hatukuwa na RB mwengine kiasi ya kwamba mpaka leo tuna RB mmoja tu ambaye ni TAA pekee.
Kuhusu Robertson ulichokisema sio kweli kuwa tulikosoa au kuponda usajili wake kwani hakuna aliyekuwa akijua kuhusu usajili wa Mchezaji Huyo kwani kusajiliwa kwake ni sawa na Fabinho waliibuka tu from nowhere bila ya kiwepo tetesi za kuaminika kuhusu usajili wao.
Wengi wetu tulikuja kumuona tu Robertson akiwa uwanjani na tukamsifia sana kuhusu uchezaji wake.
"Kuna watu hutumia kivuli cha usajili wa Robertson kama kichaka kuhalalisha hoja zao eti tuliukosoa! Sio kweli hakuna aliyeukosoa"
Kwahiyo na hawa Madogo waliosajiliwa hakuna hata mmoja aliyeponda usajili wao! Sote tunajua kuwa Elliot, Ki-jana na Berg ni talented Young boys, na tunaamini kuwa ni Future nzuri! Lakini Nina uhakika kuwa Mutakuja kusema tulimlaumu Klopp kwa kuwasajili hawa. I swear!
Kama hamujui tunachokosoa sisi ni kutosajili Backups za baadhi ya wachezaji ambao hutumika muda Mkubwa bila ya kupumzishwa kwani hawana mbadala jambo ambalo wakiumia tu au wakichoka kipindi cha January huwa timu inaboronga, na kutokuziba baadhi ya sehemu zenye weakness kama vile namba 10 ambayo mpaka sasa haina Mtu bali inaungwaungwa tu.
Timu ina namba 2 mmoja tu TAA
Timu ina namba 3 mmoja tu Robertson
Je wakiumia hao nafasi zao ataziba nani? Au ndiyo Hendo aje acheze namba 2 kama msimu uliopita?
Hivi Mane, Salah na Fiemino ndiyo waendelee kutumika kama Punda bila ya mtu wa kuziba nafasi zao?
Je mido ndiyo waendelee kucheza kina Milner?
Usidhani kama hawa waliosajiliwa wote msimu huu watacheza kikosi cha kwanza moja kwa moja! Ni wadogo mno Klopp hawezi kutake risk hata Siku moja.
Wote atawapeleka U23 wakakue.