Keyboard_Warrior
JF-Expert Member
- Oct 10, 2015
- 6,106
- 10,471
Maswali mengine ya ajabu sana..!Newcastle najua wapo, hata rais mstaafu Jakaya kikwete ni mshabiki kindakindaki wa Newcastle , ila man city napata ukakasi,.
Ni iko hivi chief, nje ya Uingereza mashabiki wengi wamekua mashabiki wa timu za nchi hiyo kulingana na mafanikio yanayofikiwa na timu husika...
Ili timu iwe na mashabiki nje ya mipaka ya nchi yake ni lazima iwe maarufu,na umaarufu unapatikana kupitia mafanikio...
Bila shaka hata wewe ulianza kuishabikia Arsenal kipindi ukiwa inatisha katika ligi ya Uingereza...
Newcastle ilikua timu ya kutisha kipindi cha akina Alan Shearer, sasa hivi timu imechoka na umaarufu wake umepungua...
Sasa utashangaaje Man City kuwa na mashabiki Bongo wakati ndio timu inayotisha zaidi ndani ya Uingereza kwa wakati huu..!?
