Hivi wadau Ox akipona akawa fit na kurudi kwenye kiwango chake cha mwaka jana. Fabinho, Keita na Gini nao wakaendelea kuperform vizuri. Mnafikiria pale kati Klopp atamweka nani na nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hili swali kwa sisi tunaojua mpira lipo nje ya uwezo wetu! Hatuwezi kulijibu.

But tunaweza kuchangia mawazi yetu tu kwavile hii ni forum.

• FABINHO hwezi kucompete namba na OX au KEITA coz anacheza position tofauti na wao.

So, watakao Compete ni HENDO, GINI, OX na KEITA.

HENDO hapo anakaa pembeni coz hapana anayeweza kumueka bench ikiwa watakuwa fit.

Vita itakuwa ni Kati ya GINI/KEITA/OX

Hapo Wawili wataungana na Fabinho kucheza na mmoja atasubiri kwenye bench.

Kuhusu nani atacheza ni kwamba atakayeperform vizuri zaidi ndiye atakayecheza.
 
Kijiwe cha Liverpool

Unataka Liverpool ipi? Ya Shankly, Dalglish, au Gerrard?

*Bill Shankly*

ROHO za ki-Merseyside. Ngoja nikupe simulizi flani kuhusu wachezaji wa Liverpool na namna ambavyo tunaipenda Timu yetu.

Unaifahamu Blackburn Rovers? Achana na hii inayopambana huko madaraja ya chini. Wala siyo ile ya muuza sura Santa Cruz.

Ipo ile Rovers ya akina Chris Sutton na Alan Sheerer. Sheerer huyu ambaye ni mfungaji bora wa muda wote England na Gwiji la Newcastle.

Unadhani aliyewapa ubingwa Rovers ni Sutton na Sheerer? Unajidanganya. Walipewa ubingwa na mwana-Liverpool.

Sir King Kenny Dalglish. Mfalme na Kocha wa mwisho kuipa Liverpool ubingwa. Ndio aliipa pia Rovers ubingwa wao wa mwisho wa Ligi Kuu.

Stori ya kusisimua ni kwamba baada Rovers kutwaa ubingwa msimu wa 1994/95 ndipo Sir Dalglish alipofanya maamuzi ya ‘ajabu’.

King Kenny alitangaza kujiuzulu ukocha wa Rovers baada ya kutwaa kombe. Na baada ya kujiuzulu ndipo alipofichua dhambi kubwa aliyowahi kuifanya maishani mwake.

Alifichua kuwa hakuna dhambi kubwa amewahi kuifanya kama kuiongoza Rovers kutwaa ubingwa huku Liverpool ikitoka patupu.

Wakati wengine wangesheherekea kwa kuweka rekodi yeye King Kenny aliona bado ni dhambi kubwa kuipa timu nyingine ubingwa.

Jezi namba saba iliyowahi kuvaliwa na Dalglish inatajwa kuwa miongoni mwa jezi zenye thamani na heshima zaidi Anfield.

Unayakumbuka maafa ya Hillsborough yale yaliyoua mashabiki wetu 96 na kujeruhi wengine 700? Basi Kocha alikua ni Dalglish. Mzee kapitia mengi huyu!

Unataka Liverpool ipi? Oke kuna ile ya ‘mungu’ wetu, Bill Shankly. Yule ambaye alianzisha spirit ya upambanaji pale Merseyside.

Ni yeye ambaye aliagiza wimbo wa You'll Never Walk Alone uwe wimbo rasmi wa klabu. Ni yeye ambaye alikianzisha kibao cha ‘This Is Anfield’

Kwaa ambao hawajui ni lazima kila mchezaji na benchi la ufundi kukigusa kibao hiko kabla hawajaingia uwanjani.

Bill alifanya hivyo ili kuwakumbusha wachezaji thamani ya kucheza Liverpool.

Ni yeye ambaye alisema duniani kuna timu bora na kubwa mbili tu. Liverpool na Liverpool ‘Reserve’

Nakupa nyingine: Bill alikua akiichukia dhahiri Everton. Huyu Mzee alikua hasimu kweli wa wale watoto wa Blue.

Aliwahi kusema “ Nikiwa sina kazi yoyote hukaa bustani kwangu na kuiangalia Everton wanavyopambana mwishoni mwa msimamo wa Ligi kuepuka kushuka daraja”

Hii ni kauli yenye kuonesha chuki ya dhahiri kwa mahasimu wetu. Na ni wazi hata Mimi naeandika makala hii siipendi haswa Everton.

Naipenda Liverpool ya Mzee Gerrard Houllier. Hii ilijawa na vijana wenye roho ya upambanaji na vipaji maridhawa kabisa.

Naachaje kumpenda Houllier ilihali yeye ndio alimpa nafasi nahodha bora wa muda wote, Steven Gerrard?

Ni yeye anaeshikilia rekodi ya mataji matatu ndani ya msimu mmoja pale Anfield. Wakati Alex Ferguson akishinda na United makombe matatu 1999, Houllier alifanya hvyo kwetu 2001.

Akiwa na Gerrard, Owen, Steve MacMaman, Jamie Redgnapp na wakali wengine aliwaongoza kushinda mataji matatu. Europa League, FA Cup na Carling Cup (Kombe la Ligi).

Sikiza wewe. Kuna Liverpool ya Rafael Benitez. Hii inatajwa kuwa Liverpool ya kibabe toka karne ya 21 iingie.

Wanaume haswa ambao wangepambana na wewe kwa dakika 90 bila kuchoka.

Usijifanye hujui tulichomfanya AC Milan 2005 na baadaye West Ham mwaka 2006. Hii ni Liverpool ya maajabu kabisa kuwahi kutokea.

Ndio Liverpool ya mwisho kumchapa Manchester United goli nne kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Achana na hiyo ya Benitez: Naipenda Liverpool ya Steven Gerrard pia. Huyu nae mapenzi yake kwetu hayapo mbali na ya Sir Kenny Dalglish.

Akiwa katika kilele chake cha ubora duniani, Real Madrid na Chelsea yake Jose Mourinho ziliweka mezani pauni 30 milioni mwaka 2004 ili kumnasa.

Kwa kipindi hicho ilikua ni pesa kubwa sana. Pengine Gerro angeweka rekodi England. Pesa kitu gani bwana? Gerro akatangaza kwamba hatoondoka na atafia kwetu.

Nini unajua kuhusu mwanaume huyu wa shoka? Ngoja nikupe mastori yake kadhaa. Usichoke!

Kwanza pamoja na kuwa na jezi zaidi ya 100 za timu tofauti kutokana na kubadilishana na wenzake lakini hana hata moja ya Manchester United.

Huwezi kuwa Kop halisi halafu ukawa na jezi za ‘Manyumbu’.

Unakumbuka fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Milan 2005? Hadi mapumziko tulikua nyuma kwa goli tatu.

Wakati wa mapumziko, Gerrard aliwatoa nje watu wote wakiwemo viongozi na benchi la ufundi kisha akabaki na wachezaji tu. Alichowaambia kinabaki kuwa siri yao. Tulivyorudi tulichomoa zote na ubingwa tukabeba.

Naipenda pia Liverpool ya Brendan Rodgers napenda namna ambavyo ilitusisimua na soka lake mujarabu licha ya kwamba tulishindwa kubeba ubingwa.

Hii ni miongoni mwa Liverpool zilizokua zikiutwanga mpira Mkubwa na wenye kuburudisha.

Kombinesheni ya Sturridge na Suarez (SAS) ilikua ni kamambe sana. Tulitoa dozi nene na soka la kuvutia.

Ni kama Rodgers aliihamishia Tik Tak ya Barcelona pale Anfield.

Mimi ni nani niache kuihusudu hii Liverpool ya Jurgen Klopp? Bwana wee. Hii ni Liverpool inayotisha ndani na nje ya uwanja.

Chini ya Klopp tumeweza kuondoka kwenye falsafa yetu ya kizamani ya kununua wachezaji wa bei nafuu na kuanza kuvunja benki.

Kama hufahamu chini ya Klopp tumeweka rekodi mbili za usajili.

Tulimsajili Virgil Van Djik kwa dau la pauni million 75 na kumfanya kuwa beki ghali duniani.

Miezi kadhaa mbele tukalipa pauni 60M tena kumnasa Allison Becker na kumfanya kuwa golikipa ghali.

Ni Klopp huyu ambaye amewavutia nyota kibao kutua Anfield. Unadhani bila yeye leo tungemmiliki Keita, Fabinho na Salah?

Unadhani bila yeye tungefika fainali tatu ndani ya misimu mitatu? Huyu Mzee amerudisha ule ubabe wetu wa enzi ya Shankly na Paisley.

Ni wazi hakuna timu isiyotuogopa kwa sasa. Hao Bayern Munichen wanapiga hesabu watakujaje Anfield.

Manchester United wana hofu na sisi hiyo February 24. Unaambiwa Bobby Charlton, Ferguson, Carlos Quiroz, Phelan na Soljker wamejifungia tayari kupanga kikosi ambacho kitatukabili.

Ghafla nimeikumbuka Liverpool ya pili ya King Kenny. Ndio Liverpool ya mwisho kutwaa kombe. Tulibeba taji la Ligi mwaka 2012.

Sitaki kuikumbuka Liverpool ya Roy Hodgson. Hii ndio Liverpool ya hovyo kuwahi kuishuhudia maishani mwangu. ‘Am sorry Roy’
 
Good article man,

but, Kenny Daglish alichangia kwa kiasi kikubwa poromoko la LFC as a big club.

it took the club years to rectfiy and clear his mess

SG is the most legendary figure in LFC history apart from Shankly and Paisley.
 
BREAKING: Fabinho is set to play at centre back alongside Joël Matip against Bayern Munich tomorrow. It looks as if Dejan Lovren will not be fit in time. [Paul Joyce]

Sent using Jamii Forums mobile app

Brexit Midfield kesho (if thats true)

gonna be long 90 minutes

Bayern are not that good now, so tuna advantage kidogo.

hope Keita starts Aisee
 
Mnasikia kinachowakuta wenzenu hapo Darajani? Ukiona mwenzako ananyolewa anza kutia zako maji mapema

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
jamani watu wanajeuri eti page ya liverpool ya 2947
eti wame chati kwa kingereza jamani

come on liverpool

cityzen chairman am here
 
Back
Top Bottom