Kwanini hiyo miaka yote hakubeba aje kubeba mwaka huu?
Ahahaaah...
Ungesema kuwa Liverpool atabeba kombe mwaka angekubali bila kukuuliza sababu,kwasababu yeye anaamini hivyo...
Ila umesema kuwa Liverpool hawezi kuchukua ubingwa mwaka huu,anahitaji kujua kwanini umesema hivyo,kwasababu yeye anaamini kuwa msimu huu Liverpool atabeba kombe..!
Binadamu anafurahisha sana,anachokiamini yeye anataka kiwe fact,ambacho unakiamini wewe kwake ni porojo..!
 
Kwanini hiyo miaka yote hakubeba aje kubeba mwaka huu?
Miaka ambayo utawala wa Liverpool unakomeshwa paliibuka na utawala mpya kutoka jiji la Manchester, Manchester United ya Ferguson worked hard for about 6 years mpaka kuondoa huu utawala, kutoka Ferguson aanze kubeba mataji ya EPL hakupata mpinzani hasa financially, huyu mzee alikuwa na economic power kubwa sana, utawala ulioiuzuia Liverpool miaka yote umetoweka

Kwa hiyo katika past season hakukuwepo na team bora ya kuizidi Manchester United ya Ferguson

Kwa hiyo Liverpool wana nafasi kubwa msimu kwa sababu aliyewanyima hayupo, lakini tumeona tangu Klopp aje Liverpool nao wamekuwa na uimara sokoni, hivyo kuwafanya kuwa moja ya team zenye nguvu kubwa kiuchumi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahahaaah...
Ungesema kuwa Liverpool atabeba kombe mwaka angekubali bila kukuuliza sababu,kwasababu yeye anaamini hivyo...
Ila umesema kuwa Liverpool hawezi kuchukua ubingwa mwaka huu,anahitaji kujua kwanini umesema hivyo,kwasababu yeye anaamini kuwa msimu huu Liverpool atabeba kombe..!
Binadamu anafurahisha sana,anachokiamini yeye anataka kiwe fact,ambacho unakiamini wewe kwake ni porojo..!
Sio kwamba atachukua ila yupo kwenye position nzuri ya kubeba ubingwa, kikosi imara, kocha mzuri na wapo vizuri kiuchumi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni swali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza, swali hili limepata uzito siku za hivi karibuni kutokana na sababu kuu mbili

1. Historia ya Liverpool kutobeba ubingwa kwa miaka 29,mara ya mwisho majogoo walibeba taji la ligi kuu mwaka 1990,wamejaribu mara kadhaa kupambana kwa ajili ya taji hilo ila wameishia kumaliza nafasi ya pili,miaka ya hivi karibuni Rafael Benitez(2008/2009) alichuana vikali na Manchester United ya babu lakini aliambulia patupu, kipindi hiki alikuwa na watu bora sana kama Fernando Torres, Javier Mascherano,Steven George Gerrad, Dirk Kuyt, ulikuwa msimu mzuri sana kwa Liverpool licha ya kuukosa ubingwa,kilichowagharimu kipindi hili ilikuwa ni kukosa squad imara, hawakuwa na bench players wengi ambao wanaweza kuingia na kuamua matokeo

2013/2014 Liverpool walikuwa kwenye kiwango bora sana baada ya kupitia kipindi kigumu in between chini ya mkufunzi Brendan Rodgers, team imara ilitengenezwa kumzunguka Luis Suarez, ilisifika kwa kufunga magoli mengi sana lakini ukuta wake wa biscuit ambao uliruhusu magoli mengi uliwagharimu... unaikumbuka Gerrad famous slip??

Kwa sababu hiyo mashabiki wengi wa Liverpool bado hawana imani thabiti kwamba team yao itatwaa tena ubingwa wa EPL licha ya kuwa juu kwa tofauti ya alama 4 dhidi ya Manchester City

2. Uzoefu kwenye mbio za ubingwa, ni rahisi kuwa na team nzuri ila sio rahisi kubeba ubingwa wa ligi kuu pale Uingereza, kwenye hatua za mwanzo hasa round ya kwanza unaweza kucheza mpira bila kuwa na presha yoyote na ukashinda mechi nyingi, lakini inapoingia round ya pili na upo kileleni unapatwa na presha kubwa ambayo inahitaji uzoefu flani ili kutoathirika na hicho kinakosekana kwa Liverpool, kwa hiyo mashabiki wa mpira wanaamini at some stage presha itawazidia Liverpool na watajikuta wanapoteza pointi na kumruhusu Manchester City kuutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo

KWA MAONI YANGU BINAFSI, LIVERPOOL WANA NAFASI KUBWA YA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, KWA SABABU HIZO HAPO CHINI

1. Team imara yenye wachezaji wengi wa kiwango cha Dunia (world class players),ndio Liverpool kwa sasa imetengenzwa na wachezaji wengi wazuri ambao wametengeneza muunganiko mzuri baina yao..kwenye nafasi ya ulinzi wana Allison, VVD na Robertson, hawa watatu ni nguzo imara kwenye safu ya ulinzi ambayo imeruhusu magoli machache zaidi kwenye ligi kuu nchini Uingereza (not more than 11 goals),Title is won by defense..wana watu wazuri katika ambao bado hawajaonyesha umahiri na kutambulika sana ila kazi yao ni maridhawa..kwenye safu ya ushambuliaji ni sehemu nyingine ambayo Liverpool wanajivunia..eneo hili wana Mohamed Salah, Firmino na Mane ambao wamecheza kwa pamoja kwa misimu miwili,hawa pamoja na Xherdan Shaqiri ndio msingi wa magoli ya Liverpool..utofauti wa hii team ya sasa na ya 2013/2014 ni ubora kwenye defense na hii ndio itakuwa sababu kubwa ya Liverpool kutwaa ubingwa

2. Wamebaki na michuano miwili, Liverpool wametolewa katika michuano ya EFL na FA cup, wamebaki na michuano miwili tu ambayo ni UCL na EPL, hii ni advantage kwao kwa sababu inawapa mda wa kutosha wa kufanya recovery after game na kufanya good preparation for the next game,kwa hiyo wanaingia kwenye game nyingine wakiwa na fresh legs contrary na mpinzani wao kwenye mbio za ubingwa ambaye yupo kwenye all four fronts, hii itampa City hasara over Liverpool

3. Jurgen Klopp, sifa moja kubwa ambayo inamfanya Klopp kuwa tofauti na makocha wengine ni kwamba hakupi mafanikio instantly, anachokifanya ni kutengeneza team nzuri na imara alafu hii team ndio iwape mafanikio, wakati anaichukua Liverpool huyu bwana alisema tumpe misimu minne ndio tuanze kuuliza makombe anayoipa Liverpool, wapo tupo kimya na mda wa kumtia kitanzi kwa kudai yale makombe umewadia..ila wakati anatoa kauli hii, niliamua kumsoma huyu jamaa na kupata historia yake vizuri wakati yupo Mainz na Borussia Dortmund, I was impressed,huyu aliipandisha Mainz daraja, huyu aliichukua Dortmund iliyochoka ambayo wakati anaichukua 2008 walikuwa nafasi ya 13 kama sio 14 alafu baadae akaja kubeba ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga back to back, huyu jamaa ndio silaha kubwa sana katika mbio za ubingwa...baada ya kutengeneza team imara sasa ndio wakati wake wa kutamba na kubeba makombe akianza na hili la ligi kuu, uzoefu wake kutoka kule Dortmund ndio silaha ya kuondoa presha kutoka kwa wachezaji wa Liverpool

4. Champions instincts, nikuibie siri tu, kila bwana anapata pointi nyingi kwa kushinda mechi nyingi ila kuna baadhi ya pointi zinapatikana kibahati sana, yes you need some lucky to gain title winning points, unakumbuka vs Everton wakati watu tushainuka kwenye viti tukiamini mechi imeisha??mimi nilikuwa nje ya ukumbi wa kuangalizia mpira, nilisikia shangwe za mashabiki humo ndani, kurudi nikakutana na habari ya Divok Origi, mpira ulikuwa unakwenda nje, Pickford anaurudisha ndani na Origi anakutana nao...siku hii Klopp alivamia uwanjani, hizi ndio points ambazo zinakupa ubingwa...vipi juzi na Crystal Palace golikipa Speroni anampa Salah goli?? BINGWA ANAHITAJI BAHATI KUPATA POINTI ZA KUMPA UBINGWA

#Steph

Sent using Jamii Forums mobile app
Man city Ndo wana world class hao Liverpool wakikosekana baadhi ya wachezaji tu tatizo
 
Hahaaaa our number 6 Kani-block IG lol

Yaah social media zinachanganya sana nahisi watu wameanza kuzitumia kuwatoa wachezaji wetu kwenye reli, majuzi walimzushia maneno Mane hadi nikashangaa Mane kaanza kuongea upuuzi hivi

LeBron James huwa playoffs zikianza anafunga mitandao yote kuziba kelele.

Na hata wenzake anawaambia wasimsimulie chochote watakachoona kumhusu.
 
Mo Salah deleted his all accounts kwenye Social Media!
Now Lovren will not exist any more coz he used him to get followers kwenye Social Media
 
123 Reactions
Reply
Back
Top Bottom