Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

DullyJr
LC amfunge Liverpool Anfield?
Liverpool isajili mchezaji mpya wa nn?Nafasi gani?
Hatuna haja ya kusajili mpya yyt na mapumziko haya ya siku 10 yatatumiwa vyema na LC anapigwa Anfield no matter nani atacheza na hata wao wanajua kama watapoteza
Mechi ngumu Liverpool ni tatu na ndiyo zitaamua ubingwa wetu,Man U,Spurs na Chelsea!Hizi mediocre teams Klopp kaisha zijulia zitasumbua tu kama CP lkn usiku zitakaa!
If we beat two of these three we are champs regardless of Man City results!!



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Liverpool have been linked with a massive double deal for Callum Hudson-Odoi and Timo Werner, according to German sources.

Newspaper Sport Bild have said that Chelsea starlet Hudson-Odoi is now on the Reds radar, while striker Werner could also be an option.

Odoi is shit, bring Werner in Reds.
 
Liverpool have been linked with a massive double deal for Callum Hudson-Odoi and Timo Werner, according to German sources.

Newspaper Sport Bild have said that Chelsea starlet Hudson-Odoi is now on the Reds radar, while striker Werner could also be an option.
hivi huyu Odoi mbona sioni ataleta nini zaidi ya tuluchonacho kwa Origi au Rhian,Wilson, Kent n.k

labda wamnunue kuja kuuza kama Solanke lakini Chelsi kuuza sio pungufu ya £38m na sio EPL proven or any big league...

huyu abaki huko huko.

Bring Werner.
 
On this day 100 years ago, the great Bob Paisley was born.

He is the most successful English football manager of all times. Having spent nearly half a century at Liverpool FC as a player, physiotherapist, coach and then manager.
IMG_20190123_125412_962.jpeg
images%20(18).jpeg
BJ61k4tCIAEklPM.jpeg
 
DullyJr
LC amfunge Liverpool Anfield?
Liverpool isajili mchezaji mpya wa nn?Nafasi gani?
Hatuna haja ya kusajili mpya yyt na mapumziko haya ya siku 10 yatatumiwa vyema na LC anapigwa Anfield no matter nani atacheza na hata wao wanajua kama watapoteza
Mechi ngumu Liverpool ni tatu na ndiyo zitaamua ubingwa wetu, Man U, Spurs na Chelsea! Hizi mediocre teams Klopp kaisha zijulia zitasumbua tu kama CP lkn usiku zitakaa!
If we beat two of these three we are champs regardless of Man City results!!



Sent from my iPhone using JamiiForums

Hapo Mimi naondosha Spurs ninaweka Everton coz Spurs ni wagumu mwanzo wa msimu tu lakini ikifika kuanzia kati ya msimu wanakuwa ni wa kawaida tu.

Na vilevile Spurs huwa hapati Matokeo Mazuri kwenye Anfield.

But Everton akihisi Liverpool anaelekea Ubingwa atapania kutaka kutukwamisha kama alivyotaka kifanya kwenye Mechi ya Kwanza.

Everton ni washenzi kweli wanapoiona Liverpool.
 
hivi huyu Odoi mbona sioni ataleta nini zaidi ya tuluchonacho kwa Origi au Rhian,Wilson, Kent n.k

labda wamnunue kuja kuuza kama Solanke lakini Chelsi kuuza sio pungufu ya £38m na sio EPL proven or any big league...

huyu abaki huko huko.

Bring Werner.
Kuna kila dalili anakwenda Bayen mana kakataa 85 kwa wiki kisingizio hakua akipangwa ha ha haa huko ameahidiwa mpaka jezi ya Roben hata mimi sikai

Haya mamboa ya kupuuza vipaji na kuwatenga sana ni mbaya sana.

Kocha wa Glujic huko anadai kama siyeye wangekua chini kabisa wa msimamo.

Ajabu kule Madridi naziona sura ngeni ambazo sizani kama ningeziona kwa kocha asie jiamini yan Close hayupo na tim ipo poa kabisa

Makinda ni muhimu sana wanapunguza ghalama Suso alikua poa sana tim alipo ndo inamuangusha kwa sasa kuna kijana kapewa jezi 10 Lazio yuko vizuri nazani hakupewa muda pia hakupangwa mahali apendapo.
Hili lakupangwa sehem usio ipend tunaipuuza tu ila inawakera sana wachezaji Pogba amekua mfano hai wasioweza kutamka wakipangwa hucheza chini ya kiwango maksudi ajabu walimu walimu wananunua wachezaji wa aina moja wakilazimisha kuwapanga wapendapo.

Salah anakua bora sana akiwa kulia anapangwa kati Mane amezoea kuwa kushoto juzi kapangwa kulia ili Keita acheze kushoto na alivyotoka tuliona Mane alirudi kushoto na kufanya jambo muhimu.

Namuombea mema Santigo Sorari kwa nilicho ona juzi na Sevila
 
Itakuwa backlashes za diving, just thinking.

Hahaa diving, No haziwezi mvuruga hivyo

Wengine wasa speculate wanasema eti ni kwasababu anakuwa linked na Madrid

Labda kila mtu na jambo lake ila wengi waliihusisha last tweet yake na kutaka ku-solve disputes na Egyptian FA

All in all yeye ndo anajua zaidi
 
Hahaa diving, No haziwezi mvuruga hivyo



Labda kila mtu na jambo lake ila wengi waliihusisha last tweet yake na kutaka ku-solve disputes na Egyptian FA

All in all yeye ndo anajua zaidi
Okay, hope siyo distraction kwake.
Ni jambo jema naona kwa team yetu maana hatakuwa na sehemu ya ku consume negativity.

Kama mnakumbuka ile incidence ya Lovren kuedit profile yake ya Insta kisa matusi ya mashabiki waliokuwa wamemchoka.

So ni dhahiri hawa wachezaji huwa wanasoma comments na ni dhahiri last weekend kulikua na influx ya matusi na kejili kwenye social media accounts za Mo.

Good thing for him and Liverpool as a whole.
 
Ni jambo jema naona kwa team yetu maana hatakuwa na sehemu ya ku consume negativity.

Kama mnakumbuka ile incidence ya Lovren kuedit profile yake ya Insta kisa matusi ya mashabiki waliokuwa wamemchoka.

So ni dhahiri hawa wachezaji huwa wanasoma comments na ni dhahiri last weekend kulikua na influx ya matusi na kejili kwenye social media accounts za Mo.

Good thing for him and Liverpool as a whole.

Hahaaaa our number 6 Kani-block IG lol

Yaah social media zinachanganya sana nahisi watu wameanza kuzitumia kuwatoa wachezaji wetu kwenye reli, majuzi walimzushia maneno Mane hadi nikashangaa Mane kaanza kuongea upuuzi hivi
 
Ni swali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza, swali hili limepata uzito siku za hivi karibuni kutokana na sababu kuu mbili

1. Historia ya Liverpool kutobeba ubingwa kwa miaka 29,mara ya mwisho majogoo walibeba taji la ligi kuu mwaka 1990,wamejaribu mara kadhaa kupambana kwa ajili ya taji hilo ila wameishia kumaliza nafasi ya pili,miaka ya hivi karibuni Rafael Benitez(2008/2009) alichuana vikali na Manchester United ya babu lakini aliambulia patupu, kipindi hiki alikuwa na watu bora sana kama Fernando Torres, Javier Mascherano,Steven George Gerrad, Dirk Kuyt, ulikuwa msimu mzuri sana kwa Liverpool licha ya kuukosa ubingwa,kilichowagharimu kipindi hili ilikuwa ni kukosa squad imara, hawakuwa na bench players wengi ambao wanaweza kuingia na kuamua matokeo

2013/2014 Liverpool walikuwa kwenye kiwango bora sana baada ya kupitia kipindi kigumu in between chini ya mkufunzi Brendan Rodgers, team imara ilitengenezwa kumzunguka Luis Suarez, ilisifika kwa kufunga magoli mengi sana lakini ukuta wake wa biscuit ambao uliruhusu magoli mengi uliwagharimu... unaikumbuka Gerrad famous slip??

Kwa sababu hiyo mashabiki wengi wa Liverpool bado hawana imani thabiti kwamba team yao itatwaa tena ubingwa wa EPL licha ya kuwa juu kwa tofauti ya alama 4 dhidi ya Manchester City

2. Uzoefu kwenye mbio za ubingwa, ni rahisi kuwa na team nzuri ila sio rahisi kubeba ubingwa wa ligi kuu pale Uingereza, kwenye hatua za mwanzo hasa round ya kwanza unaweza kucheza mpira bila kuwa na presha yoyote na ukashinda mechi nyingi, lakini inapoingia round ya pili na upo kileleni unapatwa na presha kubwa ambayo inahitaji uzoefu flani ili kutoathirika na hicho kinakosekana kwa Liverpool, kwa hiyo mashabiki wa mpira wanaamini at some stage presha itawazidia Liverpool na watajikuta wanapoteza pointi na kumruhusu Manchester City kuutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo

KWA MAONI YANGU BINAFSI, LIVERPOOL WANA NAFASI KUBWA YA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, KWA SABABU HIZO HAPO CHINI

1. Team imara yenye wachezaji wengi wa kiwango cha Dunia (world class players),ndio Liverpool kwa sasa imetengenzwa na wachezaji wengi wazuri ambao wametengeneza muunganiko mzuri baina yao..kwenye nafasi ya ulinzi wana Allison, VVD na Robertson, hawa watatu ni nguzo imara kwenye safu ya ulinzi ambayo imeruhusu magoli machache zaidi kwenye ligi kuu nchini Uingereza (not more than 11 goals),Title is won by defense..wana watu wazuri katika ambao bado hawajaonyesha umahiri na kutambulika sana ila kazi yao ni maridhawa..kwenye safu ya ushambuliaji ni sehemu nyingine ambayo Liverpool wanajivunia..eneo hili wana Mohamed Salah, Firmino na Mane ambao wamecheza kwa pamoja kwa misimu miwili,hawa pamoja na Xherdan Shaqiri ndio msingi wa magoli ya Liverpool..utofauti wa hii team ya sasa na ya 2013/2014 ni ubora kwenye defense na hii ndio itakuwa sababu kubwa ya Liverpool kutwaa ubingwa

2. Wamebaki na michuano miwili, Liverpool wametolewa katika michuano ya EFL na FA cup, wamebaki na michuano miwili tu ambayo ni UCL na EPL, hii ni advantage kwao kwa sababu inawapa mda wa kutosha wa kufanya recovery after game na kufanya good preparation for the next game,kwa hiyo wanaingia kwenye game nyingine wakiwa na fresh legs contrary na mpinzani wao kwenye mbio za ubingwa ambaye yupo kwenye all four fronts, hii itampa City hasara over Liverpool

3. Jurgen Klopp, sifa moja kubwa ambayo inamfanya Klopp kuwa tofauti na makocha wengine ni kwamba hakupi mafanikio instantly, anachokifanya ni kutengeneza team nzuri na imara alafu hii team ndio iwape mafanikio, wakati anaichukua Liverpool huyu bwana alisema tumpe misimu minne ndio tuanze kuuliza makombe anayoipa Liverpool, wapo tupo kimya na mda wa kumtia kitanzi kwa kudai yale makombe umewadia..ila wakati anatoa kauli hii, niliamua kumsoma huyu jamaa na kupata historia yake vizuri wakati yupo Mainz na Borussia Dortmund, I was impressed,huyu aliipandisha Mainz daraja, huyu aliichukua Dortmund iliyochoka ambayo wakati anaichukua 2008 walikuwa nafasi ya 13 kama sio 14 alafu baadae akaja kubeba ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga back to back, huyu jamaa ndio silaha kubwa sana katika mbio za ubingwa...baada ya kutengeneza team imara sasa ndio wakati wake wa kutamba na kubeba makombe akianza na hili la ligi kuu, uzoefu wake kutoka kule Dortmund ndio silaha ya kuondoa presha kutoka kwa wachezaji wa Liverpool

4. Champions instincts, nikuibie siri tu, kila bwana anapata pointi nyingi kwa kushinda mechi nyingi ila kuna baadhi ya pointi zinapatikana kibahati sana, yes you need some lucky to gain title winning points, unakumbuka vs Everton wakati watu tushainuka kwenye viti tukiamini mechi imeisha??mimi nilikuwa nje ya ukumbi wa kuangalizia mpira, nilisikia shangwe za mashabiki humo ndani, kurudi nikakutana na habari ya Divok Origi, mpira ulikuwa unakwenda nje, Pickford anaurudisha ndani na Origi anakutana nao...siku hii Klopp alivamia uwanjani, hizi ndio points ambazo zinakupa ubingwa...vipi juzi na Crystal Palace golikipa Speroni anampa Salah goli?? BINGWA ANAHITAJI BAHATI KUPATA POINTI ZA KUMPA UBINGWA

#Steph

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom