Lee
JF-Expert Member
- Jul 31, 2013
- 44,001
- 150,526
Liverpool wanahitaji kucheza kama hawatocheza tena, vivyo hivyo kwa SS Napol. Inawezekana Liverpool wanauhitaji mkubwa sana wa alama tatu(3), ila pengine SS Napol wanauhitaji mkubwa zaidi wa alama moja(1).Hizi Rekodi Zimewekwa Kwa Ajili Ya Kuvunjwa!
Hata Stoke City, Crustal Palace na West Bromwich Albion Wakati anakuja Klopp Liverpool ushindi wetu kwao ulikuwa Ni Draw, tena hiyo Draw tunaweza kuipatia Anfield na si Away lakini tukapambana mpaka tukaondosha Rekodi za Uteja Kwao.
Sasahivi Hao wote tunapiga Nje Ndani.
Kwahiyo na Huyo Refa Bundi wake tunamchoma Mishkaki Leo usiku na Kumlia Ugali.
Kitu kizuri kwa Liverpool ni kuwa mchezo huu wanaucheza nyumbani(Anfield).... Home ground mentality imekuwa nzuri kwa Liverpool na kitu pekee chakuchunga kwao ni kutowaruhusu Napol kupata goli, kwamaana ya kwamba Liverpool inahitaji alama 3 na clean sheet juu.
Ni fainal kwa Liverpool kabla ya fainal. Sina shaka na current form ya Liverpool kwa sasa ila ninashaka na form ya Liverpool kwenye champions league. Wanachokihitaji ni kufanya Shift tu ya kuuhamisha ubora wa kwenye EPL kuupeleka Champions League.