Alisson Becker ni kipa mmoja ambae tumeokota dodo kwenye mchongoma.
Nimejaribu kuangalia highlights za mechi ya jana nimegundua Alisson kwa sasa hana mpinzani duniani.
Goli letu la tatu lilitokea kwenye kona ya Burnley baada ya piga nikupige Alisson aliokoa mchomo ambao kwa type ya Karius pale jana mechi ingeisha 2-2..
Baada ya beki kuosha mpira haukuenda mbali ukaangukia miguuni mwa Burnley na shambulizi likawa bado lipo on, ikapigwa cross ambayo ilifanyiwa deflection na Salah na ilionekana kabisa inaenda kuwa kona ila Alisson (akiwa under pressure) akaokoa mpira usiwe kona na akauweka kwenye himaya yake.
Sasa tuje kwenye point; Jiweke wewe au kipa mwingine average kama Arizibagabaga kwenye nafasi ya Alisson, team inaongoza 2-1, umetoa mchomo na umeokoa mpira umeuweka kwenye himaya yako. Wakati huo zimesalia sekunde kama 40 mechi kuisha..
Aisee pale nauhakika makipa asilimia 98+ wangelala na kuchukua sekunde zao tano sita ili game iishie 2-1.
Lakini huyu sio kipa wa kawaida, huyu sio De Gea wala sio Leno wala sio Arizibagabaga. Huyu ni Alisson Becker wenyewe wanamwita Ali Hassan Bakari mtoto wa Mwananyamala kwa Kopa.
Kipa mchezaji a.k.a kipa mchezeshaji a.k.a kipa mshambuliaji.. Kutokana na kuwa na jicho kama la Coutinho aliona nafasi ya goli la tatu tofauti na makipa wengine ambao wangeona nafasi ya kupunguza kufungwa goli la pili na kulalia mpira kama yai.
Alisson akamchungulia DS15 nae bila hiyana kwa MS11 kisha kwa Big Shaq and Boom..
Ushujaa wa Alisson akaukamiliza kwa kuizawadia Liverpool goli la tatu.. Ndio goli amefunga Shaqiri lakini kwa wenye jicho na akili ya soka Alisson alicheza kama Pele.
Tuifufue ile form yetu ya last season pale mbele tu na hatuhitaji kuombea team fulani iifunge fulani ili sisi tuwe kwenye nafasi nzuri ya kubeba EPL. Tutaenda sisi kama sisi, mechi moja baada ya nyingine.
Come On Reds.
You'll Never Walk Alone.

Chaliifrancisco