Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Besiktas wanataka kuturudishia mzigo wetu Karius. Yani hata wao umewashinda.

Lakini nini kimeenda kombo na Karius?

Alipokuwa Mainz alikuwa ni moja ya makipa bora kabisa katika league, kupitia gazeti maarufu la michezo la Kicker alichaguliwa kuwa kipa namba mbili kwa ubora nyuma ya Neuer katika Bundesliga.

Alikuwa ameokoa penati nne kati ya saba zilizopigwa langoni mwake katika mechi mbalimbali lakini sasa kageuka kuwa "kituko". Tulidhani tukimtoa kwa mkopo itasaidia kurejesha imani na kujiamini kwake lakini bado.

Hata huko Besiktas hafanyi vema kiasi kwamba wanataka kukatisha mkopo.

Nahofia hili ni anguko lake. Anazidi kumomonyoka kisaikolojia kiasi kwamba hataweza tena kung'aa.
 
Sikuwahi kumuamini Karius mbele ya Mignolet!



Huyu jamaa kilichompoteza ni kutokujifunza kupitia makosa yake yani kama unakumbuka alishapigiwa shuti na Kolarov kama la bale alilazimisha kumeza ikaenda kwenye post mashabiki wakalalamika lakini jamaa hakubadirika....


Mdogo mdogo akatujengea imani wana liver japokuwa bado aliendeleza viujinga vyake lakini havikuwa na madhara sana kutokana na vile vipigo vikubwa vikubwa tulikuwa tukivitoa ukichanganya na ujio wa VVD...




Fainali anakuja kufanya upuuzi ambao hata Ramadhani Kabwili awezi kuufanya na ukicheki alivyopigiwa kelele ni halali jamaa apotee na anahitaji msaada wa kisaikolojia ikiwezekana aachane na soka kabisa kabla ajafa kwa msongo wa mawazo!!
 
maneno mengi hayo Sari kombe hana...Klopp akiwa Dortmund na ushindani na utajiri wa Bavarians alichukua.....
Sarri ni kamari mlicheza na so far anawapeleka vizuri..
 
everyone is replaceable, hakuna aliejuu ya timu hivyo wakiona anagoma wamuuze mapema mkwaja wa kueleweka sio kukubebeleza inafika kama Can au Ledowski anaodoka bure...
 
League goals conceded since Virgil van Dijk made his league debut for LFC :

Real Madrid - 44 (!!!!)
Barcelona - 32
ManUtd - 30
Bayern - 27
ManCity - 17
Juventus - 16
Atletico - 14
Liverpool - 14

Malizia na Trophies won since VVD made his league debut for LFC:

Real Madrid -
Barcelona -
ManUtd -
Bayern -
ManCity -
Juventus -
Atletico -
Liverpool -
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…