Jamaa kalewa sifa I'm telling you, jinsi anavyocheza sio kwa kujitoa na juhudi kama anavyojitoa Sadio. Nimeiona mipira mingi ambayo Salah angeiintercept lakini hakufanya hivyo, amekuwa ni mpotezaji mipira halafu hatumii nguvu kuikaba and the likes
Aisee sifa mbaya sana! Waarabu wamemsifia sana pamoja na Dunia mpaka jamaa akalewa and sometimes nikawa nafikiri labda style anayoplay sasa hivi ni anafanya hivyo ili asiangukie kwenye majeruhi ama Lah?
Firmino amekuwa ni mtu anaecheza kwa kujitoa na ubunifu tofauti na jamaa yetu wa Misri, italeta maswali kama goli la Firmino ambalo ni la ushindi tena katika dakika ya 90+1 halafu jamaa akasirike ukizingatia yeye ni mchezaji tena wa Liverpool????????????????????????????????
Jamanieee nyie mnaoleta hizi mada kuwa Salah alikasirika wakati mmeona tu scene ikimalizikia hamjajua kabla ya kuitupa hiyo chupa chini alifanyaje.
Jamaa alishangilia mikono yote miwili hewani kisha baada ya hapo ndio akaitipitilia mbali chupa kwa furaha.
Sasa kwa kuwa wengi mmeona hapo alikuitupilia chupa chini na hamkuona mwanzo wa tukio ndio mnaleta mambo ya ajabu.
Hivi Salah professional kabisa hata kama hakufurahia goli la Bobby anaweza kufanya hizo antics kwenye bench pale? Anajua kabisa kuna camera na watu mamilioni wanaangalia?
Siwezi kuamini kama mtu mwelewa yoyote atasema eti Salah alichukia kisa Bobby kafunga, kwahiyo mnamaanisha Salah alitaka tusipate matokeo?. Haya maneno ni yenu huku kwenye mitandao tu. Huku ndipo mnapokuza mambo kinyume na uhalisia ulivyo.
Kabla hamja judge kitu tulizeni akili msikurupuke kuanza kuhukumu kwa mambo msiyokuwa na ushahidi nayo. Mbona Klopp alikua mbele ya Salah kwenye touch line na alimgeukia kabisa wakati Salah anaitupa hiyo chupa? Unadhani Salah anaweza kuwa unprofessional kiasi hicho mpaka afanye kitendo cha kuchukia team yake inapofunga goli?
Sometimes tushirikishe bongo zetu bana kwenye haya mambo.
KWA UPANDE MWINGINE: KUHUSU SUALA LA MANE KUTOMPASIA SALAH
Hizi hate campaigns zinazoanzishwa na fanpages za Salah na Mane kwenye mitandao ndio zinaleta chuki kwa mashabiki wakati kiuhalisia wala Salah na Mane hawana beef yoyote maisha yanaenda sana tu tena ni mabest wakutupwa.
Wanalalamika Mane hampasii Salah, sawa hakumpasia alijaribu kugunga yeye mwenyewe kwakuwa aliona ana uwezo wa kufunga lakini bahati mbaya hakufanikiwa (hii ni kawaida katika mpira).
Au alijaribu kumpasia mtu mwingine labda akafunga au akakosa (nayo ni kawaida kwenye mpira). Kama asingempasia na yakawa magoli msingefurahi? Kwakuwa hatukufanikiwa kufunga basi ndio mnalalamika. Kwani mara ngapi Salah amepasiwa nafasi za wazi na akakosa?
Tatizo wa mashabiki wengi wa Salah sio mashabiki wa Liverpool wao wanampenda tu Salah na ikitokea hajafunga wataanza kutafuta sababu zao za kipuuzi puuzi tu ilimradi ionekane Salah anaonewa. Wao shida yao sio Liverpool kushinda mechi bali waone mchezaji wao akifunga magoli. Wanashindwa kutambua kuwa mpira ni mchezo wa kitimu zaidi kuliko individual glory.
Mimi sio kwamba simpendi Salah, Salah nampenda sana kama wachezaji wengine wa Liverpool. Lakini kuna baadhi ya watu wanataka kutuvurugia team yetu kisa mapenzi yao kwa mchezaji mmoja mmoja.
Tuachieni team yetu, hizo maneno zenu kaeni nazo. Hatutaki kuingiliwa kwenye mambo yetu. Haijalishi kafunga Alisson au Robertson. Ilimradi Liverpool inshinda mechi sisi tunafurahi. Hata Salah asipofunga au Firmino au Mane. Haijalishi ilimradi Liverpool inashinda mechi.
Hata tukishinda kwa OGs sisi cha muhimu ushindi. Haya mambo ya kutafua sifa binafsi ambayo yanachochewa na mashabiki uchwara wapelekeeni akina Harry Kane huko wanaogombaniana hadi penalty.
We Go Again.
We Are Liverpool. This Means More.
You'll Never Walk Alone

ChaliiFrancisco