ROBERTO FIRMINO, FOWADI MWENYE ASILI YA MAKELELE.
Na Haatim Abdul
Wakati watu wanafurahia mabao ya Mohammed Salah msimu huu nadhani ni wakati wa kutambua pia uwezo na mchango wa Roberto Firmino pale Liverpool. Roberto Firmino ni fowadi wa kipekee katika uchezaji wake lakini tena uwezo wake haupewi sifa stahili pale England wazungu wanasema "Underrated".
Ni wachezaji wachache duniani ambao wangeinufaisha Liverpool hivi afanyavyo Firmino hata Salah hawezi pia. Kuna kitu cha kipekee ambacho anakileta kwenye timu ambacho kimemfanya atajwe kama mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho kwa miaka kadhaa iliopita. Firmino ni defensive forward kwa maana ya mshambuliaji wa Ulinzi.
Katika miaka 130 ya historia ya mchezo wa mpira wa miguu narudia katika historia hakuna mshambuliaji yoyote kwenye soka aliewahi kufunga mabao 30, kufanya tackles 50+ na interceptions 60+ kwenye mashindano yote kwenye msimu mmoja. Hebu jiulize huyu fowadi ana muda gani wa kufunga magoli na mchango wake kwenye ulinzi ni huo hapo. Na tangu atue Liverpool amefanya tackling na interception nyingi kuliko hata nahodha wake, Jordan Henderson ambae ni kiungo wa kati.
Roberto Firmino ni mzaliwa wa Brazil eneo la Maceio, Alagoas. Alijiunga na timu ya vijana ya Figueirense akiwa na miaka 17 tu mwaka 2008. Daktari wa meno Marcellus Porteilla aligundua kipaji chake na Firmino alitumika kama kiungo mkabaji sikuizi tunaita mkata umeme. Firmino alikuwa mkata umeme huko Brazil na haishangazi akafunga mabao 8 kwenye mechi 36 za timu hiyo.
Bobby alifanya kutumika tu kama Defensive Midfielder mapema kabisa kwenye mpira wake licha ya kwamba kiasili ni mshambuliaji lakini ana uwezo mkubwa wa kukaka na Liverpool kwa sasa wanafaidika na Bobby mkata umeme wa Figueirense na huyu namba 9 muongo wa Liverpool. Hapa ndipo Firmino anapobaki mchezaji muhimu zaidi kwenye pressing ya Jurgen Klopp.
Firmino sio mshambuliaji ambae ataongoza chati za wafungaji, hana misuli ya kina Costa, wala mashuti ya Ibrahimovich, sio mpiga vichwa hatari kama Morata lakini Bobby ni wa kipekee sana. Ni mchanganyiko wa Bobby na mtu kama Casemiro wakati huo huo. Yani Casemiro au Kante angekuwa mshambuliaji basi angekuwa kama huyu jamaa.
Tangu atue Liverpool amefanya zaidi ya tackling 160 na zaidi ya Interceptions 60. Huyu ni beki ndani ya mshambuliaji. Ndio anaifanya kazi ya Liverpool kuwin mipira kule mbele iwe rahisi sana. Huyu hasa ndio Mr. Gengenpressing pale Liverpool. Ndio mchezaji anaeuelewa zaidi mfumo wa Klopp unahitaji nini. Na ndio mchezaji muhimu zaidi pale Liverpool. Mwenyewe Klopp amemwita "Injini".
Kazi anayoifanya Firmino pale Liverpool hakuna mchezaji mwingine yoyote mwenye uwezo wa kuifanya, kukaba na kushambulia. Kuongoza kwenye tackles na interceptions na bado ukafunga na kutoa pasi za goli. Historia haijapata mshambuliaji mwenye takwimu kama za Bobby.
Anakimbia, hachoki na anautafuta mpira baada ya kupokonywa kama mtoto alieporwa chapati. Anawin mpira na anawapa wenzie wamalize kazi. Huyu ndio Roberto Firmino Barbosa De Olivieira. Fowadi mwenye asili ya makelele. Fowadi wa kipekee kwenye soka.