Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Since the arrival of Jürgen Klopp tulikuwa tukilalamika Kwamba Ni lazima Timu itafutiwe Talented Striker ambaye Ni Natural No 9 lakini Some Fans walikuwa WanatuCriticize na KuClaim Kuwa Kutokana na attacking force yetu hatuhitaji Striker.

Lakini Game ya Jana Baada ya Salah Kuto Kucheza pamoja na Hile ya Burnley zimeprove right kwa tunayoyasema Ni Sahihi Kwani Ushindi wetu umekuwa Ni Wa Kunyemelea tu
.

Kiukweli Salah amekuwa Akitubeba sana Kiasi Ya Kwamba Asipokuwemo Yeye Timu Yetu Katika ufungaji inakuwa Ni Shit.

Kwahiyo Salah Hatokuwa Mzima Siku Zote Ni Wazi Kuwa Timu inahitaji Mfungaji Wa Uhakika ili anapokosekana Salah Yeye Ndiye awe Goal Scorer
..

Still nasimamia Hoja yangu Kuwa Firmino Ni False 9 na si mfungaji Wa Kutumainia Bali Ni Creator Midfielder Wa Kutumainiwa.
 
SAKATA la usajili wa Philippe Coutinho kwenda Barcelona bado pasua kichwa. Wahispaniola hao wanaamini watampata Mbrazili huyo kwenye dirisha hili la Januari.

Staa huyo wa Liverpool jana Ijumaa aliaminika kwamba alicheza mechi yake ya mwisho wakati walipomenyana na Everton kwenye Raundi ya Tatu ya Kombe la FA.

Liverpool itavuna pesa nyingi tu kwenye mauzo ya mchezaji huyo na sasa kazi itakuwa kwa Jurgen Klopp kupata mtu wa kuziba pengo lake. Itabidi Liverpool irudi tu kwa mastaa hawa kujisalimisha ili kufuta kabisa pengo litakaloachwa na Mbrazili huyo.
 
Thomas Lemar (Monaco)

Liverpool ilitaka kumsajili Lemar tangu Agosti mwaka jana na hata alitumiwa ndege kwa ajili ya kumsafirisha hadi Paris kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya, lakini dili hilo liligoma dakika za mwisho, akabaki AS Monaco kwa sababu iligoma kumuuza kwa ilishauza wakali wake kadhaa.

Kwa sasa haina jinsi kwenye dirisha hili la Januari itabidi tu Liverpool iende tena huko Monaco kuulizia huduma yake kutokana na ishu inayomhusu staa wao, Coutinho kutakuwa huko Barcelona. Lemar bado kijana mdogo, umri wake wa miaka 22 unamfanya awe na muda mrefu wa kuitumikia timu yoyote itakayofanikiwa kupata huduma yake.

Julian Draxler (PSG)

Alikuwa mmoja mastaa matata sana ndani Ulaya kipindi hicho alipokuwa Wolfsburg. Januari ya mwaka jana, Liverpool ilihitaji kumsajili Mjerumani huyo ili kuboresha safu yake ya ushambuliaji, lakini ilishindwa na staa huyo akatimkia PSG msimu ulipomalizika.

Lakini miezi 12 imepita sasa na Liverpool inaweza kurudi tena kwa staa huyo kutaka kumsajili. Draxler maisha yake si mazuri huko PSG baada ya kucheza dakika zote 90 kwenye mechi tatu tu msimu huu.

Kwenda Liverpool kitakuwa kitu muhimu kwake kwa sababu anapata muda wa kucheza kwenye kikosi hicho cha Anfield.

Alexis Sanchez (Arsenal)

Mwaka 2014, Liverpool ilifanya jaribio la kutaka kumsajili Alexis Sanchez kabla ya kuzidiwa kete na Arsenal na mchezaji huyo kutimkia Emirates. Lakini, kwa sasa ndani ya Januari hii, Liverpool inaweza kurudi tena kwa staa huyo wa Chile kwenda kuulizia huduma yake kutokana na kupiga hesabu za kuondoka Arsenal.

Liverpool inafahamu wazi pesa tu ndiyo itakayoifanya Arsenal kukubali kumpiga bei fowadi wake huyo kwenye dirisha hili la Januari kuliko kusubiri mwishoni mwa msimu kumuona akiondoka bure.

Manchester City na PSG zinahitaji pia huduma ya fowadi huyo wa zamani wa Barcelona.
 
Yannick Carrasco (Atletico Madrid)

Kiwango cha Mbelgiji huyo kimekuwa kikikuwa siku hadi siku tangu alipoanza kucheza kwenye kikosi cha Atletico Madrid ya Diego Simeone.

Tangu msimu uliopita, Carrasco amekuwa sehemu muhimu kabisa ya kikosi cha Atletico akicheza mechi 53. Msimu huu amekumbana na balaa la kuumia goti Oktoba mwaka jana na baada ya hapo bado hajarudi katika ubora wake ule wa awali. Staa huyo ataipa Liverpool machaguo yote kwenye sehemu ya mbele, akicheza kushoto au kulia na wakati mwingine anaweza pia kucheza katikati jambo litakalomfanya Klopp kuingiza mtu muhimu kabisa kwenye kikosi chake.

Manuel Lanzini (West Ham)

Licha ya Wilfried Zaha na Riyad Mahrez ndiyo wanaonekana kuwa ni wachezaji bora zaidi kwenye Ligi Kuu England kwa wakali wasiokuwa wa timu za Top Six, lakini hakuna ubishi Lanzini ndiye mwenye kiwango kinachofanana na Coutinho. Staa huyo miguu yake imejaa ufundi mkubwa na hakika ni mchezaji anayevutia kumtazama wakati mpira unapokuwa kwenye miguu yake.

Ubora wa Lanzini unaonyesha ni mchezaji anayeweza kuboresha kiwango chake na kuwa msaada kama atakwenda kuichezea Liverpool.

Christian Pulisic (Borussia Dortmund)

Ni mmoja kati ya wachezaji wenye viwango bora kabisa barani Ulaya kwa sasa, akifunga mabao kama anavyopenda na kuwa mchezaji mwenye hadhi kubwa.

Liverpool ikipata huduma yake itakuwa imefanya kitu cha maana kwelikweli kwa sababu itavuna mengi mazuri kutoka kwake.

Klopp amekuwa akivutiwa sana na mchezaji huyo, lakini alichoambiwa na Borussia Dortmund, Pulisic hauzwi.

Lakini kwa sababu mambo yanaweza kuwa tofauti, kama Liverpool ikipata pesa za kumuuza Coutinho, basi haitakuwa na kisiki chochote mbele yake itakapohitaji mchezaji, pesa itakuwa inaongea.

Nabil Fekir (Lyon)

Chaguo jingine ambalo Klopp anaweza kulifanya katika kuziba pengo la Coutinho ni kumsajili Fekir.

Kiwango cha staa huyo kipo wazi kiasi cha kuivutia hadi Real Madrid ya Zinedine Zidane. Takwimu za Fekir zinavutia kwelikweli, amefunga mabao 13 katika mechi 16 za Ligi Kuu alizocheza msimu huu.

Fekir amefunga mara mbili pia kwenye Europa League na moja ya mabao yake aliifunga Everton. Fekir atakuwa msaada mkubwa kwenye kikosi hicho kama Klopp atafanikiwa kuipata huduma yake.
 
Firmino aingia Matatani Kuhusu Maneno aliyomtupia Holgate Beki Wa Everton Katika Mchezo Wa Jana!
FA inachunguza ikiwa maneno hayo Ni ya Kibaguzi ama Si ya Kibaguzi.
 
Huenda issue Ya Coutinho kwenda Barcelona ikawa Deal Done Coz Kikosi Cha Liverpool Leo Kimeondoka Kwenda [HASHTAG]#Dubai[/HASHTAG] Kwa Ziara Ya Kimazoezi Na Coutinho ameachwa Hakujumuishwa Katika Kikosi Hicho...

 
Van dijk pesa inaongea.. Jamaa has been dreaming for.Liverpool .... He is in the right place..
Ka link up vizur

We all know merseyside derby n ngumu sana. so sitegemei mtu kudai leo clean sheet.. Cha msingi n hii win

Ila klopp ajfkrie tena.. Hawa Goalkeepers sio wa kwenda nao Champions League.. wanadaka kwa kubahatisha.. its a fact
Halafu yule solanke anakipi mpaka anampanga hata kwenye mechi ngumu mbona mimi namuona hata under 23 hafiti?
 
Coutinho to fc barca is a done deal according to sky sports spanish football expert Guillem ballague
 
SAKATA la usajili wa Philippe Coutinho kwenda Barcelona bado pasua kichwa. Wahispaniola hao wanaamini watampata Mbrazili huyo kwenye dirisha hili la Januari.

Staa huyo wa Liverpool jana Ijumaa aliaminika kwamba alicheza mechi yake ya mwisho wakati walipomenyana na Everton kwenye Raundi ya Tatu ya Kombe la FA.

Liverpool itavuna pesa nyingi tu kwenye mauzo ya mchezaji huyo na sasa kazi itakuwa kwa Jurgen Klopp kupata mtu wa kuziba pengo lake. Itabidi Liverpool irudi tu kwa mastaa hawa kujisalimisha ili kufuta kabisa pengo litakaloachwa na Mbrazili huyo.

Huenda issue Ya Coutinho kwenda Barcelona ikawa Deal Done Coz Kikosi Cha Liverpool Leo Kimeondoka Kwenda [HASHTAG]#Dubai[/HASHTAG] Kwa Ziara Ya Kimazoezi Na Coutinho ameachwa Hakujumuishwa Katika Kikosi Hicho...


Done deal
Screenshot_20180106-202213.png
 
All your reaction to the breaking
Coutinho story on our live blog this
afternoon- and this man wishes him
all the best
 
Nakutakia mafanikio mema Coutihno ingawa kwa wazi kabisa umepishana na mafanikio makubwa yatakayo fika!
Klopp tuletee kipa Oblak au Allison tuanze kuchukuea tena EPL yetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom